Hii changamoto ya majungu kwenye ajira mnapambana nayo vipi wenzangu?

Hii changamoto ya majungu kwenye ajira mnapambana nayo vipi wenzangu?

Habari wana jukwaa?
1.Unaamka asubuhi na stress unajiuliza leo itakuaje tena nini kitatokea huko?
2.Kuna wale wanajua kujipendekeza kwa boss na kujifanya wanainformation zote jinsi shughuli za kiofisi zinavyokwenda(Machawa).
3. Kuna wale wana vijikundi vyao vya masengenyo, hao ukitoka tu wanakusema , kuna muda wanasemana mpaka wao wenyewe.
4. Kuna yule boss mwenyewe kutwa kujinunisha, salamu usipo msalimia wewe basi usitegemee yeye kuanza kukusalimia wewe.

Wakuu nipo mkoa X napigania ugali, nalipwa 500k taasisi binafsi, ila naona hizi changamoto zinanivuruga sana. Nina Akiba ya 1.5million nategemea mwez wa 11 niwe hata na 3+ million,, nafikiria kuachana na hii kazi kwakweli, nikajaribu hata biashara. Mimi ni wale watu ambao napenda kuyachukulia mambo personal sana sasa Nateseka sana na Mambo kama hayo juu kwenye maofisi, sina Amani kabisa.

Mwenye ushauri tafadhali wakuu.
Natanguliza shukrani
Kwenye biashara kuna chuma ulete, ukikaa vibaya unapigwa kombora, mbali na hayo majungu
 
Usiishi kwa kuangalia watu wanasema nini au wanafanya nini
fanya kazi zako pokea mshahara wako mengine achana nayo,

huku kwenye biashara kuna makubwa zaidi kama maneno yanakuumiza huku utachizika ndugu
Hayo matatizo yako serikalini huko watu hawana sifa za kazi halafu wanapewa kazi au ajira wawe wakubwa au wadogo

Nenda sekta binafsi hasa za watu weupe awe mzungu,mhindi au Mwarabu au mpemba

Ujinga wa wafanyakazi kuongea ongea hawataki fanya kazi iliyokuleta full stop

Haiwezekani mtu anatoka nyumbani kwenda kazini kuongelea mbo ya Simba na yanga au majungu yoyote hamna mfanyakazi hapo fukuza wote ajiri wengine ndilo jawabu asibaki mtu hapo

Kama ni ofisi ya serikali wahamishe kama wako dar wapeleke maeneo tofauti tofauti porini huko mikoani hakikisha unampeleka porini hasa bila huruma.Kule akifika akiona na mazingira yalivyo kidomodomo kitaisha
 
Kazi za mshahara mdogo majungu kama yote yaan nimewahi kuwa mkuu wa shule ya binafsi yaan watt wakichelewa kula dk 10 manager kapiga simu, nimesoma mambo anachokiongea mtoa mada nakijua mtoa mada kwenye education sector hasa vyuo ya ualimu vya diploma, secondary na msingi kuna majungu balaa utachunguzwa unavaaje, unakulaje utachimbwa vibaya halafu kuna watu full kujipendekeza kwa bosi.
Kweli kabisa mkuu, yote haya ninayapitia.
 
Habari wana jukwaa?
1.Unaamka asubuhi na stress unajiuliza leo itakuaje tena nini kitatokea huko?
2.Kuna wale wanajua kujipendekeza kwa boss na kujifanya wanainformation zote jinsi shughuli za kiofisi zinavyokwenda(Machawa).
3. Kuna wale wana vijikundi vyao vya masengenyo, hao ukitoka tu wanakusema , kuna muda wanasemana mpaka wao wenyewe.
4. Kuna yule boss mwenyewe kutwa kujinunisha, salamu usipo msalimia wewe basi usitegemee yeye kuanza kukusalimia wewe.

Wakuu nipo mkoa X napigania ugali, nalipwa 500k taasisi binafsi, ila naona hizi changamoto zinanivuruga sana. Nina Akiba ya 1.5million nategemea mwez wa 11 niwe hata na 3+ million,, nafikiria kuachana na hii kazi kwakweli, nikajaribu hata biashara. Mimi ni wale watu ambao napenda kuyachukulia mambo personal sana sasa Nateseka sana na Mambo kama hayo juu kwenye maofisi, sina Amani kabisa.

Mwenye ushauri tafadhali wakuu.
Natanguliza shukrani
Kwa uzoefu wangu kwenye ajira nahisi tatizo ni wewe mwenyewe. Na bila shaka unafanya kazi chini ya uwezo ama wewe ni mzembe. Kama wewe ni mchapa kazi, kazi yako itaonekana tu na majungu yote yatapotea bila kutumia nguvu. Ajabu unajadili mpaka hoja ya kumsalimia bosi wako huo ni udhaifu, kwani ukisalimia unapungukiwa nini? GEN-Z mnamtatizo kweli mnatamani kwenda mahali lakini hamjui mnafikaje.
 
Majungu ni kila mahali mengi mzazi.

Wewe fanya kazi zako kwa muda wako na tambaa. Pia usipende kulilia vitu vya ofisi kama usafiri na vingine.

Ni rahisi sana kuepuka kuwasema watu vibaya ukiwa unajali mambo yako pekee. Wewe mtu akimsema mwingine kuwa ni mbaya wewe onaa ni mzuri ukiona kundi wamekaa hizo ndio mada zao ondoka sehemu hiyo.

Kuwa mtu wa utani na kupotezea mambo wakikufahamu hivyo hawatakupiga majungu wala hawatakuletea stori za watu wengine.

Kuna mahali nimefanya kazi sikuwa na mda na mtu wala stori za kuwasema watu. Wakisema mbaya mi nasema nzuri kuepuka traps ama nasema sifahamu kitu, kila habari wakiileta kwangu naifanya kama ni mpya kabisa na mtu wanayemsema simfahamu hata kama nipo nae ofisi moja.

Wao wenyewe walinyosha mikono na kuniita mimi ni msiri kwa sababu sijawahi kuleta personal issues ofisini pia wananifahamu huwa sichangii kwwnye mada za kusemana na watu na sikuwa napend kutumia vitu public kama magari ya ofisi n.k.

Ukifanya hivi hawakupati na utakuwa na amani kichizi.
 
Ukiwa kazini usitake kuzoweana na watu.. nenda kazini, fanya kazi zako, kuwa bize na mambo yako.. ukitaka hivyo juu utaumizwa sana, waja wana maneno sana.

Usimzingatie mtu, hutasikia hayo maneno na ukiyasikia hayatakuumiza.. usisahau kusali kwa imani yako.
 
Ukitaka kuepuka majungu basi usiishi na watu bali ishi peke yako.....lakini kama kila unachofanya unakifanya ukiwa na watu basi majungu ni sehemu yake. Otherwise kuwa na moyo wa chuma piga kazi!
 
Ungekuwa mwajiriwa wa TAMISEMI, Halmashauri ungeshajinyonga zamani sana, huko kwako kuna afadhali we chapa kazi, huku halmashauri kuna unafiki, majungu na uchawi kutoka kwa wakuu wako wa idara, bado watumishi wenzako kituo cha kazi, bado viongozi wa serikali ya kijiji wakufanyie fitina, bado wananchi wa kijiji bado figisu za Mwenge wa uhuru, ndio maana mimi nimekuwa kama gogo la choo sisikii harufu ya mavi.
 
Back
Top Bottom