Mkuu, ninaongelea ukumbini ambapo kuna watu usiowajua si chini ya 200, ni lazima mtu ajifunze nidhamu ya kula mbele ya kadamnasi, tena wengi ni strangers.
Nyumbani kama watu ni wengi sana basi mpo 10 mpaka 15, tena wote mmezoeana.
Mkuu, wewe haujawahi kuona mtoto anashabikia pilau msibani kisha aibu yote inaenda kwa wazazi wake na kuonekana kwamba kuwa huyu mtoto huwa ali akashiba huko kwao.
Sasa watoto (watu) kama hawa ndio wanapaswa kufundishwa discipline ya kula mbele za watu.
Una uhakika gani kwamba hao watu watatu hawakuwa wamechelewa kula, yaani walifika ukumbini baada ya watu kuwa wameshaanza kula na kukuta foleni ya chakula ikiwa imekatika, wakajua kuwa chakula tayari kimeshaisha, ila Mc alipochukua jukumu la kuwatangazia watu kwamba chakula bado kipo, ndiyo wakajua kuwa chakula kumbe bado kipo na hivyo nao wakaamua sasa kwenda kuchukua kwa mara ya kwanza ili waweze kula, vinginevyo wasingekula kwa sababu hapo awali hawakuwa wamekula?
Kuna shemeji yangu mmoja, alishatangulia mbele ya haki, aliwahi kuniusia maneno fulani kipindi kirefu nyuma. Aliniambia kuwa: Shemeji, maisha haya tunayoishi ni magumu sana, na inabidi ujinyime sana kwenye kipata chako ili uweze kupata savings zitakazokuwezesha kufanya mambo mengine ya msingi katika maisha LAKINI, usijinyime kiasi cha kushindwa kula ukashiba. Hakikisha unakula na kushiba kwanza halafu ndiyo maswala ya kujinyima yaanzie pale, baada ya kuwa umekula na kushiba.
Huyu mtu alikuwa hamaanishi nile mimi na kushiba, bali watu walio pamoja na mimi wakati wowote ule. Mimi nina principal moja katika maisha, linapokuja swala la kula, bajeti yake huwa inategemea kiwango cha ulaji cha wale ninaotakiwa kuwalisha, na si kutokana na idadi za kilo za mchele au unga ambazo huwa nimeweka kama budget yangu ya matazamio (tentative budget) kwenye mwezi au wiki husika, maana kwa upande mwingine ni lazima mtu uwe na budget, huwezi ukawa unapuyanga tu. Kwa hiyo huwa nanunua chakula wakati mwingine kulingana na rate ya ulaji wao, na namna namba yao inavyobadilika, na si vinginevyo.
Unajua ndugu yangu Mungu ametutunuku mwanadamu akili ambayo ni kubwa muno kiasi kwamba hatutakiwi kabisa kuitumia kuwaza mambo madogo madogo kama haya, isipokuwa inatokea wakati mwingine inabidi tuyawaze kwa sababu si muda wote tunatumia akili zeu kama ambavyo Mungu anataka tuzitumie. Mungu alipomuumba mwanadamu, mojawapo ya majukumu aliyompa, kubwa kabisa ilikuwa ni kuitawala dunia , swala la kula lilikuja tu by the way. Mungu angeweza hata kumuumba mwanadamu bila hitaji la kula kwa sababu halikuwa kusudi lake kumuumba ili awe anakula pia. Kula kulikuja tu by the way!
Kwa swala la watoto wadogo, hilo sasa ni jambo jingine tena kwa sababu hao bado ni wanafunzi wa kila jambo!