Hii changamoto ya majungu kwenye ajira mnapambana nayo vipi wenzangu?

Hapoo kwenye kufanya kazi kwa weledi panazimisha midomo machawa wote...wanabaki hawana Cha kusemaa
 
Hio ela nzuri kuna watu hawana hio mkuu kaza roho weka pamba masikioni fanya mambo yako, jipende mwenyewe. Usiache kazi wekeza hio hela ukiwa unafanya. Tafuta kijana wakufanya naye. Usikurupuke sana maana hata kilimo, biashara changamoto zipo haziepukiki, hivyo komaa.
 
Nashukuru sana Mkuu.
 
Majungu ya halmashauri ni next level. Narudia Ukiona sehem mishahara midogo mqjungu yake hapo sio mchezo... Nahisi njaa na majungu vina vinasaba.
Nimecheka sana aisee, halafu bila kusahau chuki na roho mbaya
 
Komaa na kazi

Umewahi itwa na Boss akakuambia ulistahili hiki kitu ila HR aliripoti ishu hii na hii kwa mkuu wa idara?

Komaa mzee.
 
Acha kuchukulia mambo personal maana majungu yapo hadi kwenye biashara. Utasikia yule jamaa ana ndumba ndio maana anauza sana na story inasambaa mtaa mzima.
Kama boss hana shida na wewe acha tu waongee wewe chapa kazi. Wakenya wanasema talk huwa haipiki rice.
 
Nimeipenda hii
 
Pole..

Be you, kwa kifupi ninachofanya sina upande wowote na ukileta story zako niko bizee na mambo yangu utaongea weee wala hakuna chenye nakusupport labda iwe ishu ya kujadilika sio kumjadili mtu.

Kuhusu biashara kama unataka unaweza anza ukiwa hapohapo kazini ili kuizoea kabla hujatoka kazini..

kama uko Arusha njoo nikuuzie juice ya tende na maziwa inaondoa stress 😩
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…