Heri ya kuzaliwa Jakaya Mrisho Kikwete, nguli wa diplomasia na mwanajeshi uliyeiva

Heri ya kuzaliwa Jakaya Mrisho Kikwete, nguli wa diplomasia na mwanajeshi uliyeiva

Ndugu zangu Watanzania,

Ninayo furaha kubwa sana Moyoni Mwangu kumtakia heri ya kuzaliwa mzee wetu Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu wa awamu ya Nne,Mwanajeshi mstaafu,mwanadiplomasia Nguli,Kipenzi cha waafrika na DUNIA nzima kwa ujumla wake aliyezaliwa siku kama ya leo yaani Tarehe 7 -10-1950.

Nitaendelea kumkumbuka kwa Mengi sana huyu mzee wakati wa utawala na uongozi wake. Ni yeye aliyenishawishi kujiunga CCM mwaka 2005 alipokuja kwenye kampeni za Urais mkoani Rukwa ,wilaya ya Sumbawanga vijijini mji mdogo wa Laela Jimbo la Kwela lililoongozwa kwa muda mrefu na Marehemu mzee Chrisant Maji ya Tanga Mzindakaya. Ni yeye na serikali yake aliyenipatia mkopo wa Elimu ya juu ambapo kama siyo kupata mkopo basi nisingeweza kupata Elimu hiyo ndani ya chuo kikuu cha Dar es salaam.

Watanzania na hususani vijana wataendelea kumkumbuka mzee huyu asiye na makuu wala majivuno.ni kiongozi ambaye alifikika na makundi yote ,akimfariji kila mtu,alimpatia matumaini kila mtu,aligusa maisha ya wengi sana ,alitoa misaada kwa wengi sana.na kwa hakika watu waliguswa vyema sana.Alikuwa mtu wa Msaada na hakuona uvivu kuinuka na kutoka ofisini kwenda kumpa faraja mtu au mtanzania mmoja tu mwenye shida na tatizo iwe ni hospitalini au nyumbani.

Alitoa ajira kwa vijana mpaka watu wakawa wanachagua mahali pa kufanyia kazi kati ya mijini na vijijini. Ukimaliza tu chuo hasa ualimu na udaktari ilikuwa ni lazima upate ajira tu .ilikuwa ni raha sana kiukweli kwa waliomaliza vyuo wakati wake maana walipata bahati sana na kubwa.

Alitukanwa sana ,alidhalilishwa sana lakini alibakia mtulivu mwenye tabasamu ya uso na moyo na kumsamehe kila mtu na kuwafanya watu waliomtukana kujutia baadaye alipoondoka madarakani. Alijuwa kuwalea viongozi na kuibua vipaji vya uongozi .hakuwa na chuki na mtu wala baya na mtu.alikuwa mvumilivu sana huyu Mzee na aliwapenda sana Watanzania.hakuwa na visasi wala chuki na mtu.ni Mwenyewe alisema za kuambiwa changanya na zako maana hakupenda kurithishwa adui au maadui au kumezeshwa chuki au uongo au uchonganishi na mtu fulani.

Alileta tabasamu kwa kila mtu.yeyote aliweza kuwa kiongozi wakati wake bila kujali hali yake au ukoo alipotokea mtu.alichoangalia ni uwezo wa mtu kiuongozi.mikono yake imewabeba watu wengi sana kiuongozi, Mabega yake na mgongo wake umewabeba wengi sana kuwainua na kuwasogeza mbele. Hata sasa ukiangalia viongozi wakubwa na hata katika Baraza la Mawaziri utaona wamepita mikononi mwake .

Mungu aendelee kumjalia maisha marefu yenye heri ,amani ,furaha na baraka tele.aishi maisha marefu zaidi ya karne moja hapa Duniani.View attachment 3117304

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Nakubaliana Jakaya ndio alikuwa mwana demokrasia na mwana diplomasia wa kweli na wakati wake upinzani ulifanya vizuri sana lakini sio Magufuli na Samia.
 
Kufa tu kama una hasira na chuki binafsi kwa Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka , chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.

Mama ndio chaguo la watanzania kuongoza muhula wa pili.na anatosha kufanya kazi hiyo.ameonyesha uwezo na utayari wa kulibeba Taifa letu.ametuvusha nyakati ngumu mpaka hapa tulipo.
 
Kikwete ndiyo Rais pekee wa Tanzania ambae ni Mwanajeshi wa kweli.

Hiyo rikodi njema ys kuwa Mwanajeshi kabla ya kuwa Rais bado ni yake pekee baada ya Marais sita wa Tanzania, watano wao kutokuwa wanajeshi mpaka walipokuwa MaamiriJeshikwa Urais wao.
 
Uwe na adabu kwa Mheshimiwa Rais. Ni daktari Samia Suluhu Hasssan aliyetoa na kuruhusu vyama vya siasa kufanya siasa za majukwaani,kutoa uhuru kwa vyombo vya habari,kuruhusu watu kuzungumza kwa uhuru bila shida,kuondoa mahakamani kesi zote zenye sura ya kisiasa,kufanya mazungumzo na vyama vya siasa na kusikiliza mawazo yao ,kuwarejesha Nchini waliokuwa wamekimbia kwa sababu za kisiasa kuhofia usalama wao.
Hivyo alivyo ruhusu vilikuwa vimekatazwa kufanyika kwa mujibu wa katiba??
 
Kikwete ndiyo Rais pekee wa Tanzania ambae ni Mwanajeshi wa kweli.

Hiyo rikodi njema ys kuwa Mwanajeshi kabla ya kuwa Rais bado ni yake pekee baada ya Marais sita wa Tanzania, watano wao kutokuwa wanajeshi mpaka walipokuwa MaamiriJeshikwa Urais wao.
Ndio maana alikuwa Mvumilivu sana huyu Mzee.Mungu aendelee kumbariki sana.Ndio maana unaona pamoja na kustaafu kwake lakini bado Dunia inaendelea kumtumia katika majukumu mbalimbali
 
Maigizo matupu na upumbavu mtupu.

Watu walitia hasara bilion 11.5

Adhabu ni faini milion 5 na kifungo miaka 3

Na bado wakabadilishiwa kifungo kutoka jela miaka 3 hadi kufagia hospitali.

Msifikiri tumesahau na sio kila mtu anatokea Kolomije.
Kiongozi pekee aliyewafunga Jela Waziri wa Fedha na Waziri wa Madini kwa Ufisadi

Happy birthday JK 🌹
 
Back
Top Bottom