Hii changamoto ya majungu kwenye ajira mnapambana nayo vipi wenzangu?

Hii changamoto ya majungu kwenye ajira mnapambana nayo vipi wenzangu?

Nilikutana na kitu ya aina hii kipindi nimeajiriwa aisee kidogo nidate. Ila leo namshukuru sana Mungu asilimia kubwa wapo upande wangu.

Muhimu jitahidi kufanya kazi zako kwa weledi wa hali ya juu taratibu utaanza kuona utofauti japo mwanzo mambo yatazidi kuwa mengi kwa hao machawa wa boss sababu kazi zinazohitaji akili kubwa zote utapewa wewe wao watabaki kupiga story za umbea na boss na hapo kimbembe ndipo kitaanza utachukiwa mpaka na mfanya usafi hapo ofisini kwenu lakini mwisho watanyoosha mikono juu.
Hapoo kwenye kufanya kazi kwa weledi panazimisha midomo machawa wote...wanabaki hawana Cha kusemaa
 
Hio ela nzuri kuna watu hawana hio mkuu kaza roho weka pamba masikioni fanya mambo yako, jipende mwenyewe. Usiache kazi wekeza hio hela ukiwa unafanya. Tafuta kijana wakufanya naye. Usikurupuke sana maana hata kilimo, biashara changamoto zipo haziepukiki, hivyo komaa.
 
Nashukuru sana Mkuu.
 
Majungu ya halmashauri ni next level. Narudia Ukiona sehem mishahara midogo mqjungu yake hapo sio mchezo... Nahisi njaa na majungu vina vinasaba.
Nimecheka sana aisee, halafu bila kusahau chuki na roho mbaya
 
Komaa na kazi

Umewahi itwa na Boss akakuambia ulistahili hiki kitu ila HR aliripoti ishu hii na hii kwa mkuu wa idara?

Komaa mzee.
 
Habari wana jukwaa?
1.Unaamka asubuhi na stress unajiuliza leo itakuaje tena nini kitatokea huko?
2.Kuna wale wanajua kujipendekeza kwa boss na kujifanya wanainformation zote jinsi shughuli za kiofisi zinavyokwenda(Machawa).
3. Kuna wale wana vijikundi vyao vya masengenyo, hao ukitoka tu wanakusema , kuna muda wanasemana mpaka wao wenyewe.
4. Kuna yule boss mwenyewe kutwa kujinunisha, salamu usipo msalimia wewe basi usitegemee yeye kuanza kukusalimia wewe.

Wakuu nipo mkoa X napigania ugali, nalipwa 500k taasisi binafsi, ila naona hizi changamoto zinanivuruga sana. Nina Akiba ya 1.5million nategemea mwez wa 11 niwe hata na 3+ million,, nafikiria kuachana na hii kazi kwakweli, nikajaribu hata biashara. Mimi ni wale watu ambao napenda kuyachukulia mambo personal sana sasa Nateseka sana na Mambo kama hayo juu kwenye maofisi, sina Amani kabisa.

Mwenye ushauri tafadhali wakuu.
Natanguliza shukrani
Acha kuchukulia mambo personal maana majungu yapo hadi kwenye biashara. Utasikia yule jamaa ana ndumba ndio maana anauza sana na story inasambaa mtaa mzima.
Kama boss hana shida na wewe acha tu waongee wewe chapa kazi. Wakenya wanasema talk huwa haipiki rice.
 
Majungu ni kila mahali mengi mzazi.

Wewe fanya kazi zako kwa muda wako na tambaa. Pia usipende kulilia vitu vya ofisi kama usafiri na vingine.

Ni rahisi sana kuepuka kuwasema watu vibaya ukiwa unajali mambo yako pekee. Wewe mtu akimsema mwingine kuwa ni mbaya wewe onaa ni mzuri ukiona kundi wamekaa hizo ndio mada zao ondoka sehemu hiyo.

Kuwa mtu wa utani na kupotezea mambo wakikufahamu hivyo hawatakupiga majungu wala hawatakuletea stori za watu wengine.

Kuna mahali nimefanya kazi sikuwa na mda na mtu wala stori za kuwasema watu. Wakisema mbaya mi nasema nzuri kuepuka traps ama nasema sifahamu kitu, kila habari wakiileta kwangu naifanya kama ni mpya kabisa na mtu wanayemsema simfahamu hata kama nipo nae ofisi moja.

Wao wenyewe walinyosha mikono na kuniita mimi ni msiri kwa sababu sijawahi kuleta personal issues ofisini pia wananifahamu huwa sichangii kwwnye mada za kusemana na watu na sikuwa napend kutumia vitu public kama magari ya ofisi n.k.

Ukifanya hivi hawakupati na utakuwa na amani kichizi.
Nimeipenda hii
 
Habari wana jukwaa?
1.Unaamka asubuhi na stress unajiuliza leo itakuaje tena nini kitatokea huko?
2.Kuna wale wanajua kujipendekeza kwa boss na kujifanya wanainformation zote jinsi shughuli za kiofisi zinavyokwenda(Machawa).
3. Kuna wale wana vijikundi vyao vya masengenyo, hao ukitoka tu wanakusema , kuna muda wanasemana mpaka wao wenyewe.
4. Kuna yule boss mwenyewe kutwa kujinunisha, salamu usipo msalimia wewe basi usitegemee yeye kuanza kukusalimia wewe.

Wakuu nipo mkoa X napigania ugali, nalipwa 500k taasisi binafsi, ila naona hizi changamoto zinanivuruga sana. Nina Akiba ya 1.5million nategemea mwez wa 11 niwe hata na 3+ million,, nafikiria kuachana na hii kazi kwakweli, nikajaribu hata biashara. Mimi ni wale watu ambao napenda kuyachukulia mambo personal sana sasa Nateseka sana na Mambo kama hayo juu kwenye maofisi, sina Amani kabisa.

Mwenye ushauri tafadhali wakuu.
Natanguliza shukrani
Pole..

Be you, kwa kifupi ninachofanya sina upande wowote na ukileta story zako niko bizee na mambo yangu utaongea weee wala hakuna chenye nakusupport labda iwe ishu ya kujadilika sio kumjadili mtu.

Kuhusu biashara kama unataka unaweza anza ukiwa hapohapo kazini ili kuizoea kabla hujatoka kazini..

kama uko Arusha njoo nikuuzie juice ya tende na maziwa inaondoa stress 😩
 
Back
Top Bottom