MADA YA LEO: NI MUHIMU SANA MTU KUWA NA NIDHAMU YA KULA KWA STAHA MBELE YA WATU (KADAMNASI)
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.
Sio kila muda tunapaswa kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya
cold war, jeshi na ujasusi wa KGB, CIA na Mossad. Ngoja leo tujadili kidogo changamoto za maisha katika jamii tunamoishi. Kila siku tukikaa kujadili masuala ya wazungu ni nani atazungumzia ustaarabu wetu?
Ndugu zangu wa Tanzania;
Miezi kadhaa iliyopita nilipata kuhudhuria sherehe moja ya harusi ya mtoto wa kike wa ndugu yangu wa karibu sana iliyofanyika katika ukumbi fulani maarufu sana kule mkoani Arusha. Kusema ukweli wa Mungu harusi ile ilifana sana. Ndugu, jamaa na marafiki sote tulijumuika tukala na kufurahi kwa pamoja.
Tulipiga story mbalimbali pamoja na kukumbushana mambo ya zamani kwa maana ilikuwa ni fursa pia ya kuonana na watu ambao hatukuweza kuonana kwa muda mrefu sana. Sasa kama inavyofahamika na wengi kwamba sherehe huwa ni ratiba mahususi na ratiba ile huwa ina vipengele vingi ndani yake ikiwa ni pamoja na kuwapokea maharusi, kutambulishana, kwenda kuchukua chakula pamoja na utoaji wa zawadi.
Hapa kwenye uchukuaji wa chakula ndio mada kuu ya mjadala kwa siku ya leo. Muda wa chakula ulipowadia ndugu mshereheshaji (MC) aliwaita maharusi kwanza, kisha wakafuata wazazi wa pande zote mbili na kumalizia na sisi akina Infantry Soldier (Kwa maana mimi kudandia sherehe ni kama ulimi na mate hahahaaaaaa I am joking....!!!!!!)
Bwana harusi alikuwa ni mtoto wa kiongozi fulani huko na yeye binafsi alikuwa anafanya kazi katika NGO moja kubwa tu huku Dar, hivyo ile sherehe ilikuwa ni ya budget kubwa kiasi. Hakika chakula kile kilikuwa ni kitamu sana sana tena saaaaana.
Kila mtu alikula na kufurahi lakini cha ajabu MC yule yule akatangaza kwa mara kadhaa kwamba ndugu wageni waalikwa mabibi na mabwana,
CHAKULA BADO KIMEBAKI KINGI TU KWA ANAYETAKA KUONGEZA RUKSAAA hahahaaaaaa hapa ndio kasheshe ilipokuwapo. Amini usiamini, hakuna aliyethubutu hata kusimama kwenda kuongeza msosi isipokuwa jamaa fulani 3 ambao ni rafiki wa bwana harusi.
Kile kitendo walikifanya wao lakini aibu niliiona mimi. Inakuwaje mtu mzima na ndevu zake anashindwa kuizuia tamaa ya muda mfupi na kuamua kujidhalilisha namna ile mbele ya kadamnsi?
Sasa ndio nikajawa na maswaki mengi kuliko majibu kwamba;
Je, unafikiri ni jambo sahihi na busara mtu kukosa Busara na nidhamu ya chakula (Table Manners) mbele ya kadamnasi ya wageni?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
BIASHARA:
Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher
MAONI YA MDAU
=======