Kutokana na kutingwa na mihangaiko nimechelewa kumjibu bwana deception ila sasa nitajaribu kadri nitakavyoweza natumai watu wengi watajifunza
Kwanza kabisa nitaeleza kwa ufupi kuhusu kansa maana hapo ndio tumetofautiana na bwana deception, na itakuwa kwa faida ya wengi maana pamoja na yeye kuielezea vizuri, ameiandika kwa lugha ya kiingereza kwa hiyo mimi nitaelezea kwa Kiswahili.
Miili yetu imejengwa na viini hai (cells). Tabia ya cells ni kujigawanya mara mbili (cell division) mpaka itakapochoka na kufa. Kujigawanya huku husimamiwa na genes. Kila cell inapojigawanya kuna makosa hufanyika ila genes inayosimamia ugawanyo huu utafuta makosa hayo na kujaribu kuyarekekebisha.
Wakati mwingine makosa hayo hushindwa kurekebishwa na kusababisha cells kujigawanya bila utaratibu na kwa kasi zaidi ya kawaida na kutengeneza cells zisizo za kawaida
.hii husababisha tumors ! Tumors hutengeneza mishipa ya damu ili kuizunguka ili kuhakikisha haifi(angiogenesis)
Kupitia mfumo wa damu cells za tumors usafiri kuelekea sehemu nyingine za mwili na kusababisha KANSA.
Nini husababisha tumors ambazo hupelekea kufanya kansa ndani ya mwili? Kwa ufupi hakuna sababu moja inayosababisha kansa. Ni mjumuiko wa vinasaba tunavyorithi (genetic), mazingira yanayotuzunguka (air pollution etc), aina ya maisha tunayoishi (uvutaji wa sigara nk) maambukizi ya virusi na kadhalika.
Njia bora Zaidi ya kupigana na tatizo la kansa ni uzuiaji (prevention)...kansa nyingi zinaweza kuepukwa kwa kubadili aina ya maisha kwa kula vizuri, kupunguza uchafuzi wa mazingira, kupunguza matumizi ya sigara na pombe, kujenga tabia ya kupima afya na kadhalika..
Tiba ya kansa imegawanyika katika aina tatu
.upasuaji, tiba ya mionzi (radiotherapy) na tiba ya kemikali (chemotherapy). Kama zilivyo tiba nyingi za magonjwa mengine
tiba za kansa zina madhara na mapungufu yake pia mfano chemotherapy haiwezi tibu kansa ya ubongo pia sio mara zote hufanya kazi. Pamoja na mapungufu hayo bado zimeonyesha mafanikio makubwa kwa wagonjwa.
Bwana deception ni shabiki wa tiba asilia (naturopathy treatment) na anasimamia hasa tiba kupitia chakula..Nakubaliana nae kuwa chakula ni tiba ndio maana nimesema kula vizuri kunaweza kuzuia kansa kwa kiwango kikubwa ila sikubaliani nae kuwa baada ya kansa kutokea basi diet Fulani inaweza kutibu hiyo kansa
Ni ukweli kwamba kama mwili ungeachwa ujitibu wenyewe labda na chakula tu basi binadamu asingeweza kuishi zaidi ya miaka 45
.. hii inathibitishwa na kuongezeka kwa survival rate ya wagonjwa wa kansa kwenye nchi zilizoendelea kuliko nchi masikini ambazo wagonjwa wa kansa hukosa tiba sahihi nilizotaja hapo juu. Pia tukubaliane kwamba hizo tiba asilia natural remedies zilikuwapo kabla ya hii mainstream medicine ila kwa sababu haina scientific facts haijawahi kuwa na mafanikio kama mainstream medicine. Natural remedies ni placebo tu hamna la Zaidi.
Pia ndugu zangu wasidanganyike na neno natural maana sio kila kitu natural ni safe au effective. Hawa wanaojiita naturopathy doctors hawana natural diagnostic tests zozote
hata explanation ya magonjwa wameiba kwenye mainstream medicine maana kabla ya hapo hawakuwi kuelezea jinsi ugonjwa unavyotokea (physiopathology) kwa kutumia scientific facts, yote haya yamefanywa na mainstream doctors na scientists ambao leo hii wanaitwa wasiojua ama waficha tiba/ukweli.
Kinachoumiza hawa wagonjwa baada ya kuhangaika na tiba za aina hizo hurudi hospitali wakiwa terminal stage.
Hakuna kitu chochote kilichofichwa....hizi tiba za natural remedies zipo miaka tele na mpaka leo kuna clinics ziko wazi huko magharibi kwa kila mtu anayetaka kwenda kujaribu.... Ila mafanikio yake huwezi kucompare na mainstream medicine ndio maana mahospitalini kumejaa.
Just a simple fact
.nchi kama ya Tanzania ambayo wananchi wengi hawana access na tiba za mahospitalini kama marekani tungetegemea life expectancy yetu iwe juu lakini sivyo hivyo kabisa
.pamoja na kutegemea hizo natural remedies bado magonjwa madogo madogo yanatushinda.
Ndugu zanguni dawa ni kuishi healthy life kwa kula vizuri, jali usafi, fanya mazoezi, jenga utaratibu wa kupima afya hata kama huna magonjwa, na mwone dakari ukihisi ugonjwa. Haya mambo ya kutibu kansa na mihogo yalishatuponza tusirudie kosa. Diet itabadili vipi gene mutation jamani.
Mwenye macho aone....nakaribisha majibizano ya kistaarabu...ukileta jazba sitajibu.
Deception RGforever kupe