Hekima, busara na nidhamu ya chakula (Table Manners) mbele ya kadamnasi ya wageni

Hekima, busara na nidhamu ya chakula (Table Manners) mbele ya kadamnasi ya wageni

Wenyewe wanasema hicho chakula kikibaki kitapelekwa wapi so acha watu wale.
Kama unakula kwa kuongeza basi watembee meza kwa meza kugawa chakula kwa anayetaka au wakuletee pale ulipo kama wafanyavyo kwa vinywaji na sio mtu mmoja unanyanyuka na sahani yako kwenda kuongeza nyama ya kuku wakati watu wengine wote 200 wametulia tuli.

Aibu sana hii. Tena ni uroho wa hali ya juu.
 
Kwanini hauwezi msibani mkuu???
Msiba n janga mtu unakuwa hujajipanga Yaani haina hodi.. so hata bajeti inakuwa finyu. hiv yaani ile ya kushtukiza...so mfiwa hajui atakuwa na wagen wangapi N. K, akifikilia ukute ndo vile pengine ana Debe 10 tu za chakula.. Sasa wewe ukila mara 2 wengine si watakosa
 
Mkuu, unaweza ukanyanyuka na lisahani lako kwenda kupakuliwa nyama ya kuku wakati watu wengine wote wamekaa?
Bila hofu yoyote mkuu. Tena na vile ndo DJ napanga playlist ya kutosha nazama zangu kwenye minofu...huku nimeweka wimbo ule wa alikiba usinisemeeeee
 
Nilifikiri wageni wanajiamsha wenyewe na kwenda kuchukua chakula ilhali kuna ambazo bado hawajapewa nafasi ya kwenda kuchukua chakula. Hiyo ingekuwa mbaya.
Ile kama wote wamepata fursa ya kupata mlo, na imetangazwa anayetaka kuongeza aende, sioni taabu hapo.
 
Mimi nilikula hapo hapo ukumbini muda ambao kila mmoja alikuwa anakula. Sasa kwa akili ya kawaida tu wewe unafikiri kwanini watu wengine wote wapotezee kwenda kuongeza chakula ila wao tu ndio waende?

Wao ndio wana njaa sana ya kufa?
Hapana
Wao wanaishi maisha yao wakati wewe na wenzako mnaishi maisha ya kuwa monitored na watu ..

Ishi maisha yako
 
Kama unakula kwa kuongeza basi watembee meza kwa meza kugawa chakula kwa anayetaka au wakuletee pale ulipo kama wafanyavyo kwa vinywaji na sio mtu mmoja unanyanyuka na sahani yako kwenda kuongeza nyama ya kuku wakati watu wengine wote 200 wametulia tuli.

Aibu sana hii. Tena ni uroho wa hali ya juu.


Unafki huo haujashiba kwanini uvunge kisa watu watakuonaje kila mtu ana kiwango chake cha kushiba hata hivyo.
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Sio kila muda tunapaswa kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya cold war, jeshi na ujasusi wa KGB, CIA na Mossad. Ngoja leo tujadili kidogo changamoto za maisha katika jamii tunamoishi.

Ndugu zangu wa Tanzania;

Miezi kadhaa iliyopita nilipata kuhudhuria sherehe moja ya harusi ya mtoto wa kike wa ndugu yangu wa karibu sana iliyofanyika katika ukumbi fulani maarufu sana kule mkoani Arusha. Kusema ukweli wa Mungu harusi ile ilifana sana. Ndugu, jamaa na marafiki sote tulijumuika tukala na kufurahi kwa pamoja.

Tulipiga story mbalimbali pamoja na kukumbushana mambo ya zamani kwa maana ilikuwa ni fursa pia ya kuonana na watu ambao hatukuweza kuonana kwa muda mrefu sana. Sasa kama inavyofahamika na wengi kwamba sherehe huwa ni ratiba mahususi na ratiba ile huwa ina vipengele vingi ndani yake ikiwa ni pamoja na kuwapokea maharusi, kutambulishana, kwenda kuchukua chakula pamoja na utoaji wa zawadi.

Hapa kwenye uchukuaji wa chakula ndio mada kuu ya mjadala kwa siku ya leo. Muda wa chakula ulipowadia ndugu mshereheshaji (MC) aliwaita maharusi kwanza, kisha wakafuata wazazi wa pande zote mbili na kumalizia na sisi akina Infantry Soldier (Kwa maana mimi kudandia sherehe ni kama ulimi na mate hahahaaaaaa I am joking....!!!!!!)

Bwana harusi alikuwa ni mtoto wa kiongozi fulani huko na yeye binafsi alikuwa anafanya kazi katika NGO moja kubwa tu huku Dar, hivyo ile sherehe ilikuwa ni ya budget kubwa kiasi. Hakika chakula kile kilikuwa ni kitamu sana sana tena saaaaana.

Kila mtu alikula na kufurahi lakini cha ajabu MC yule yule akatangaza kwa mara kadhaa kwamba ndugu wageni waalikwa mabibi na mabwana, CHAKULA BADO KIMEBAKI KINGI TU KWA ANAYETAKA KUONGEZA RUKSAAA hahahaaaaaa hapa ndio kasheshe ilipokuwapo. Amini usiamini, hakuna aliyethubutu hata kusimama kwenda kuongeza msosi isipokuwa jamaa fulani 3 ambao ni rafiki wa bwana harusi.

Kile kitendo walikifanya wao lakini aibu niliiona mimi. Inakuwaje mtu mzima na ndevu zake anashindwa kuizuia tamaa ya muda mfupi na kuamua kujidhalilisha namna ile mbele ya kadamnsi?

