Hii hapa Television ya kumiliki kulingana na kipato chako

Tafuta Evvoli OG (kama bado zipo) utanishukuru baadaye. Mi ninayo mwaka wa saba huu bonge la tv. Nimehamahama nayo mara kibao inajipigiza ila ukifunga na kuwasha iko fresh tu
Yes nami nazikubali zipo vzr ila sijajua kwa upande wa picha quality yake ipo vzr mkuu like hisense au au ndo za kucompare na solar na rising tu
 
Hivi Hitachi zilikufa mkuu?
 
Vp mkuu hizi za evvol zipoje maana nilitaka nichukue nilienda dukani kwao nikaambiwa zimeisha
Ni stock za mda kwaiyo si rahic uzikute dukan,wengi wanaangalia soko wateja wanapenda brand kama izo TCL Hisense Samsung nk

Evvoli ni nzuri ila chukua ya 1080p na kuendelea,Mimi ninayo ya 1080i ila natakaka ni upgrade ninunue 4k
 
Ni stock za mda kwaiyo si rahic uzikute dukan,wengi wanaangalia soko wateja wanapenda brand kama izo TCL Hisense Samsung nk

Evvoli ni nzuri ila chukua ya 1080p na kuendelea,Mimi ninayo ya 1080i ila natakaka ni upgrade ninunue 4k
Poa mkuu nitachek mzigo wao mpya watakao leta utakuaje
 
Vip kuhusu tv za Itel?
 
Kwa mliowahi kutumia HISENSE au TCL zikoje hizi quality yake ya sound na quality ya picha? Nataka nichukue 55"
 
Koffi Annan hapa nimeona TCL C655 model ni mashine, ni kujichapa hiyo inchi 65 maisha yawe mepesi. Maduka ya Dar naona wanauza Tshs. 1.9m vipi wako sawa?
Iangalie zaidi hapa
 
Ni Kwa nn dstv chanel zao ni ukungu? Jana nikasema nipite maduka wanayouza tv nikakuta TCL 4k
wameweka mpira , super sport,nikamwambia aweke tbc akaweka ,ikawa inaonyesha wingu kama TV yangu ya maskani evvoli 43" smart ,akaweka tena wasafi ndio kabisa ni mawingu .ila tv ni 4k

Sasa najiuliza inakuwaje tv ni 4k ila ukiweka channel za tv ni mawingu?
 
Ni kwa sababu hizo stations unazoangalia hazirushi matangazo kwa teknolojia ya 4K.

Ili uone picha ya 4K, lazima video unayotazama iwe ilisafirishwa (rendered) kwa 4K resolution na pia kifaa unachotumia kupitishia hiyo video kiwe cha 4K pia.

Sasa dekoda za dstv na hizo za azam nk sio za 4K, bali za HD tu ile ya 1080p, hapo huwezi ona picha ya 4K. Na hata ungenunua dekoda yenye uwezo wa 4K bado picha za TBC na Wasafi nk zingekua mbaya maana kituoni kwao hawarushi matangazo ya 4K.

Nafikiri nimeeleweka mkuu. Channel za DSTV za HD ukiweka kwenye hiyo tv utaona ni angavu sana, mfano, Ch. 223, 132 nk
 
Vicenza Nahisi umeelewa vizuri kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…