TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

Jana pia niliiona helicopter anayosafiria Kinana, Mh!!! Inabidi ufumbe macho wakati unapanda maana ni chakavu mno.!
 
Dah Deo usiondoke bado tunakuhitajiiii ...mola awalinde
 
tusubiri tutaendelea kupata taarifa na kujua nini kinaendelea.

Mwenye baba mtu kasema hivyo taarifa za Radio one zinasema vingine.
Slaa.png
 
Nadhani baada ya Mwandosya kususa na Mwakyembe kushindwa kuwa na ushawishi Nyanda za Juu kusini, walitaka kumtumia huyu bwana ili wapate kura huko maana ukimtoa Prof Mwandosya sidhani kama kuna mwingine mwenye ushawishi pande za kule. Nadhani ndiyo akapewa mpaka hiyo Helikopta atembee pande zote huko kumnadi Magufuli.. Sijui kwanini na yeye aliingia kwenye mkenge wa wahuni safari hii..


Acheni uchochezi na kupotosha ukweli. Mwandosya hakusema amesusa bali alichosema ni kuwa anahamia kijijini kwao LUFILYO kwasababu amestaafu siasa. Kustaafu na kususa ni vitu mbali mbali ; muwe waangalifu na hayo mnayoandika!!
 
Kwe page ya wananchi blog wanadai wamepona

Tutende kwa haki,na Mungu atatutendea mema.Tuhukumu kwa haki nasi tutaepuka ghadhabu zake Mungu.Tuwatakie wengine mema nasi tutakingwa dhidi ya mabaya.Tusijitwalie nafasi ya Mungu kuhusu uzima na umauti wa wengine nasi hatutahukumiwa.
 
jerry silaa amethibitisha kwenye account yake ya tweeter kuwa alikuwemo kwenye ile helcopter ni baba yake cpt silaa...ila toka helcopter hio imeanguka hawana mawasiliano na watu walioko humo ...usiku kucha juhudi zilikua zinafanyika kuwatafuta lkn imeshindikana........chopa ilikua inatoka dar kwenda ludewa
 
Ndio utakapoona kuwa maisha yetu ni kudra za mwenyezi Mungu tu. Hata hao ambao wana uwezo kiasi cha kumiliki au kukodi chopa, hawawezi kuhakikishiwa 'immediate rescue' kama tatizo litatokea. Uhai inabidi ulindwe kwa gharama yoyote ile, watu wa uokoaji inabidi wawe na vifaa vya kwenda 'terrains' zote iwe usiku au mchana. Sasa mambo ya kusubiria mpaka asubuhi haya...
 
Sasa hao wanaosema wamepona wamejuaje wakati MTOTO wa pilot,Jerry Silaa anasema hawana mawasiliano nao na wameanguka msituni!?
Tunawaombea wawe salama!
 
Sasa Mbugani huko si kuna King wa Pori na Nyau wa Pori(Chui) Mungu uwaepushe ingawa wanatukana sana
 
Hivi nawezaje kuwasiliana na Izrail Mtoa Roho?? Kuna kitunataka nimuombe
 
Back
Top Bottom