Hii Dunia Ina vituko sana,Kuna watu wanasema Real Madrid anamtoa Arsenal

Hii Dunia Ina vituko sana,Kuna watu wanasema Real Madrid anamtoa Arsenal

Nsikuchoshe na Usinchoshe, Tusichoshane!


Yaani Kuna Vichaa wanywa komoni kutoka pale Bitaraguru na Wanywa Ulanzi kutoka pale Kilolo wanapanua na kukenua Kwa bashasha wakiamini kabisa ya kwamba Arsenal (The Gunners )anakwenda kutolewa na timu ya Wazee Vijana (Real Madrid).

Huwa kila siku mkipewa ushauri wa Bure na Bujibuji Simba Nyamaume muachane na hizo pombe za kienyeji nyie mnajifanya wajuaji,hayo ndiyo madhara yake!,Ni mtu mwehu na asiyekuwa na akili timamu tu anayedhani Arsenal atatolewa na Real Madrid!


Arsenal kufungwa atafungwa hilo nakubali lakini si kutolewa,Hakuna timu ya Hispania inayo msumbua (ga) Arsenal tofauti na Barcelona siyo hao wazee waliochoka!

MATOKEO

REAL MADRID 3 - 1 ARSENAL
UMUGHAKA
 
Nikiangalia beki ni wale kina rudiger, alaba and Co halafu pale kati palivyo vibaya. Naiona Madrid ikikusanya virago bila kupepesa macho, mchezaji ni mmoja tu Federico Valverde.
 
Brother, kwanza heshima yako.....lakini acha kuukosea heshima mpira wa miguu, najua ni mahaba yako....lakini mpira wa miguu una matokeo ya kikatili sana, ndio maana ndio mchezo pendwa duniani kote, ungekuwa wa kutabirika basi usingekuwa na mvuto!
 
Nafikiri Madrid mechi ya kesho kiungo chake kitakuwa kimeimarika zaidi, baada ya kurejea Cebalos.
 
Arsenal kufungwa atafungwa hilo nakubali lakini si kutolewa,Hakuna timu ya Hispania inayo msumbua (ga) Arsenal tofauti na Barcelona siyo hao wazee waliochoka
Kama real madrid watacheza kama walivyocheza gem ya kwanza tutawafunga tena.
 
AC Milan ile ya akina Prince Boateng mechi ya first leg AC Milan alishinda mbili kwa sifuri mechi ya marudiano pale Bernabeu AC Milan alikufa nne kwa sifuri endeleeni tu kuongea ujinga
Na aliteseka hasa sitasahau iyo game walidhalilishwa mamaee
 
Zikipita dk 20 hatujagungwa holi hata moja basi game imeisha ila tukipigwa goli la mapema kazi ipo
VAR na refee kama kawaida Real Madrid watapewa mbeleko.

Na Madrid watatafuta magoli ya mapema sana, Arsenal wakiteleza kidogo penati na Nyekundu zawadii kwa Real Madrid.
 
Mimi naomba nipigwe ban kwa wiki moja ikitokea Madiridi kuqualify to the semis
 
Jana Dortmund na Aston Villa waliweza kupata magoli matatu matatu, hii iwastue Arsenal lolote linawezekana.
 
Back
Top Bottom