Hii Dharau ni mwisho, Sidhani kama kuna ya juu yake

Hii Dharau ni mwisho, Sidhani kama kuna ya juu yake

Poa,utaacha funguo Kwa jirani au nakukuta ndani?....niandalie na kitaulo Cha kukung'utia vumbi[emoji6]
Funguo utaukuta chini ya jiwe hapa pembeni ya mlango, vitaulo vipo vya kutosha Hadi tissue paper, shughuli ushindwe ww tu yani
 
Polee!!
Kwa hiyo Hela uliyompa as a tip ni sawa kabisa ni vile umemkuta yupo na negative attitude.
 
Funguo utaukuta chini ya jiwe hapa pembeni ya mlango, vitaulo vipo vya kutosha Hadi tissue paper, shughuli ushindwe ww tu yani
Sawa,Haina shida mkuu wangu 🤜
 
Asee kuna watu wanajeuri na madharau katika hii Dunia sijawahi ona, Leo ilikuwa ni safari ya kurudi home baada ya kukamilisha kilichonileta huku, nimetoka sehemu niliyofikia (Donholm) fresh sihisi njaa nimepanga nifike Border ndio nipige msosi wa Nguvu (Supu chapoo ya kibongo) Supu za huku sizielewi Sasa sijafika hata mbali njaa ikaanza kuita saa hio Niko Mlolongo nikaona kutoka Mlolongo Hadi border ni parefu sana sitaweza vumilia njaa, nikasogea sogea hadi Athi River nimepitia tu Roundabout ya Athi river mbele kidogo nikaona Hotel nikachoma ndani

Nikapiga hesabu pale kabla ya ku order nikaona nipige tu msosi kabisa niachane na Chai, nikaitisha Ugali Matumbo na Greens, nikaletewa bill ni Ksh 350/= Nikatoa Soo 4 nikampatia yule muhudumu akaenda kwa Cashier akaniletea balance yangu Ksh 50 mm sijaipokea nikamuambia utakunywa soda hiyo, yule mhudumu kwani alinijibu nilimuona tu karudi kwa Cashier tena, alivyorudi kwangu sasa

Akanambia "I have nothing to do with 50 bob, I can see ww ndio unafaa kukunywa soda na si mimi" kumbuka Ile shilingi 50 niliyompatia aliicha pale kwenye meza akatoa mia tano (Ksh 500) "utakunywa soda na food imejisort kwa hiyo pesa balance utatumia kupanda matatu urudi mahali umetoka" halafu akasepa, Asee nilibaki nimeduwaa

Yani Pesa yangu mwenyewe hata kama ni ndogo ndio inanifedhehesha kiasi hiki? kusema ukweli na Mimi sijajivunga nikabeba Ile mia tano, ila na mm nilitaka kumuoneshea dharau yule mkikuyu sijui ni mkikuyu yule, ikabidi tu niwe mpole kwasababu nipo Nchi ya watu ila ingekuwa Bongo haki ya nani nisingekuwa mpole hivyo

Uzuri hajajua kama mm ni Mbongo maana angejua pengine ningehisi kubaguliwa, kwasababu Wakati natoka pale hotelini nikamsikia anamuongelesha mwenzake "Hawa watu wa Mombasa 'Chuani' kwao wanaona ni kama Thao" asee Dada aliniamulia yule sijui alitumwa, sijawahi kukutana na dharau kama hii maisha mwangu


Tafuteni Pesa wadau tena sio Pesa tu, Tafuta Utajiri kwa namna yoyote ile ili ukitoa tip utoe inayoeleweka, Mimi hiyo dharau imenipata katika pilikapilika za kutafuta Utajiri so imeniongezea kasi/speed zaidi, Kasi ilikuwa inasoma 3G baada ya hilo tukio imepanda hadi 4GView attachment 2272915
Hahaha nimecheka sana. Pole sana kwa masaibu yaliyokukumba. Sio Wakenya wote wana tabia mbaya hivyo. Huyo amekosa adabu lakini tusamehe tu. Karibu Kenya siku nyingine.
 
Mimi nilifika hapo Kitengela kwenye kibanda cha Gidheri ilikuwa majira ya saa mbili usiku vijana wawili wakatoka baruti nikashangaa sana

Yule Mhudumu akanishukuru sana akaniambia walikuwa ni Wakora wanataka kupora na wamekufikiria kuwa wewe ni Flying Squad.

Nikamwambia yule Mama kuwa mimi ni Dereva wa Roli kutoka Arusha akasema basi wamekufananisha nikajisemea moyoni Alhamdulilaah..
Very dangerous
 
Ukitajirika urudi pale kula na umwachie angalau 50,000 hii ni sawa 1,000,000 ya bongo.
Yeye amekupa 500=10,000 ya bongo.
 
2 hrs behind Tz time

Nazingua nini?
Nahisi unadhani masihara ninaposema niunganishe na box.....Niko more than serious nataka nikache hii kaz inayonidumaza kiuchumi mwenzio....nataka nivae ukiume nipambanie michongo yoyote yaan.Hata wewe unaweza niajiri tu ilimradi Ilo donge nono lipo kweli....naitaka sana pesa ya jasho langu aisee 🤜
 
Back
Top Bottom