MtamaMchungu
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 8,974
- 12,662
Uchaguzi wa 1995 ulikuwa moto balaa... nakumbuka nilikuwa Mbeya, alikuja Mrema palikuwa hapatoshi! Mtiti wake haukuwa wa kitoto.Du kumbe ilikuwa ivi miaka hiyo ikawaje chadema imepata nguvu na mvuto kiasi hiki
Migogoro imekuwa ikififisha sana juhudi za mabadiliko hapa nchini. Hakuna kipindi vyama vya upinzani vimetulia. Baada ya moto wa 1995, NCCR ilijikuta kwenye migogoro mizito balaa; mpaka ikazaliwa TLP na baadae vyama vyote viwili vikapotea. Ikaja CUF, uchaguzi wa 2000 walikuwa moto balaa; nao wameishia humo humo.
Kwenye CHADEMA majaribio ya kuvuruga yamekuwa mengi, ila chama kina roho ya paka! Ilianza na kina Mwigamba, Kitila, Mchange et al; wakadhibitwa. Baadae ikaja Zitto, naye akadhibitiwa; ukaja mkasa wa "kuunga juhudi" nao ulishindwa; ikaja ya Mwambe, Lowassa na Sumaye nalo likashindwa. Sasa ni Covid-19, nalo litapita.
No wonder wanamchukia Mbowe