Henry Kilewo: CHADEMA ya sasa sio ile iliyopita, hii achaneni nayo

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Kada wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye kwa sasa ni Kada wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Henry Kilewo, amewataka wanaojiita watawala kuachana na madalali wa kisiasa wanaowadanganya kuwa wanaweza kukigawa chama hicho.

Kupitia chapisho aliloliweka katika mtandao wake wa X (zamani Twitter) juzi Agosti 31, 2026, Kilewo amebainisha kuwa mfumo na uongozi wa sasa wa CHADEMA ni tofauti na ule wa zamani, kwani umerithi uzoefu wa nyuma na kujifunza kutokana na makosa yaliyopita ili kuepuka gharama kubwa za kisiasa

“Version ya CHADEMA ya leo sio ile iliyopita, hii imekulia kwenye ile version na ikaona makosa yake na haiwezi kuishi yale makosa kwakuwa inajua makosa yale yatawagharimu kuliko gharama wanazolipa leo,” ameeleza Kilewo.

Amesisitiza kuwa CHADEMA ni taasisi imara mno ambayo haiwezi kugawanywa hata kwa kutumia medali za juu za kivita, huku akiongeza kuwa njia iliyochaguliwa na chama hicho ndiyo sahihi katika kuondoa utawala kandamizi.

Kilewo amehitimisha kwa kutoa rai ya kimaadili akisema ni heri kuishi miaka michache duniani kwa wema na haki kuliko kuishi miaka mingi kwa uongo na unafiki ambao mwisho wake ni mbaya zaidi.
 
Attachments

  • 1000170151.png
    1000170151.png
    1.7 MB · Views: 14
Anachonifurahisha Henry Kilewo ni kuwa yuko huko ubwabwani (CHAUMMA) lakini nafsi na roho yake zimeshikamanishwa na CHADEMA..

Hawa kina Henry Kilewo, Benson Kigaila, Yericko Nyerere, Lembros Mchome, John Mrema, na wengine waliotimkia ubwabwani ni kama wanawake walioolewa kwa ndoa za mkeka (kwa kulazimishwa) lakini mioyo yao Iko mbali na waume zao, muda wote wanafikiria wanaume waliozitoa bikra zao - CHADEMA..

Kirini makosa yenu (UKWELI), ikumbatieni HAKI, Kisha chukueni wajibu wenu (UWAJIBIKAJI)...

Mkimaliza hayo, zaliweni upya, Rudini nyumbani, maana huku ndiko kumenoga kwa sasa...!
 
Kilewo amehitimisha kwa kutoa rai ya kimaadili akisema ni heri kuishi miaka michache duniani kwa wema na haki kuliko kuishi miaka mingi kwa uongo na unafiki ambao mwisho wake ni mbaya zaidi.
🙏💎🇹🇿
 
Back
Top Bottom