Heri ya kuzaliwa Jakaya Mrisho Kikwete, nguli wa diplomasia na mwanajeshi uliyeiva

Ndugu zangu Watanzania,

Ninayo furaha kubwa sana Moyoni Mwangu kumtakia heri ya kuzaliwa mzee wetu Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu wa awamu ya Nne,Mwanajeshi mstaafu,mwanadiplomasia Nguli,Mwana Demokrasia aliyekomaa,Kipenzi cha watanzania na waafrika na DUNIA nzima kwa ujumla wake aliyezaliwa siku kama ya leo yaani Tarehe 7 -10-1950.

Nitaendelea kumkumbuka kwa Mengi sana huyu mzee wakati wa utawala na uongozi wake. Ni yeye aliyenishawishi kujiunga CCM mwaka 2005 alipokuja kwenye kampeni za Urais mkoani Rukwa ,wilaya ya Sumbawanga vijijini ,mji mdogo wa Laela, Jimbo la Kwela lililoongozwa kwa muda mrefu na Marehemu mzee Chrisant Maji ya Tanga Mzindakaya. Ni yeye na serikali yake aliyenipatia mkopo wa Elimu ya juu ambapo kama siyo kupata mkopo huo basi nisingeweza kupata Elimu hiyo ndani ya chuo kikuu cha Dar es salaam.

Watanzania na hususani vijana wataendelea kumkumbuka mzee huyu asiye na makuu wala majivuno.ni kiongozi ambaye alifikika na makundi yote ,alimfariji kila mtu,alimpatia matumaini kila mtu,aligusa maisha ya wengi sana ,alitoa misaada kwa wengi sana.na kwa hakika watu waliguswa vyema sana.Alikuwa mtu wa watu,mtu wa Msaada na hakuona uvivu kuinuka na kutoka ofisini kwenda kumpa faraja mtu au mtanzania mmoja tu mwenye shida na tatizo iwe ni hospitalini au nyumbani.

Alitoa ajira kwa vijana mpaka watu wakawa wanachagua mahali pa kufanyia kazi kati ya mijini na vijijini. Ukimaliza tu chuo hasa ualimu na udaktari ilikuwa ni lazima upate ajira tu .ilikuwa ni raha sana kiukweli kwa waliobahatika au waliomaliza vyuo wakati wake maana walipata bahati sana tena kubwa ya ajira..

Alitukanwa sana huyu Mzee ,alidhalilishwa sana lakini alibakia mtulivu mwenye tabasamu ya uso na moyo na kumsamehe kila mtu ,na kuwafanya watu waliomtukana kujutia baadaye alipoondoka madarakani. Alijuwa kuwalea na kuwakuza viongozi na kuibua vipaji vya uongozi .hakuwa na chuki na mtu wala baya na mtu.alikuwa mvumilivu sana huyu Mzee na aliwapenda sana Watanzania.hakuwa na visasi wala chuki na mtu.ni Mwenyewe alisema za kuambiwa changanya na zako maana hakupenda kurithishwa adui au maadui au kumezeshwa chuki au uongo au uchonganishi na mtu fulani.

Alileta tabasamu kwa kila mtu.yeyote aliweza kuwa kiongozi wakati wake bila kujali hali yake au ukoo alipotokea mtu.alichoangalia ni uwezo wa mtu kiuongozi.mikono yake imekuwa daraja na imewabeba watu wengi sana kiuongozi, Mabega yake na mgongo wake umewabeba wengi sana kuwainua na kuwasogeza mbele. Hata sasa ukiangalia viongozi wakubwa na ngazi ya juu kabisa serikalini na hata katika Baraza la Mawaziri utaona wamepita mikononi mwake .

Mungu aendelee kumjalia maisha marefu yenye heri ,amani ,furaha na baraka tele.aishi maisha marefu zaidi ya karne moja hapa Duniani.View attachment 3117304

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kumbukumbu nzuri sana Mwashambwa hata Boni yai kapata dhamana Leo tarehe 07_10_2024, Hongera Kikwete, hongera Mwashambwa kwa kuliona hili pia la Boni yai!
 
Sio
Uwe na adabu kwa Mheshimiwa Rais. Ni daktari Samia Suluhu Hasssan aliyetoa na kuruhusu vyama vya siasa kufanya siasa za majukwaani,kutoa uhuru kwa vyombo vya habari,kuruhusu watu kuzungumza kwa uhuru bila shida,kuondoa mahakamani kesi zote zenye sura ya kisiasa,kufanya mazungumzo na vyama vya siasa na kusikiliza mawazo yao ,kuwarejesha Nchini waliokuwa wamekimbia kwa sababu za kisiasa kuhofia usalama wao.
Sio mamaKatiba ndio inaruhusu kufanya mikutano na maandamano,katiba hiyo hiyo ndio iliompa madaraka, katiba hiyo hiyo unaweza kupata uteuzi wa kukimbiza mwenge wewe.
 
Heri ya siku ya kuzaliwa mzee JK Kikwete...bado ninakukubali na nitaendelea kukumbuka mazuri ulioyafanya enzi za utawala wako japo mengine ilikuwa ni sehemu ya changamoto katika uongozi mfano la TEGETA ESCOW....Pia hata mama yetu DKT Samia Suluhu Hassani tunaimani naye asilimia 100 naamini hili la PPP atakuwa nalo makini lisije likaleta changamoto kama lile la ESCROW.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ninayo furaha kubwa sana Moyoni Mwangu kumtakia heri ya kuzaliwa mzee wetu Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu wa awamu ya Nne,Mwanajeshi mstaafu,mwanadiplomasia Nguli,Mwana Demokrasia aliyekomaa,Kipenzi cha watanzania na waafrika na DUNIA nzima kwa ujumla wake aliyezaliwa siku kama ya leo yaani Tarehe 7 -10-1950.

