Kati ya watu mil 67 wanaoishi hapa Tanzania wamekubali na kusema kuwa jezi alizotengeneza Sandaland kwa mkataba halali ni nzuri na zinafaa.
Ila mtu mmoja tu ambaye ni waziri anadai kwenye macho yake ni mbaya na hazifai.
Kuna nini? Kuna ka ten pasenti kamempita kushoto?
Kwanza, WaTanzania ni zaidi ya 70M WaTanganyika wakiwa wengi zaidi.
Pili, ni kweli wala si UONGO. Jezi zile ni mbaya kuanzia ubunifu hadi rangi. Wengine watasema zimeakisi bendera ya TANZANIA, mimi nitabisha mbingu na ardhi!
Hatuna rangi ya njano wala nyeupe kwenye bendera. Na hata bluu iliyopo kwenye bendera ni tofauti kwenye jezi!
Hapo nakubali jezi ni MBAYA. Na huo ulikuwa msimamo wangu toka kipindi cha Maxio Maximo timu ilipoanza kucheza soka la kueleweka.
Tatizo WaTanzania wengi wanachukulia mambo poa na kishabiki oya oya!
Sikutaka kumjadili Daudi Albert Bashite maarufu kama Paulo Makonda kwa sababu zilizo wazi kabisa. Hana ana akili timamu... Ni chawa mbabaishaji mwenye nyodo, dharau, chuki, ubinafsi, ukatili na utemi! He is a psychopath, populist and bully. Kifupi Bashite hana sifa za kiongozi wa chochote!
Sakata la jezi wala halikuwa jambo la kulete taharuki wiki mbili mfululizo... Na huo ni uthibitisho kuwa hana akili za kujua majukumu yake. Zaidi ya yote hana uwezo wa kutengeneza teamwork ofini kwake!
Sitaki kuamini hajui matokeo ya anachokifanya. Ukifuatilia kwa ukaribu na kwa kauli zake mwenyewe unabaini yafuatayo:
1. Dharau/ubinafsi: kama naibu alihusika na yeye alitaka Rais wake ndo ahusike si wangesawazisha huko ndani? Pengine tatizo ni unaibu! Alafu muonekano wa mwanasheria wa Sandaland ulihusikaje kwenye ufafanuzi wake?
2. Ana maslahi binafsi: kama suala ni Nike etc si angewalete rasmi na kuwakutanisha na wadau, Sandaland, TFF, etc?
3. Matumizi mabaya ya madaraka
4. Alitaka a-trend kumfunika Tundu Antipas Lissu na kuhamisha upepo wa Eda.
Mimi ni mwanafunzi na muumini wa elimu na weledi!
Sijui kwanini Sandaland hakusubiri subiri hadi avunjiwe mkataba rasmi. Hii ingesababisha incurable brand damage. Pengine na yeye ni chawa promax!