Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kumbe ni haya matunda... hapa iringa yanaitwa mapindigesi.. ni matunda yanayolimwa sejhemu za baridi... yanapatikana sana wilaya ya mufindi
Nimejaribu Kutafuta Source Za Vitamin B17 nimepata hizi hapa hope zitasaidia
Zinazopatikana kwa Urahisi zaidi na Zina High amount
1. Mihogo (cassava)
2. Mbegu za Mapeazi
3. Mbegu za Apple/Tufee
Zingine unaweza Pata hapa
Foods Containing B17 (Nitrilosides)
Mkuu RGforever ahsante,nimeangalia hiyo website ulioiweka hapo ,nimekuta vitu vyingi ndugu zanguni tuleni Mihogo,viazi vitamu, magimbi, Maharage .
Shida ya magimbi zinatoka kwa msimu, ingekuwa ni kila siku aaaa ningekula sana, yaani jamii za mihogo ndo zinatokaga kwa misimu sana!
watu ambao hawajaelimika, sanasana waafrika wanakufa kwa speed sana sababu ya vitu kama hivi, ulichoandika hapo juu hakina ukweli wowote! kusema pharmaceutical industries zinafaidika sana ndo sababu wanaziba ukweli kuhusu treatments ni uongo mtupu.
Mkuu unajua kweli hata process ya cancer ilivyo? tatizo moja la mtanzania akiambiwa tu kua achana na hizo dawa za wazungu zina madhara, tumia hii ya asili anarukia fasta, tena kudanganywa zaidi anaambiwa watu wengi wametumia wakapona, anakomaa nayo mwisho wa siku anakufa..
Kama una cancer, pitia tu hizo options ambazo ni bei kubwa, huna option nyingine hadi pale cure itakapopatikana, yaweza kua kesho, ama kesho kutwa ila itabidi usubiri tu. Njia nyingine zote endelea kupoteza muda mwisho wa siku uifanye iwe worse tukuage, cancer kwenye first stages inatibika kirahisi tu, ila mnavoendekeza njia za asili inakua inafika stage inakua haiwezi kua controlled tena..
Ningekua admin wa jf post kama hizi ningefuta sababu ni za uongo mtupu, zitaua watanzania maana wao ni mstari wa mbele kuamini kila wanachosoma kwenye internet
Suala siyo kufa, suala ni kulinda afya zetu kwa kujenga afya zetu kwa kutumia vitu alivyotupa Mungu, kwanini mungu kaumba hivi vyakula vya asili? na baadhi yake vingine vinatumika kama dawa!
Ni afadhali kujenga miili bora kwa kutumia vyakula vya asili kuliko kushinda kwenye mionzi na kuharibu kwa kiwango chochote kwa kutumia vitu visivyo salama!
Wachina wanajali sana vitu vya asili na ndo maana afya zao ziko bora sana, kwanini tusijenge tabia ya kujali vitu vya asili?
Mkuu huyu jamaa anaongelea 'cure' for cancer sio prevention, mtu ukiishi healthy siku zote unakula vizuri na unafanya mazoezi utaishi vizuri na vitu kama cancer au magonjwa mengi hutogusa...
Sema tukija kwenye swala la cure, mtu ambaye cancer ishakua, kusema kuna njia za asili kutibu ni kudanganya watu tu ambao wana uhitaji mwisho wa siku wanapoteza muda kua na false hopes na vitu ambavyo havifanyi kazi au mbaya zaidi kupoteza maisha..
Watu walio kwenye matatizo hua wako desperate sana, wako easily deceivable, nadhani unakumbuka babu wa lolliondo kama mfano mzuri, sasa mtu akiwa na cancer anaweza akaona hii kitu akaachana na njia sahihi akaenda kula mihogo sijui madude gani mwisho wa siku tatizo likazidi
Naona kama unamshambulia mleta hoja bila ya hata kujadili hoja yenyewe,uzuri ameweka links za wapi alikotoa anachokizungumzia lakini hata hutaki kugusia huko na wala hujathibitisha sehemu yoyote kuwa jamaa ni muongo.
Nahisi una wivu
Nadhani hujasoma kua nimepinga alichosema jamaa, ndio kudiscuss hoja kwenyewe huko, hujasoma post zangu uanzia pale juu umesoma reply niliyomjibu mtu alafu unakuja na conclusion.. Hehehe! wivu wa nini? wivu wa kuanzisha thread JF?? hilo si ni swala la bure au? Nimeipinga hoja kama umesoma post zangu hapo juu, na nimeeleza wazi kabisa kua it won't work. Wabongo kwa kuamini conspiracy theories mmejaliwa, mtabaki nyuma hadi siku jua lilipuke.
Wewe leta discussion yako sasa, umechangia nini kwenye hoja ya jamaa kuliko mimi niliyempinga??
Ila Mkuu Deception nina Maswali mawili ya Kuanzia..
