Israel si kitu pasipo msaada wa US na nchi za EU.
Egypt tu inaitandika Israel inapotea wakienda man to man, hakuna kuingilia, japo ni kitu kisichowezekana katika uhalisia.
Hata six days war Israel ilipewa msaada mkubwa na nchi za magharibi kuanzia intel hadi silaha.
Hujajibu nilichokuuliza!
Ni kweli, Israel bila msaada wa US atapata wakati mgumu sana kwenye vita.
Ila wewe umezungumzia vita vya ardhini.
Ni hivi, vita vya ardhini ni vya kizamani, ni vyenye hatari nyingi, na havina mwenyewe.
Jeshi moja linaweza kuwa na vifaru, bunduki za kisasa, na kadhalika lakini ikija kwenye mpambano, linaweza kupoteza askari wengi pia.
Hiyo ni kwa sababu dynamics za ardhini ni tofauti kabisa na za angani.
Ardhini ni mwendo ya kuviziana na kunyatiana tu. Wewe hata uwe na AK 47, mwenye gobole anaweza akakujambisha, hususan kama umeingia kupigana alipo yeye.
Risasi ni risasi tu. Unakuja kwangu na AK 47 yako halafu mimi nakusubiri kwenye sehemu yangu ya kujificha na gobole langu.
Ukiingia tu kwenye 18, nakudungua na gobole langu. Wewe na AK 47 yako chali.
Vita vya ardhini havihitaji akili kubwa. Vya angani na vya majini ndo vinahitaji akili kubwa.
Ndo maana unaona vita nyingi za siku hizi zinapiganiwa angani zaidi.
Ardhini hakuna mwenye advantage kubwa na ndo maana unadhani Israel ni mchovu wakati si kweli.
Risk yake ipo palepale kwa pande zote.