Hii changamoto ya majungu kwenye ajira mnapambana nayo vipi wenzangu?

Hii changamoto ya majungu kwenye ajira mnapambana nayo vipi wenzangu?

Mzee yaani Bora wewe unapigwa majungu kazini je sisi ambao Wana wakiona umepanda kidogo tu kosa mtaani yaani kijiweni ukifika unatakiwa uwe wa mwisho kuondoka ukiondoka wa kwanza nyuma lazima usemwe
 
Shukuru hapo ni majungu tu.. Kuna sehemu nyingine na uchawi upo..

Kikubwa ni kuwa mvumilivu.. Changamoto haikimbiwi.. Changamoto inakabiliwa.. Kuwa mpole, angalia majukumu yako.. Timiza majukumu yako kwa wakati.. Usijibizane na mtu hapo ofisini.. Siku zote kwenye ukweli uongo hujitenga.. Njia ya muongo ni fupi.. Ipo siku ukweli utajulikana na utaishi kwa amani..
 
Nashukuru sana mkuu.
 
Kila penye ridhiki hapakosi majungu, ziba masikio piga kazi kwa bidii weka mipango yako.
Vijana hao hawajitambui mkuu. Yaani vitu vidogo vidogo kama hivyo vinaamkatisha tamaa. Wapi ambapo hakuna majungu kwa sisi ngozi nyeusi. Yaani watu unaokaa nao masaa 7 au 8 wakuumize?

Nijuavyo kwenye maisha yetu ya kiswahili, huwezi kutoboa bila kujifunza kupuuzia na kuacha mambo yapite. We unatakiwa kusimama katika unyoofu na kutimiza wajibu wako, hayo mengine unatakiwa uyapuuzie.
 
Habari wana jukwaa?
1.Unaamka asubuhi na stress unajiuliza leo itakuaje tena nini kitatokea huko?
2.Kuna wale wanajua kujipendekeza kwa boss na kujifanya wanainformation zote jinsi shughuli za kiofisi zinavyokwenda(Machawa).
3. Kuna wale wana vijikundi vyao vya masengenyo, hao ukitoka tu wanakusema , kuna muda wanasemana mpaka wao wenyewe.
4. Kuna yule boss mwenyewe kutwa kujinunisha, salamu usipo msalimia wewe basi usitegemee yeye kuanza kukusalimia wewe.

Wakuu nipo mkoa X napigania ugali, nalipwa 500k taasisi binafsi, ila naona hizi changamoto zinanivuruga sana. Nina Akiba ya 1.5million nategemea mwez wa 11 niwe hata na 3+ million,, nafikiria kuachana na hii kazi kwakweli, nikajaribu hata biashara. Mimi ni wale watu ambao napenda kuyachukulia mambo personal sana sasa Nateseka sana na Mambo kama hayo juu kwenye maofisi, sina Amani kabisa.

Mwenye ushauri tafadhali wakuu.
Natanguliza shukrani
Cha msingi unapiga mpesa? Its enough
 
Pole sana, jambo la kawaida sana kwenye taasisi, hasa hizi za umma, MA HR huwa wanajifanya kana kwamba Taasisi ni za Baba Zao.

Usiache kazi, Biashara fungua huku ukiendelea kufanya kazi. Biashara ikifeli kazi itakupa backup.
 
Mie sijui nimeumbwaje sihangaiki kabisa ni majungu ya watu, iwe jirani au familia nikikujua nakuongeza kwenye 🗑 🚮, nikiweza nakutia block nakupuuza mpk ujishtukie km haupo yani, kwa kazini unatakiwa usalimie shirikiana nao kwenye kazi km kawaida ila habari zisizohusu kazi hapana, mazoea na utani wa kijinga hapana huwezi pendwa na kila mtu we sio fedha
 
Biashara kidogo tofauti na kwenye kufanya kazi hasa private sector halafu ukute bosi anapenda majungu ni noma kuna dada mmoja mume wake akalazwa muhimbili siku kapewa discharge wakapita kwenye mgahawa wapete supu mdau akapita akawaona kesho yake kafika kikao cha kusema uongo.

Kikubwa wasikujue na usiwe na kundi kazini au kwa wanawake kuendekeza ushoga kwa ujumla usitabirike ila mtu akiingia anga yako ukijiridhisha mzingue.. Watapika mambo ila watakosa mengi yanayokuhusu itafika mahali watu watakukutea mbona yule hana mpango na mtu mnamsingizia.
 
Nashukuru sana mkuu.
Million3+ sina mke sina mtoto,, naona kwa biashara naweza nikafunguliwa na mtoa riziki.
Mkuu kwenye biashara ndiko pasua kichwa!! Hiyo pesa milioni 3!!unaiona nyingi?!! Hahaaa, unaanza tu biashara TRA, hao, manispaa hao, wanataka chao!! Huku kama una roho nyepesi na huna kazi nyingine, ndio utegemee hapo hapo, ni balaa, labda uanze biashara wakati bado upo kazini, kuna unafuu,
 
Kazi za mshahara mdogo majungu kama yote yaan nimewahi kuwa mkuu wa shule ya binafsi yaan watt wakichelewa kula dk 10 manager kapiga simu, nimesoma mambo anachokiongea mtoa mada nakijua mtoa mada kwenye education sector hasa vyuo ya ualimu vya diploma, secondary na msingi kuna majungu balaa utachunguzwa unavaaje, unakulaje utachimbwa vibaya halafu kuna watu full kujipendekeza kwa bosi.
 
Ukisoma lugha zilianzaje au kwann binadam alianza kuzungumza, Bw Muller anasema lugha zilianzia kwenye kupeana umbea, Mfano umeenda kuchota Maji ukakutana na kitu huko ukirudi utatamani kumuelezea mtu aliepo nyumbani,
Eventually lugha zikaanzia hapo,
Kwahyo asilia ya lugha ni umbea, kwahyo usichukie na usitake personal
 
Back
Top Bottom