GE2025 Hersi atemwa tena ubunge Kongwa, 13 wapita

GE2025 Hersi atemwa tena ubunge Kongwa, 13 wapita

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Rais wa Klabu ya Yanga, Hersi Said ameshindwa kupenya katika mchujo wa majina 13 ya wagombea ubunge Jimbo la Kongwa.

Hersi ameungana na wagombea wengine 11 ambao majina yao yameshindwa kupenya katika mchakato huo, huku aliyeshika nafasi ya pili kwenye kura za maoni Agosti 4, 2025, Isaya Mngurumi akipenya.

Soma pia: Ndugai huna chako Jimbo la Kongwa, Hersi Said wa Yanga ni Mbunge ajae Kongwa

View attachment 3442191
Mapema leo, Katibu wa CCM Wilaya ya Kongwa, Joyce Mkaugala amesema jina la Hersi lilikuwa miongoni mwa makada 24 waliojitokeza kugombea ubunge wa jimbo hilo.

"Ni kweli Hersi ni miongozi mwa watiania wa nafasi ya ubunge ndani ya chama chetu, subirini taratibu zingine tutawajulisha, bado tunasubiri majina tuanze kampeni," alisema Mkaugala.

Hata hivyo, kwenye orodha iliyotolewa baadaye, jina la Hersi halikuwemo, sawa na la Mwalimu Deus Seif, mgombea aliyeshika nafasi ya tatu kwenye kura za maoni.

Hii ni mara ya pili kwa jina la Hersi kuondolewa kwenye mchakato wa ndani ya CCM katika majimbo mawili tofauti.

Awali, Hersi aliomba katika Jimbo la Kigamboni lakini majina ya walioteuliwa yalipotangazwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Amos Makala la kwake halikuwemo.
Safi sana wajumbe
 
Huyo kichwa sungwi tu. Wewe huku umekatwa, ukiende kwingine si utabebenwa vile vile. Chama ni kile kile, maelekezo ni yale yaleee. Kaumbuka, hatakiwiiii!!
 
Waliambiwa wasaidie Yatima hawataki,ona Sasa m1:ya form umeenda Bure Kigamboni:500,000,Kongwa:500,000,arudi tuu Yanga huko!
Huko nako asubiri rungu la FIFA. Tamaa ya fisi- amekosa vyote. Na endapo rungu la FIFA likiwa zito kwelikweli sijui kama wanachama wa Yanga watamwacha salama.
 
Duh kwahiyo Hersi ni incompetent Vs hawa wengine? yaani pale mjengoni watu ni competent kuliko dongo janja Hersi ?
Ngoja niendelee kutafakari.

Safarini Benghazi - Libya
 
Aliyemchinja ni boss wake Gharib kuanzia Kigamboni na sasa KONGWA

HANA AKILI ZA KUMJUA MCHAWI WAKE

GHARIB BADO ANATAKA KUENDELEA KUMTUMIA HAPO YANGA ILI ATIMIZE MALENGO YAKE
Nimeandika same thing nikafuta, Tusigombanishe watu 😅

GSM hawashindwi kitu wakiamua, ila hapa kuna namna. Shida ya kufanya kazi na hawa watu waasia siku wakimalizana na wewe wanakudump kama hawajawahi kukujua, na unageuka adui….Hersi atakuwa analijua hili anatafuta pakutokea.

Ila kwasasa as long as wanamuhitaji bado watatumia kila manipulation kumbakiza. Unless aamue kuacha kazi abaki nyumbani.

In a way nimeonea huruma.
 
Nimeandika same thing nikafuta, Tusigombanishe watu 😅

GSM hawashindwi kitu wakiamua, ila hapa kuna namna.

Jamaa yupo very organized and goals oriented.

Kwahiyo Maboss Kama Gharib wanaangalia faida zaidi .

Angekuwa anataka huyo jamaa apate Ubunge ingelia simu moja na angepata .
 
Kama ilivyolia simu moja tu FA akapata Handeni 2020.
Absolute is okay .

Hersi Said hata Mimi ningekuwa ndo huyo Garib ningemzunguka inshort jamaa yupo well organized .

Ukimtazama Hersi Said unaona kuwa jamaa Ana potential kubwa .

Nafikiri amefanya wrong move Kutaka kuandaa Empire yake kipindi ambacho boss wake anamuhitaji Sana

Watu wa vile akiondoka kumpata huchukua muda mrefu
 
Nimeandika same thing nikafuta, Tusigombanishe watu 😅

GSM hawashindwi kitu wakiamua, ila hapa kuna namna. Shida ya kufanya kazi na hawa watu waasia siku wakimalizana na wewe wanakudump kama hawajawahi kukujua, na unageuka adui….Hersi atakuwa analijua hili anatafuta pakutokea.

Ila kwasasa as long as wanamuhitaji bado watatumia kila manipulation kumbakiza. Unless aamue kuacha kazi abaki nyumbani.

In a way nimeonea huruma.
Hersi ni kiongozi mzuri.. na anaweza kufanya kazi vizuri kabisa ila sasa kulingana na upepo uliopo sasa hivi ilikua sio afya yeye kwenda kongwa .. maana tulilifahamu ili kuwa hersi anajiandaa kugombea kongwa tangu 2024 ..
Watu wangeunganisha dot.. na suala la.kifo cha Ndugai na ukaribu wa Gsm na msoga.. kiufupi Ndugai kifo chake ni planned

Ngoja nikupe thread

Hii hapa

 
Huyu naye hana akili tu, wewe umetemwa kigamboni lakini bado ameenda kwa marehemu. Hawa GSM wanadeal gani?
Kikwete kwa kupitia Samia anataka kujaza chawa wao kwenye bunge ili wapitishe ile Katiba yao ya kishenzi waliotaka kuipitisha huko nyuma ikashinfikana!
Huyu ni mshenzi mmoja adui mkubwa wa nchi hii.
 
Back
Top Bottom