Hesabu zinambeba Dkt. Mwigulu Nchemba

Hesabu zinambeba Dkt. Mwigulu Nchemba

Hao ulio wataja hawawezi kukupa sifa za ukweli watakudanganya ili upotee ili mambo yao yafanikiwe
 
Wanajamvi wasalaam.

Napitia report ya AFDB, IMF na World Bank hakika ni report zilizoshiba sana.

Report hizi kwa pamoja zimeangazia masuala mtambuka, waataalamu mahiri wa uchumi wamechambua kinagaubaga.

[emoji117] Projection ya uchumi iko vizuri sana, uchumi unakuwa kwa kasi sana kuliko taifa lingine ukanda wa sub sahara.
[emoji117]Reserve ipo stable, hivyo hakuna tishio kwa wawekezaji.
[emoji117]Inflation iko undercontrol kuliko nchi zote za east africa.
[emoji117]Deni la serikali bado liko kwenye standard ya nchi zenye madeni madogo sana na linalipwa on time.

[emoji117] Sera za monetary and fiscal policies zinafuatwa kwa usahihi, niko controlled.

Hii sio bahati mbaya bali ni matokeo ya management nzuri inayofanywa na wizara ya fedha chini ya Dkt Mwigulu Nchemba.


Muda ni hakimu mwema.
Mara nyingi nimesema kwamba kama mnamshutumu Mwigulu Kwa sababu za udhaifu binafsi ya ujivuni,kiburi na jeuri sawa ila linapokuja swala la kile ambacho Dunia inakiamini ambacho ni namba basi Yuko sahihi na ame outperform.

Kiongozi makini hawezi mtoa Waziri wa Fedha ambae amesimamia uchumi vizuri kisa Majungu.

Nakumbuka Aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha wa South Africa Travor Manuel kama sijakosea kipindi Cha Thabo Mbeki alisimamia uchumi vizuri na alipotolewa Kwa visa vya Kisiasa masoko ya hisa yaliyumba na Hadi Leo hii South Africa Ina struggle na umeme hawana..

So binafsi naomba Mama asisikilize kelele za wajinga maana kwanza hawatoi options na hoja zao ni hizo za zisizo na mashiko.

Rais Samia tembea na Mwigulu Hadi mwisho ila huko private muonye tuu apunguze ukali wa maneno hata kama Kuna watu wanamuudhi na Bahari nzuri Rais Samia sio mtu wa mihemko kama aliyepita.
Screenshot_20230214-094044.jpg
 
Hao ulio wataja hawawezi kukupa sifa za ukweli watakudanganya ili upotee ili mambo yao yafanikiwe
Kama mambo gani hayo Yao Ili yafanikiwe? Pili wanaoweza kukupa ukweli wa kitakwimu ni kina nani? Nitajie
 
It doesn't matter, serikali lazima iangalie namna ya kufanya ili kuwapunguzia raia wake mzigo wa kupanda gharama za maisha, wananchi wanaungua jua kujitafutia kidogo ambacho kinaishia kwenye bei kubwa ya bidhaa zinazopanda kiholela, hawa hawali data za IMF.
 
haya masuala nilikuwa nayapa uzito unaostahili mpaka niliposoma kitabu cha the confessions of an economic hitman ndipo nilipoelewa ukweli nyuma ya hizi takwimu. Najua vitabu vipo vingi sana lakini kama hujakisoma hiko nakusisitiza kitafute kitakupa mwangaza mkubwa sana.
Mkuu share softcopy kama unayo.
 
Mkuu share softcopy kama unayo.
Hicho kitabu kiufupi kinaelezea kwamba Serikali ikishirikiana na makampuni, mataasisi na mifumo mingine huandaa taarifa za uuongo yaani fallacy Kwa ustadi mkubwa na huwatumia watu wanaolipwa sana nk Ili kuelezea kwamba mambo mazuri na pia huzusha tarahuki na majanga nk Ili tuu kufanikisha malengo Yao.
 
Kama ni mjomba wako hapo ni sawa ila kama wewe ni chawa mwambie akuongezee mshahara maana unafanya kazi kubwa mno kumtetea.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom