Leo ni maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa Mheshimiwa Rais wa Tanzania. Ni Siku ya Nuru na Matumaini mapya kwa watanzania kutokana na mabadiliko makubwa ya kiuongozi yenye tija na matokeo chanya kwa maisha ya watanzania.
Kwanini Happy Birthday ya JPM ni Happy birthday Kwa Tanzania nzima, ninao ushahidi ktk nyanja 12 ambazo JPM amezisimamia vyema na kuleta matokeo chanya. Nazo ni:
1. Katika Tiba, Afya, Umeme na Maji: Ameboresha huduma za afya nchini kwa ujenzi na ukarabati wa Hospitali, zahanati na vituo vya afya. Ameimarisha usambazaji na usimamizi wa dawa na vifaa tiba katika Hospitali za umma. Huduma za Bima ya afya zimeboreshwa 100%. Ujenzi wa Stigglers Gorge na miradi ya REA ni suluhisho LA umeme mijini na vijijini. Miradi ya maji nchi nzima ni uwajibikaji wa JPM kwa wananchi
2. Katika Elimu: Amewezesha Elimu bure kwa kidato cha kwanza hadi cha NNE kwa kupeleka ruzuku kwa wakati. Ameongeza mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu. Shule Kongwe kama Iyunga, Ruvu, Msalato, Jangwani, Nganza, Kibaha, Ilboru, N.k zimekarabatiwa kwa kiwango cha rami.Pamoja na vyuo vya ualimu kama Mpwapwa, Morogoro n.k. Ujenzi wa Hostel Udsm na miundo mbinu mingine.
3. Katika ulinzi, usalama, amani na utulivu: Raia na Mali zao wapo salama. Matukio ya uporaji na uvamizi wa mabenki yamedhibitiwa, mipaka ipo salama na hakuna chokochoko za majirani
4. Katika Miundo Mbinu: Wakandarasi wapo nchi nzima wanajenga ama kukarabati barabara, madaraja, vivuko, viwanja vya ndege, fly overseas na interchange.
5. Katika Usafiri na Usafirishaji: Ndege bora za kisasa, meli, vivuko na treni vipo imara kusafirisha abiria na mizigo
6. Katika Kilimo na Ushirika: Ubadhirifu wa vyama vya ushirika katika fedha na rasilimali zingine umewekewa mkazo na fedha, maghala na majengo vimeanza kurejeshwa kwa wakulima
7. Katika michezo: Usimamizi thabiti wa fedha na mapato michezoni umeziwezesha Timu za Taifa na Vilabu kufanya vyema. Mfano: Tumefuzu CHAN, AFCON na kuandaa mashindano makubwa ya vijana Afrika. Simba imecheza makundi club bingwa na kuliwezesha Taifa kuingiza Timu NNE ktk mashindano makubwa Afrika
8. Katika Madini na uwekezaji: Serikali yake imeweza kupitia upya sheria na mikataba ya uchimbaji hivyo kunufaisha Taifa kwa mkataba wa Barrick na kuwaondoa wababaishaji Acacia. Udhibiti wa utoroshaji madini umeongeza mapato ya madini
9. Katika Utalii na Mazingira: JPM ameweza kudhibiti utoroshaji wa wanyama hai, amedhibiti uwindaji haramu na uharibifu wa mazingira. Katazo LA mifuko ya plastiki na adhabu za NEMC ni ushuhuda
10. Katika Siasa na Utawala: JPM amedhihirisha kwamba cheo ni dhamana na wajibu wa viongozi sio kujinufaisha Bali kutumikia umma. Teua-tengua imeongoza uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi maana kiongozi anapovurunda hafumbiwi macho bila kujali cheo chake. Magereza imekuwa ni kwa waharifu wote, matajiri kwa maskini, viongozi kwa RAIA, CCM kwa wapinzani.
11. Katika Kodi na Mapato ya Taifa: Serikali ya JPM imesimamia vyema makusanyo ya TRA kwa kuziba mianya ya Rushwa na ufujaji. Pia udhibiti wa safari za nje na udhibiti wa makontena bandarini umeongeza mapato ya serikali
12. Katika Vita dhidi ya Madawa ya kulevya na Heshima ya Tanzania kimataifa: Serikali ya JPM imeweza kudhibiti vita dhidi ya madawa ya kulevya kupitia vyombo mbalimbali. Heshima ya Nchi kama Taifa lenye Amani, Utulivu, Heshima na Uzalendo ni dhahiri Kimataifa na mataifa mengi wanatamani JPM awe kiongozi wa nchi yao. Fursa tele vimefunguliwa kwa watanzania kusoma na kufanya biashara ktk nchi mbalimbali
Kwa Hayo Machache niliyoelezea, Watanzania wote tunayosababu ya Kufurahia, kusherehekea siku ya kuzaliwa JPM na Kumtakia Heri, Afya njema na Uzima ili kuliendeleza Taifa letu. Happy Birthday My Coach JPM, May the Lord Protect You Forever.