Heshima kitu cha bure. Rais Samia ni lazima aheshimiwe na wote, akosolewe kwa staha na asitukanwe

"Nazi mbovu, harabu ya nzima"

Jifunze kunyamaza dingilai. Sio lazima kila mtu ajue wewe ni mbumbumbu.
 
Samahani, sijasoma bandiko lako lote ila kichwa cha habari kitafanya wengi wasisome.(Mawazo tu) Hali ya nchi kwa sasa waijuia then bandiko kama hili.
 
MAWAZO YA UWANDISHI WAKO BADO NI MGANDO - Huwezi kuandika hoja nzito kama hii bila kupangilia hoja zako kwa mantiki ya msingi kama msomi mzuri - Unakuwa kama hujataka kuandika andiko kama msomi huru nadhani ujitafakari mwandishi kwa hilo maana upo very poor kabisa katika andiko lako unakuwa kama sio msomi au mtu umeenda shule kabisa .....
 
Kwani Rais ni malaika anayetakiwa kujua kila kitu?

Kama sio malaika, akikosea tumuite vipi kama sio mjinga?
Rais sio malaika ni binadamu na anaweza kukosea hili hata mimi nimelisema humu na sio mara moja https://www.jamiiforums.com/threads...-ya-kukoseshwa-tumvumilie-tumpe-muda.1883239/

Anapokosea akosolewe kwa lugha ya staha, huwezi kuandika "Kama Samia angekuwa na akili timamu" "kwasababu ya ujinga"

Mkuu wa nchi ni kama mzazi wako, hata akikosea huwezi uliza kama ana akili timamu au kumuita mjinga huko ni kumtukana!
P
 
Kumuita mzazi wangu mjinga kama hajui jambo fulani ni kosa?
 
Kumuita mzazi wangu mjinga kama hajui jambo fulani ni kosa?
Waheshimu Baba na mama, upate miaka mingi na kheri duniani.
Japo neno mjinga sio tusi ni kutokujua, kwa vile linatumiwa kutukana, ukimuita mzazi wako mjinga ni kumtukana!, kama ilivyo jina la mama kwa kibantu ni mama, mae, nina, noko, nyoko, lakini kufuatia jina hilo likitanguliwa na jina la kile kiungo cha K, ni kutukana tusi, kwa sasa hata bila utangulizi wa k, huwezi kumuita mama yako mae, nina, noko, nyoko, atahesabika umemtukana.

Kuuliza kama nanii ana akili timamu, na kumuita mjinga sio heshima stahiki inayopaswa kutolewa kwake.

P
 
Unaleta tabia za mawakili wa serikali.

Maneno mengi huku umeshakiri kuita mtu mjinga sio tusi!.
 
Unajisumbua tuu, hakuna nywinywi wala nywinywi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…