1. Je mtu atumie mda gani Dozi ya Kuweka Mwili Katika Hali ya Alkaline. Mfano Kutumia Juisi ya Malimao
2. Na Muda Gani pia Mtu atumie kuondoa Sumu mwilini..
watu ambao hawajaelimika, sanasana waafrika wanakufa kwa speed sana sababu ya vitu kama hivi, ulichoandika hapo juu hakina ukweli wowote! kusema pharmaceutical industries zinafaidika sana ndo sababu wanaziba ukweli kuhusu treatments ni uongo mtupu....
...Mkuu unajua kweli hata process ya cancer ilivyo?
...tatizo moja la mtanzania akiambiwa tu kua achana na hizo dawa za wazungu zina madhara, tumia hii ya asili anarukia fasta, tena kudanganywa zaidi anaambiwa watu wengi wametumia wakapona, anakomaa nayo mwisho wa siku anakufa..
..Kama una cancer, pitia tu hizo options ambazo ni bei kubwa, huna option nyingine hadi pale cure itakapopatikana, yaweza kua kesho, ama kesho kutwa ila itabidi usubiri tu...
..Njia nyingine zote endelea kupoteza muda mwisho wa siku uifanye iwe worse tukuage, cancer kwenye first stages inatibika kirahisi tu, ila mnavoendekeza njia za asili inakua inafika stage inakua haiwezi kua controlled tena..
..Ningekua admin wa jf post kama hizi ningefuta sababu ni za uongo mtupu, zitaua watanzania maana wao ni mstari wa mbele kuamini kila wanachosoma kwenye internet
Bado hujanipa maelezo ya kutosha huyo binti alitibiwa hospitali gani na alipewa dawa gani.
Kwa maelezo yako inaonekana huyo binti atakuwa na ugonjwa uitwao vitiligo,ugonjwa huu mara nyingi unasababishwa na kinga ya mwili kushambulia mwili wenyewe maeneo mbalimbali kama vile tishu nk,kwa huyu biti yeye ngozi yake ndiyo hushambuliwa.
Sababu kubwa ya ugonjwa huu ndio hiyo niliyoeleza hapo juu au kwa kifupi tunaita 'autoimmune'.Magonjwa aina hii ndio ambayo hospitali huwa hawawezi kuyatibu zaidi ya kuondoa dalili.Kutokana na sayansi ya ugonjwa huu ulivyo,hata tiba hii ya cancer niliyoeleza,yaani vitamin B17 na mtiririko wake unaweza kumtibu vizuri kabisa huyo binti.Ukimpima huyo binti pH ya damu yake,lazima atakuwa acidic zaidi,ukitaka kuamini we nenda kajaribu uone.
Nikupe faida nyingine ya vitamin B17.Bila kujali kama una cancer au la,vitamin B17 pia huweza kutumiwa kama cosmetic ya asili hasa kwa wanawake.Vitamin B17 inapotumiwa,ukiachilia mbali kukulinda dhidi ya magonjwa sugu kama cancer pia inaweka ngozi katika hali ya ubora.Na kama wanawake watagundua siri hii basi hawawezi tena kuhangaika na vipodozi vyenye kemikali chafu.Vitamin B17 ina tabia ya kuondoa mabaka,rangi nyeusi za makovu ya vidonda au vipele kwenye ngozi,mikunjo ya ngozi na kuiweka ngozi katika muonekano mzuri kama mtu atakuwa na tabia ya kuitumia mara kwa mara.Yaani vitamin B17 hutambua vitu ambavyo si vya kawaida juu ya ngozi na kuviondoa.
Exactly.. Ndio hizo mkuu
Mwanzoni nilisema kwamba tiba hizo nilizotaja haimaanishi kwamba mgonjwa anatakiwa azitumie zote,la hasha,ila hutegemeana.Nilizungumzia hatua tatu za kutibu cancer ambazo ni kuweka pH ya damu iwe alkaline,kuondoa sumu na kuua chembe za cancer.Sasa ukiangalia vizuri kwenye tiba tajwa hapo juu utaona kwamba hatua zote tatu unaweza kuzipatia ufumbuzi kutokana na hizo tiba.
Cha msingi kukumbuka hapa ni kwamba,hatua ya kwanza na ya pili ni lazima kuzipitia.Sasa kwenye hatua hii ya tatu ya kuua chembe za cancer tayari nimeshazungumzia vitamin B17 na utaratibu wake wa matumizi.Tiba nyingine ambazo zinaweza kutumika kwenye hatua hii ya tatu ni Cannabis oil/Hemp oil.Hii ndio mojawapo ya sababu ambayo imeifanya bangi kupigwa marufuku na watu wabinafsi wanaolinda biashara zao.
Hifadhini hizi nyaraka hapo chini kwa ajili ya kumbukumbu zenu kwa yale ambayo tumeshayaongelea tayari;