Deception mimi niko interested na cannibas oil.
Sijui inapatikanaje sasa?
Najua kutengeneza medicinal oils na baby oils.
Ambayo nachukua any vegetable oil nachanganya na herb yoyote mfano lemon grass halafu naweka kwenye sufuria dogo. Jikoni nabandika maji kwenye sufuria kubwa halafu lile sufuria lenye oil na herb naweka ndani ili ichemshwe na joto la maji (not more than 100 degrees Celsius). Sasa na kwa cannibas sativa nafanya hivyo hivyo?...
Cannabis oil/Hemp oil huwa kuna watu wanaifanya kama biashara kwa kuitengeneza wao wenyewe kama Rick Simpson alivyoelekeza.Lakini kwa hapa kwetu hamna watu hao.Wengi wapo Canada,Mexico na Marekani na huwa hawaruhusiwi kuuza nje ya nchi zao(unaona utata huo?),mimi nilishawahi kuulizia kampuni moja Canada ili ninunue lakini walisema hawauzi nje ya nchi kwa kuwa sheria zao haziruhusu,baada ya kuwabana sana wakasema hawatengenezi hemp oil.Mimi nilijua kwamba hawaruhusiwi kuuza nje ya nchi lakini niliuliza kwa makusudi ili kupata uhakika kwa maana nilikuwa katika utafiti tu.Mimi mwenyewe najua jinsi ya kutengeneza.Yaani kama ningekuwa mfanya biashara kwenye tiba kama baadhi ya watu walivyodhani,basi mimi ndio ningekuwa naongoza kwa kuuza dawa zenye uhakika wa kutibu magonjwa yote sugu kuliko watu wote hapa Tanzania.
Sasa kwenye moja ya reply zangu nimeweka link ambayo nimeandika jina la RUN FROM THE CURE/RICK SIMPSON,link hii ni documentary ambayo mwishoni Rick Simpson mwenyewe anaonesha jinsi ya kutengeneza Hemp Oil/Cannabis oil kutoka kwenye bangi/cannabis,ni rahisi sana ukifuatilia na kila mtu anaweza kutengeneza mwenyewe nyumbani.Fuatilia hiyo documentary utaelewa tu.Watu wanaona haya mambo kama miujiza lakini ni kweli kabisa na hii ni kwasababu tumedanganywa kwa muda mrefu ndio maana inakuwa vigumu kwa watu kuamini,wewe fanya mwenyewe kwa kuwa kuona ndio kuamini,usisikilize watu wanaopinga bila sababu za msingi.FANYA MWENYEWE,UTAJUA TU.Kama huoni faida utakuja kuniambia hapahapa na wengine wathibitishe,haya mambo sio blaa blaa,hii ni sayansi.
...By the way bungeni weshapitisha hiyo cannibas kutumika kama dawa?
Yaani mkuu hapa ndio napata homa nikiwaza hili.Hata wale wababe wenyewe waliotushinikiza tufuate sheria hii kwamba bangi ni haramu,wameshaitoa bangi kutoka schedule I drug kwenda schedule II drug ambapo bangi sasa imethibitishwa kuwa na medicinal value.Lakini hii dunia yetu huku kwetu ni dunia ya giza,hao 'miungu' waliotuaminisha kwamba bangi haramu kwa kuiweka kwenye schedule I drug wamebadilika tayari lakini sisi wafuasi bado tuko kulekule,yaani hizi ndio akili mgando ninazozilalamikia kila siku.Bado hata leo hii mtu akikamatwa na bangi ni jela tu bila kujali alitaka kuitumiaje hiyo bangi.Polisi wajinga,wanasheria wajinga,mahakama wajinga na hadi viongozi wa serikali pia ni wajinga,wote ni wajinga,sasa katika nchi kama hiyo unafikiri nani atamwokoa mwenzake?
Hebu chukua mfano mmoja rahisi sana;Panadol ni dawa inayotumika kutuliza maumivu ya kichwa nk,ukimeza panadol kichwa au homa inatulia,hivyo panadol ni muhimu sana kwa matumizi ya binadamu.Lakini ikitokea mtu mmoja kachukua panadol tembe 50 akameza kwa pamoja atakufa tu,sasa je,kufa kwa huyu mtu kwa kumeza panadol tembe 50 inaweza kuwa sababu ya kuifanya panadol iwe haramu na isiruhusiwe kutengenezwa na hata kuuzwa hata madukani?Najua kila mtu atasema hapana,na huo ndio ukweli.Hili liko wazi kwamba uharamu wa kitu uko kwenye matumizi yake.Lakini je,kwa nini mpaka leo hii serikali yetu ni wajinga hivyo kiasi cha kumfunga mtu yeyote atakayekamatwa na bangi bila kujali anataka kuitumia bangi kwenye matumizi gani?
Hapa ndipo utakapoona kwamba ujinga ni kitu kibaya sana na hasa pale ambapo mtu atashindwa kugundua kwamba yeye ni mjinga kwa kuwa kila kitu kipya hakitamwingia akilini hata kama kina mantiki.Ukiwa unajua kujieleza vizuri mahakamani huwezi kufungwa hata kama wamekukamata na bangi tani 20,kwa kuwa sheria zao wenyewe zinawabana.Kwa hiyo mkuu sisi bado tuko gizani na bado sijui tutauona mwanga lini.Wewe kwa sasa nitakachokushauri ni kutumia elimu hii kwa manufaa yako na watu wako wa karibu.