Hii imekaaje kudharau watumiaji wa simu za Tecno na Itel ilihali wote mnakuwa na access ya vitu vinavyofanana

Hii imekaaje kudharau watumiaji wa simu za Tecno na Itel ilihali wote mnakuwa na access ya vitu vinavyofanana

Haya mambo ni hulka. Kuna watu, wengi tu wana uwezo wa kumiliki simu kali lakini wanatumia simu za kawaida sana. Na mwingine yuko radhi amiliki simu yenye thamani ya mishahara yake mitatu.

Binafsi hapa namiliki Infinix! Miaka miwili sasa. Naweza kufanya kazi za ofisi, kupiga na kupokea simu, kutuma sms na ina whatsapp. Na kwa vile maisha yangu napeleka nnavyotaka mwenyewe na serikali yangu. Hainisumbui kuitoa popote pale.

Nikienda kwa wakala au benki hawaniulizi unatumia simu gani? Ilimradi salio liwepo.
Umemaliza. Mtu anamiliki simu ya gharama ukimuuliza ina impact gani kwenye maisha yake anabaki kusema Tecno inapata joto.
 
Mimi natumia samsung sasa kuna kipindi simu yangu ilianguka hadi chini wakati naendesha boda yangu na ikapasuka kioo na mimi sikuwa vizuri mfukoni ikabidi niiweke pending nichukue tecno ya wife kwakuwa naendesha kwa kutumia bolt ili niiendelee kuwa online wakati najipanga kuirekebisha simu yangu.Sasa basi naweza nikawasha data ya bolt ili nipate request nashangaa mbona nakaa sana sipati request kumbe simu inajizima data yenyewe nakuwa offline pasipo kujua so ikabidi nimrudishie wife simu yake nkarekebisha ya kwangu hadi sasa sijapata hiyo changamoto kama niliyopata toka tecno
 
Umasikini kitu kibaya ndio maana hata Bible imekisema unaweza ukawa na kitu cha ajabu Ila unataka kukifanya kiwe Bora
Na pia umasikini huambatana na husuda ,roho mbaya,kikubwa ni kuishi kulingana na level ya uchumi
 
Hii ni verified ID. Ifuatilie vizuri
Mkuu kuwa verified maana yake kuwa na maisha bora?Mbona kuna mdau wangu humu ni verified member lakini ni choka mbaya.

Kuwa verified ni takwa la muhusika wala hakuna vigezo viiingi.
 
Wanaume wa Dar unapata 4 ya 28 unajisifu?
Umeunga unga elimu mpaka kinyaa
Sikia ndugu, soma std 7 faulu, soma f 1 hadi 4 faulu soma f 5 na 6 faulu nenda University. Kuunga unga ina maana shule wewe umelazimisha tu umetumia ujanja ujanja[emoji23][emoji23]
Kwel siku hizi elimu ya bongo imechange.
IV ya 28 unaenda diploma[emoji53][emoji53]
 
Kwa tafsiri hiyo ukiwa unamiliki bmw unakuwa na kibali cha kumdharau anayemiliki Passo kuna wakati tujifunze kuappreciate vitu vya watu.

Kuna mataasisi yenye wataalamu yanasimamia standard ya hivi vitu ukiona bidhaa imeingia sokoni ni wazi kuwa imekidhi viwango vilivyowekwa.

Sasa wewe unayejifanya mjuaji na akili zako za darasa la saba b unakomaa kuwa Tecno sio simu ilihali hata basics za kutengeneza calculator huzijui.

ukitaka kujua binadamu upenda kizuri subiri kupata pesa.

siwezi kutumia takataka ambazo project zake zinasubiri kujifunza makosa au kukusanya mitaji ili kutengeneza kitu kizuri.

jifunze kujinyima ndio unaona hata vitu vizuri vina dumi
 
Tecno, itel na infinix ni simu ila za kiwango cha chini.

Lazima tukubaliane kwamba kwenye maisha kuna viwango ama levels, hizi zinatokana na vitu vingi mojawapo ni ubora.

Mfano, unaweza kupanda toyo la miguu 3 kutoka Dar kwenda Dodoma, utafika tu sawa na Shabiby ingawa mtatofautiana muda wa kufika. Barabara mnapita moja ile ile lakini tofauti ya yoto ama guta na Shabiby iko wazi.

Wewe unaweza kua na paso mwingine ana range rover sports mnaenda Arusha kutokea Dar, yote ni magari na mtafika wote Arusha kwa nyakati tofauti lakini kuna vitu kama speed, comfortability, security, safety nk ndio vitatofautisha paso na range.

Kwenye simu iko hivyo hivyo. Tecno ni simu ila za viwango vya chini, choka mbaya. Vifaa vinavyotumika kutengeneza tecno ni vya ubora hafifu ama wa chini.

Tecno tunatumia tu kwa sababu ya umasikini ila tukiwa na hela tungetamani kutumia simu za maana kama Samsung, Iphone, Huawei, Vivo, Xiaomi, LG, Lenovo ama makampuni mengine ya maana.
Ukiwa unatumia Samsung unakuwa comfortable zaidi kulinganisha na Tecno? Naomba msaada wa kunidadavulia hili

Mtu anaweza kutumia Passo lakini akawa comfortable na akafika atakapo kwa wakati lakini wewe unayetumia benz kwa kutojiamini kwako unaanza kashfa kuwa Passo sio gari nini kinakupelekea kusema hivyo ilihali wewe unaenjoy maisha kwenye bmw
 
Hizi simu ni under quality kwa tafiti za nani? Na nani alikwambia hazitumiki zinapotoka? Narudia tena mnao diss hizi simu hamna hoja za msingi zaidi ya kashfa na dharau.

usiwe mbishi bila kujisomea.

unajua tecno,infinix na itel zinazalishwa wapi???na kuuzwa mataifa yapi??kwanini??

unajua kwanini zinauzwa bei ndogo kuliko simu sawa za kampuni kubwa??
 
Mkuu nunua iphone au Samsung Ili uwafurahishe watu,

Dunia haina usawa
Kuanzia mavazi,malazi, chakula,ndinga nzuri majumba mazuri

Vyote hivi hufanyika kulingana na walimwengu wanataka Nini .ukibisha utapata taabu Sana.

Bodi wangu alinunua Toyota Prado bila kupenda kisa tu walimwengu hawakuipenda Toyota Corolla yake[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

na ukiisikiliza nafsi yako,utagundua hata tecno ni anasa[emoji13][emoji13]
hapa ndio utajua msukumo kutoka nje una nafasi gani ktk maisha yako.
 
Kwel siku hizi elimu ya bongo imechange.
IV ya 28 unaenda diploma[emoji53][emoji53]
Kuna kigezo kingine huwa wanaweka kwa mfano ili mtu ajiunge diploma fulani basi awe na certificate ya eneo husika analotaka kusoma diploma ama awe na ufaulu wa credit 3 ( c tatu)form four.

Kwahiyo unakuta mtu ana four ya points 28 ila ana C tatu kwahiyo anakuwa qualified.
 
Back
Top Bottom