Dunia Iko hivyo na itaendelea kuwa hivyo Kuna watu wao wanajiona wamezaliwa Ili kufanya domination Kwa wengine, hii imeambukiza Dunia nzima. Kuna watu au jamii hujikuta wao ndio noble race au master race kuliko wengine wote duniani, hii mentality ndiyo imeharibu hii dunia, seek for domination and supremacy. Na kuambukiza hadi katika local regions huku afrika, gawa uwatawale.
Kule Asia wale wahan wanajikuta wao ni watu bora sana kushinda wengine, Bhutan (India) wale wahindi weupe wa kaskazini hujikuta ni bora kuliko wenzao wa kusini. Japan nayo walijiona wao ni bora kuliko majiran zao wote, ujerumani nayo Hitler alitengeneza mentality yakuwa wao ni master race hivyo dunia nzima na watu wake ni takataka, Kuna wazungu hasa wale blonde hair, blue eye, hujiona wao ndio race yenye hadhi ya juu kuliko zote duniani hujiona kama royal bloodline vile, ulaya wafalme wengi na ndugu zao wapo hivyo ni blonde hair, blue eye basi ndo hujiona bora kuliko yeyote, all reasons behind ni supremacy and domination.
Pawns ndo sisi, bahati mbaya au nzuri jamii za kiafrika nyingi hazina hii mentality ya kutoka twende tukatawale na kudominate race nyingine, wewe angalia popote alipo mzungu lazima akudominate direct au indirect Kwa kukutengenezea mazingira ya kukufanya wewe umtegemee yeye bila hata kujitambua au kujifahamu kama ni kamchezo aidha umtegemee Kwa mawazo, njia, ushauri, fedha, mali nk.
Ili uishi kwa raha lazima higher domination iwepo na ndo mvurugano unapoanza maana lazima uue, upore, uibe, uchonganishe nk hii ndo mentality ya jamii za wenzetu kwa kutumia upumbavu wetu Africans tulionao.