Mkuu
knows pole sana Kaka kwa hiyo hali unayooitia na Ushauri wa
Mshana Jr umekuwa ni bora sana kukusaidia kukupunguzia hayo maumivu unayopitia.
Mkuu asikwambie mtu hakuna kitu kinachoumiza kama usaliti hasa pale wewe unakuwa ni muaminifu halafu mtu wako anakusaliti. Nina same case na wewe lakini Mimi sio Mpenzi ni Mama mzazi, ubaya wa kila namna alinifanyia ninaposema Ubaya elewa ubaya wa Kiafrica Matusi, masimango, kufukuzwa wakati ninaumwa, ushirikina nk , ameniomba msamaha na nimemsamehe kiroho safi lakini wakati mwingine huwa najikuta nikikumbuka yale mambo aliyonifanyia huwa nakosa kabisa furaha, najisikia hasira, najisikia kulia, najisikia mnyonge na kila hali mbaya. Huwa inaumiza sana japo nimeshamsamehe lakini kumbukumbu imekuwa ni ngumu kufutika. Nimefanya njia zote za kuomba ushauri, kusoma vitabu na kujichanganya sana na watu nakaa sawa lakini nikikumbuka huwa narudi kuvunjika sana moyo.
Mkuu huo ni mtihani na imeahakuwa kama kidonda ishi nacho tu. Ngumu kuondokana na hiyo hali na ukiangalia hukuwahi kumsaliti yaani wewe upo clean. Ishi tu Mshikaji wangu ukiona hizo memories zinakujia kwa wakati huo jaribu kufanya mambo mengine yanayo ku keep busy na kukufurahisha ili kutokuendeleza hizo memories kukuathiri.
Hakuna mtu asiyekuwa na changamoto Mkuu na huo ndio mtihani wako.
La mwisho tafuta siku nzuri ya mapumziko utoke nje ya mazingira mliyoyazoea na huyo MpenZi wako mkafurahie maisha na ujaribu kumuelezea vile ulivyoumia na lile tukio alilokupiga nalo. Lakini ukiwa kama Mwanamume umesamehe. Jitahidi uwe unapata muda wa kuzingumzia maisha yenu kwa upana kila mara hata mara moja au mbili kwa mwezi. Hiyo itasaidia kuboresha afya ya mahusiano yenu.