Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Hukumu hii ni ya kutotambulika kwa Baraza la Wadhamini la klabu hiyo kufuatia hukumu iliyotolewa Agosti 2, 2023 na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hukumu inatokana na kesi ya msingi iliyofunguliwa Agosti 4,2022 na walalamikaji Juma Ally na Geoffrey Mwaipopo, wakitaka kutotambulika kwa Baraza la wadhamini la Yanga lililowekwa madarakani kwa katiba ya mwaka 2010, kukosa sifa kisheria.
Aidha, walalamikaji pia walitaka miamala yote ya fedha iliyoidhinishwa na baraza hilo, kutotambulika kisheria kwa kuwa ni batili.
Hukumu hiyo, imeitaka bodi iliyokuwa madarakani kwa katiba ya mwaka 1968 iliyofanyiwa mabadiliko mwaka 2011, kurudi madarakani kuongoza klabu ya Yanga.
Jumapili, Juni 27, 2021, aliekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla alitangaza Baraza jipya la Wadhamini la klabu hiyo mbele ya wanachama kwenye Mkutano Mkuu wa klabu. Aliowataja Walikuwa ni George Mkuchika, Geofrey Mwambe, Abass Tarimba, Mama Fatma Karume na Mwigulu Nchemba.
Mwigulu Nchemba, Mwambe na Tarimba ndio wajumbe wapya wa Baraza hilo huku wenyeji wakiwa Mkuchika na Mama Karume.
Pia, soma: LIVE - Simon Patrick: Yanga itaenda mahakamani kuweka zuio la kukabidhi timu kwa wazee walioishtaki