Sasa ndio nikajawa na maswaki mengi kuliko majibu kwamba;

Je, unafikiri ni jambo sahihi na busara mtu kuongeza chakula katika sherehe/msiba?

USISAHAU
: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

BIASHARA: Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher

MAONI YA MDAU
=======
Nikushauri kitu ndugu yangu katika hili kwa sababu nakuheshimu sana ila naomba leoo unisamehe nijaribu kukushauri kidogo: unapokuwa mahali popote pale hata kama ni nyumbani kwako, kwenye maswala haya ya chakula, jaribu kuji-tune ikiwezekana hata usiweze kabisa kujua nani alikula na nani hakula (kwa wale wasiokula kwa kupenda, ila si kwa kukosa chakula). Tuseme labda kama ni nyumbani kwako, unatakiwa ujue tu kwamba watu wamekula, na wakatosheka, details zingine tuachie sisi watu tuliokulia uswahilini, wewe kabisa huwa naona kama hauko kwenye rank yetu hiyo sisi watu wa uswahilini.
Kwa namna ulivyoielezea sherehe, inaonyesha ilikuwa ni classic ya aina fulani hivi kiasi kwamba haionyeshi kama kungeweza kuwa na rank ya watu wanaojali details za chakula, kama ulivyofanya wewe hapa. Kitu big kwenye sherehe hizi ni mtu kukosa chakula, vinginevyo kama chakula kinatosha na kiko safi, basi vitu vingine vyote kuhusu chakula hicho vinakuwa ni marginals!
Wewe rank yako huwa naiona kama haifanani fananni na maswala madogo madogo kama haya. Frankly seaking from my heart, hiki ulichopost hapa safari hii hakiendani kabisa na posts zako zote ambazo umeshawahi kuweka hapa Jamiiforums, maana posts zako nyingi huwa ziko kwenye Jamii intelligence!
 
Frankly seaking from my heart, hiki ulichopost hapa safari hii hakiendani kabisa na posts zako zote ambazo umeshawahi kuweka hapa Jamiiforums, maana posts zako nyingi huwa ziko kwenye Jamii intelligence!
Kaka mkubwa Makanyaga sio kila muda tunapaswa kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya cold war, jeshi na ujasusi wa KGB, CIA na Mossad.

Siku moja moja ni muhimu kama tujadili kidogo changamoto za maisha katika jamii tunamoishi.

Au kuna ubaya wowote mkuu???...
 
Tuseme labda kama ni nyumbani kwako, unatakiwa ujue tu kwamba watu wamekula, na wakatosheka, details zingine tuachie sisi watu tuliokulia uswahilini, wewe kabisa huwa naona kama hauko kwenye rank yetu hiyo sisi watu wa uswahilini.
Mkuu, mimi ni mtoto wa uswahilini sana. Nilizaliwa Kurasini, nikakulia Keko Akida kama unapafahamu. Mkuu, I am not that special and unique being. Mimi ni kijana wa kawaida sana tu kama wewe na Mshana Jr
 
Kitu big kwenye sherehe hizi ni mtu kukosa chakula, vinginevyo kama chakula kinatosha na kiko safi, basi vitu vingine vyote kuhusu chakula hicho vinakuwa ni marginals!
Mkuu, ninafikiri hapa tunatofautiana katika suala zima la malezi. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kukulia uswahilini na kupata malezi bora.

Mimi nimekuzwa nikijua fika ya kwamba, mtu anapaswa kuwa na discipline ya chakula mbele za watu hususan wageni...
 
hiki ulichopost hapa safari hii hakiendani kabisa na posts zako zote ambazo umeshawahi kuweka hapa Jamiiforums, maana posts zako nyingi huwa ziko kwenye Jamii intelligence!
Kaka yangu Makanyaga kila siku tukikaa kujadili masuala ya wazungu (KGB, CIA, MOSSAD) ni nani atazungumzia changamoto (ustaarabu) ndani ya jamii zetu tunamoishi?
 
kwenye kula hakuna aibu, huo ni ubishoo unakuwa kama wadada wanaagiza donati mbili halafu anakula moja anaacha moja naichukua hiyo donati nasogeza kwangu
 
kwenye kula hakuna aiu, huo ni ubishoo unakuwa kama wadada wanaagiza donati mbili halafu anakula moja anaacha moja
Mkuu, kwa hiyo watu 200 wote wametulia katika viti vyao halafu wewe mmoja ndio unanyanyuka na lisahani lako kwenda kuongeza ubwabwa? Kwani usipoongeza utakufa?

NIDHAMU YA KULA KWA STAHA MBELE YA WATU (KADAMNASI) ni lazima tufundishane.
 
Tuseme labda kama ni nyumbani kwako, unatakiwa ujue tu kwamba watu wamekula, na wakatosheka, details zingine tuachie sisi watu tuliokulia uswahilini,
Mkuu, ninaongelea ukumbini ambapo kuna watu usiowajua si chini ya 200, ni lazima mtu ajifunze nidhamu ya kula mbele ya kadamnasi, tena wengi ni strangers.

Nyumbani kama watu ni wengi sana basi mpo 10 mpaka 15, tena wote mmezoeana.

Mkuu, wewe haujawahi kuona mtoto anashabikia pilau msibani kisha aibu yote inaenda kwa wazazi wake na kuonekana kwamba kuwa huyu mtoto huwa ali akashiba huko kwao.

Sasa watoto (watu) kama hawa ndio wanapaswa kufundishwa discipline ya kula mbele za watu.
 
Back
Top Bottom