Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Maroketi ya Hezbollah hapo jana yamerushwa maeneo nyeti sana ya Israel hasa kaskazini.Hali hiyo imemfanya Netanyahu aitishe kikao cha dharura kujadili mabadiliko ambayo yamezidisha hofu kote kote nchini humo.
Ving'ora vimewashwa kote kuwafanya watu kuingia kwenye mahandaki yao.Uwanja wa bengurion umefungwa kwa muda.
Kwa upande mwengine HizbuLlaah wamekanusha madai ya Netanyahu kwamba walifanikiwa kuipiga mitambo yote ya kurushia maroketi wakati yakiandaliwa kufanya mashambulizi.
Baada ya mvua hiyo ya makombora HizbuLlaa wamesema hatua ya mwanzo kulipiza kisasi cha kifo cha kamanda wake Fuad Shukr imemalizika.Katika ujumbe huo wamesema mashambulio yao dhidi ya Israel yatasimama mara tu vita vya Gaza navyo vikisimamishwa.