Abdul Razaq Mkurugenzi wa Bodi amefafanua kwamba mnufaika ataanza kulipa baada ya miezi 24 [miaka 2 ] kama hana ajira.
Baada ya hapo Deni linakuwa kwa 10% kila mwaka.
Watu ambao hawajaajiriwa kwenye sekta rasmi wanapaswa kurejesha 100,000/= au ASILIMIA KUMI 10% ya pato analolipia kodi kwa mwezi.
Kwa sasa BODI ina wanufaika 14,021 wanaorejesha mikopo yao.
Baada ya marekebisho ya Bodi ya mwaka 2016 , ni wazi sasa Bodi itaunganisha mishahara, TIN, Passport na kadi za benki ili wanufaika wote wapate kurejesha kwa wakati.
TLS na JUDICIARY wameshauriwa kuwabana mawakili binafsi ambao wengi ni wanufaika na hawalipi kabiusa. Mawakili wakati wa ku-renew PRACTICING CERTIFICATES watapaswa kuambatanisha udhibitisho kwamba wameanza kulipa deni.
Law firms nyingi Dar es salaam zina hela sana lakini hawalipi.