Nitaendelea kumkumbuka kwa Mengi sana huyu mzee wakati wa utawala na uongozi wake. Ni yeye aliyenishawishi kujiunga CCM mwaka 2005 alipokuja kwenye kampeni za Urais mkoani Rukwa ,wilaya ya Sumbawanga vijijini ,mji mdogo wa Laela, Jimbo la Kwela lililoongozwa kwa muda mrefu na Marehemu mzee Chrisant Maji ya Tanga Mzindakaya. Ni yeye na serikali yake aliyenipatia mkopo wa Elimu ya juu ambapo kama siyo kupata mkopo huo basi nisingeweza kupata Elimu hiyo ndani ya chuo kikuu cha Dar es salaam.

Watanzania na hususani vijana wataendelea kumkumbuka mzee huyu asiye na makuu wala majivuno.ni kiongozi ambaye alifikika na makundi yote ,alimfariji kila mtu,alimpatia matumaini kila mtu,aligusa maisha ya wengi sana ,alitoa misaada kwa wengi sana.na kwa hakika watu waliguswa vyema sana.Alikuwa mtu wa watu,mtu wa Msaada na hakuona uvivu kuinuka na kutoka ofisini kwenda kumpa faraja mtu au mtanzania mmoja tu mwenye shida na tatizo iwe ni hospitalini au nyumbani.

Alitoa ajira kwa vijana mpaka watu wakawa wanachagua mahali pa kufanyia kazi kati ya mijini na vijijini. Ukimaliza tu chuo hasa ualimu na udaktari ilikuwa ni lazima upate ajira tu .ilikuwa ni raha sana kiukweli kwa waliobahatika au waliomaliza vyuo wakati wake maana walipata bahati sana tena kubwa ya ajira..

Alitukanwa sana huyu Mzee ,alidhalilishwa sana lakini alibakia mtulivu mwenye tabasamu ya uso na moyo na kumsamehe kila mtu ,na kuwafanya watu waliomtukana kujutia baadaye alipoondoka madarakani. Alijuwa kuwalea na kuwakuza viongozi na kuibua vipaji vya uongozi .hakuwa na chuki na mtu wala baya na mtu.alikuwa mvumilivu sana huyu Mzee na aliwapenda sana Watanzania.hakuwa na visasi wala chuki na mtu.ni Mwenyewe alisema za kuambiwa changanya na zako maana hakupenda kurithishwa adui au maadui au kumezeshwa chuki au uongo au uchonganishi na mtu fulani.

Alileta tabasamu kwa kila mtu.yeyote aliweza kuwa kiongozi wakati wake bila kujali hali yake au ukoo alipotokea mtu.alichoangalia ni uwezo wa mtu kiuongozi.mikono yake imekuwa daraja na imewabeba watu wengi sana kiuongozi, Mabega yake na mgongo wake umewabeba wengi sana kuwainua na kuwasogeza mbele. Hata sasa ukiangalia viongozi wakubwa na ngazi ya juu kabisa serikalini na hata katika Baraza la Mawaziri utaona wamepita mikononi mwake .

Mungu aendelee kumjalia maisha marefu yenye heri ,amani ,furaha na baraka tele.aishi maisha marefu zaidi ya karne moja hapa Duniani.View attachment 3117304

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Hakuna kitu hapo chenga tu.
 
Mfanano wa msoga na kizimkazi ni kama ifuatavyo
(1)Wote ni watekaji.mfano ulimboka kipindi Cha msoga na kipindi Cha kizimkazi wamepotea wengi kama ilivyotolewa na TLS
(2)Wote hawana huruma na rasilimali za taifa.msoga aliuza TRc Kwa wahindi na likajifia na akauza gesi yetu ya mtwara Kwa wachina ambapo sisi wachina ndiyo wanaiuzia tanesco ndiyo maana hatuoni nafuu yeyote ya umeme kushika bei.the same to kizimkazi expelled Masai from their ancenstors land for benefit of Arabs.
(3)Wote walitumia muda mwingi kusafiri kwenda nje ya Nchi kuliko kutatua kero zinazowakumba Wana chi wa Tanzania.2025 tuchukue hatua kuondoa Hawa mchwa wa Nchi.
 
Wewe hunaga akili siku zote.
 
Heri ya mfanano wa siku ya Kuzaliwa Mhe Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutimiza miaka 74 Rais mstaafu wa awamu ya 4 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanadiplomasia nguli,Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema akupe maisha marefu na sia njema.
Jakaya_Kikwete.jpg
 
Heri ya mfanano wa siku ya Kuzaliwa Mhe Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutimiza miaka 74 Rais mstaafu wa awamu ya 4 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanadiplomasia nguli,Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema akupe maisha marefu na sia njema.View attachment 3118118

Hakuwa na makuu wala baya na mtu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ninayo furaha kubwa sana Moyoni Mwangu kumtakia heri ya kuzaliwa mzee wetu Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu wa awamu ya Nne,Mwanajeshi mstaafu...
Jk ni kipenzi Cha wengi ni mtu mwungwana saana ,nakumbuka wakati alipokuwa amefika mwisho wa kipindi Cha utawala wake aliwahi kuulizwa na mwandishi mmoja wa habari kwamba Watanzania wakukumbuke kwa lipi?

jibu lake lilikuwa short and clear ,kwamba kwenye utawala wake demokrasia ilishamiri saana kwamba mtu anaweza kusimama kwenye jukwaa na kusema Rais gani huyu ,kwamba kwa nchi zingine hayo maneno ungetamka ukiwa ndani ya handaki.hahah Huyo ndiyo Jk
 
Back
Top Bottom