Arusi zilizostaarabika,huwa msosi ukiishaandaliwa hutolewa tangazo kwenda kujisevia mtu kipimo anachotaka.
Kunakuwa na msimazi tu ambaye hagawi, kazi yake ni kuangalia usalama wa vyombo na vyakula, kazi ya kujipakulia ni ya kila mtu kujikadiria atakavyo yeye.
Na huku kwenye vinywaji ni mwendo wa coctail tu, vinywaji kujazwa mezani na kuzibuliwa vizibo kabisa ili kila mtu anywe atakacho, bia iwe soda nk nk achague mwenyewe.
'Gage' ya ustarabu hupanda sana kadri mtu anapopewa uhuru wa kujisevia na si kugawiwa.
Kumekuwa na uchoyo kwa waandaaji na wahudumu.
Mtu kachangishwa 'malaki', akija kwenye msosi mgawaji anagawa kwa kusuasua hakandamizi kamusi sawasawa likasheheni zaga, mtu anaondoka kwenye vyakula kwenda kukaa kula hajaridhika.
Tukija kwenye vinywaji napo, mtu anakaukiwa chupa na akinyoosha mkono ahudumiwe, wahudumu wanajifanya hawaoni na muda unakwenda ili vinywaji vibakie!
Uchoyo uchoyo tu huku watu wamechangishwa matrilioni haufai.
Kama kuna mpangilio mzuri na management iliyokwenda shule, hatuwezi kuja na topic kama hizi sijui za kuona aibu mtu kula, huo ni udwanzi tu unaofanywa na waandaaji ili harusi inapomalizika wabakie na 'faida'!