HESLB: Serikali imeanza kulipa Malipo ya robo ya nne ya Mwaka wa Masomo 2019/2020 kwa Wanafunzi 132,119 Jumla ya TZS 66.9 Bilioni

HESLB: Serikali imeanza kulipa Malipo ya robo ya nne ya Mwaka wa Masomo 2019/2020 kwa Wanafunzi 132,119 Jumla ya TZS 66.9 Bilioni

Aisee kama ni ivo na ada ipungue kama kawaida mana nasoma mda mfupi, moto utawaka wanatuanza hawa watu
 
Kama ilivyo kwenye sheria za bofi ya mikopo, kila mnufaika atapewa kiasi kinachoendana na siku alizokaa chuoni.

Hapo awali kabla ya Corona, boom moja ilikuwa 505000 hadi 52000 lakini kwa mfumo huu itakuwa pungufu.

Je, kama boom limepunguzwa, vipi kuhusu ada na direct cost? Vilipunguzwa kulingana na siku za masomo?
Wengine tunapewa 553,000 mkuu
 
Nawaonea huruma watoto wa wanyonge wanaosoma zama hizi...unaweza kuta kwenye marejesho ya mkopo hizo pesa hazitapunguzwa popote. Ndo maana nikasema hiyo loan board ifutiliwe mbali, utaratibu urudishwe kama zamani kwa wizara ya elimu kutoa ufadhili/ siyo mikopo kwa wanachuo waliodahiliwa vyuo vikuu vya umma pekee.
 
Hivi mbona wasomi wa sasa wa kitanzania mmekuwa wajinga namna hii!!

Nikweli mmefikia hatua ya kushindwa kujua application ya hesabu za(+,-,× na ÷)?.

Mkataba upo wazi kabisa pesa ya chakula na maradhi utalipwa kwa siku utakazokuwepo chuoni kimasomo na Wala siyo kwa semester hivyo kama siku zikipungua unategemea pesa isipungue? Na Kama zikiongezeka unategemea pesa isiongezeke?

Kuhusu suala la directed cost(,otherfees) na pesa ya ada hizi haziwe pungua sabab ya kupungua kwa Siku Maana zenyewe hazilipwi kwa Siku Bali zinalipwa kwa muhula au semester,, hivyo kitu pekee Cha kupunguza hizi pesa nikuondoa semester na Wala siyo kitu kingine..

Swali je Ni chuo gani ambacho kimefuta semester na bado kinawalipisha wanafunzi wake ada?

Mwisho: Tumieni akili zenu kung'amua mambo siyo manakuja kuonyesha Ujinga wenu huku mitandaoni hivyo vichwa mlivyo navyo siyo vya kufugia nywele pekee.
Wasomi wa Tanzania mnatia aibu Sana.
Direct cost udom Ni 750 kwa siku na tulilipa ya mwaka mzima vipi hizo siku amabazo hatutakuwepo chuoni pesa inakwenda wapi?
 
Direct cost udom Ni 750 kwa siku na tulilipa ya mwaka mzima vipi hizo siku amabazo hatutakuwepo chuoni pesa inakwenda wapi?
Mkuu hebu piga picha Kisha utume hicho kipengere elekezi kinachoelekeza kuwa direct cost kwa siku Ni 750 ..

Na unasoma Udom ipi wewe Ambayo direct cost inalipwa kwa Siku..
Wasomi wa Sasa bhn [emoji16].
 
Mkuu hebu piga picha Kisha utume hicho kipengere elekezi kinachoelekeza kuwa direct cost kwa siku Ni 750 ..

Na unasoma Udom ipi wewe Ambayo direct cost inalipwa kwa Siku..
Wasomi wa Sasa bhn [emoji16].
Direct cost Ni hiyo kwa siku inajumlishwa inalipwa yote unapofanya usajili kuanza mwaka mpya wa masomo. Likizo ya March nayo hua inamalipo kwa wanaobaki chuoni malipo Ni hayohayo.
 
fafanua na ulipaji wa hilo deni... na ile jumla ya pesa wanazoonyesha kwenye account ya muhusika...

je kama kwenye account inaonyesha una jumla ya 3459000 na jumla ya pesa ya kula ikiwemo...
na kwa situation iliyotokea hilo deni linakuwa hivyo hivyo kamili ama kunakuwa na deduction ya hiyo pesa walioipungiza..????

Sent using Jamii Forums mobile app
Duduction lazima iwepo boss Na inashauriwa Mnufaika wa mkopo atunze kumbukumbu za pesa anazopewa na loan board ili ikitokea Deni la mwaka mzima limekuwa kubwa kuliko pesa halisi aliyopewa aweze kudai haki yake katika ofisi husika.

Tatizo Wasomi wa Sasa wanajali kutanua tu boom halafu wanajisahau kukagua muenendo wa Deni lao.
 
Habari zenu wanajanvi.

Ni dhahiri kuwa wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali wameishapokea pesa zao za chakula na Malazi. Ila kimetokea kitu cha ajabu sana kwa pesa imekuja pungufu mno. Hivi kweli mwanafunzi hana haki et. Inauma sana
 
Naskia ni 365000.


Hapo MTU huna hela ya field na unaenda insemister field mkoa fulani na utajua Maisha ni nin?
 
Mbn kama wamekataa hii taarifa, kama ni kweli basi ni hatari
 
Hii kitu ni serious
Screenshot_2020-07-22-21-30-32-12.png
Screenshot_2020-07-22-21-29-52-71.png
Screenshot_2020-07-22-21-30-16-39.png
 
Habari zenu wanajanvi.

Ni dhahiri kuwa wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali wameishapokea pesa zao za chakula na Malazi. Ila kimetokea kitu cha ajabu sana kwa pesa imekuja pungufu mno. Hivi kweli mwanafunzi hana haki et. Inauma sana
Ccm oyeee!!, nyie wasomi October 28 msifanye makosa
 
Wewe ulitaka bei gani? tena ushukuru kuipata hiyo pesa ya bure kuna wenzio wanasoma kwa shida sana.
 
Back
Top Bottom