kimbomba25
JF-Expert Member
- Jan 27, 2017
- 1,160
- 2,117
Shule zinazofundisha mitaala ya nje zipunguze bei twende huko.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukisoma kipengele namba 9, utaliona lipo.Hakuna somo la sayansi shule za msingi?????!!! Hili ni kosa kubwa saaaana!!!
Hicho ndio kitakachofuata,wanaanza kuwachorea watoto picha za computer ubaoniCurriculum inaweza kuwa ni nzuri sana Kwa kuangalia, ila uzuri wake utatokana na utelezaji wake Kwa ufanisi...!!
Je, mazingira wezeshi na vifaa vya kufundishia vipo? ....Au ndio tunarudi kule kule TU darasa Lina watoto 45 wanaosoma computer science ila shule Ina computer mbili TU na tena moja ni ya mwalimu kuu, muda wote imefungiwa ofisini.🙂↔️
Somo la dini limewekwa ili liwasaidie nini wanafunzi?
Mtoto anasoma dini ili iweje?
Hapa Serikali imejichanganya. Maana nchi yetu inatambulika kama ni secular state!! Sasa mambo ya masomo ya dini kwenye mitaala yanafuata nini, tena kwenye hii karne ya 21?Elimu ya DINI ingetoka kwenye list maana inaongoza kwa kuchezea bongo zetu kwa kuamini vitu vinapatikana kwa sababu ya kumtumaini MUNGU ambae hatuna uhakika nae kama ana huruma na sisi.ASANTE
Atakuwa aliyeandaa hii ana akili kama za LIKUD ...Yaani wenyewe hawafikiri nje ya box.,Wanajua mtoto kazaliwa kigoma so lazima asome fani ya uvuvi,yaanj hawafikiri kuna maisha nje ya kigoma,kuna maisha nje ya Tanzania,hawaoni maisha ya sasa tunakimbizana na globalisation,Dah Tanzania bado tuna safari sanaCurriculum inaweza kuwa ni nzuri sana Kwa kuangalia, ila uzuri wake utatokana na utelezaji wake Kwa ufanisi...!!
Je, mazingira wezeshi na vifaa vya kufundishia vipo? ....Au ndio tunarudi kule kule TU darasa Lina watoto 45 wanaosoma computer science ila shule Ina computer mbili TU na tena moja ni ya mwalimu kuu, muda wote imefungiwa ofisini.🙂↔️
Mambo yanaanzaga taratibu kaka,mwishowe utasikia yaliyomo yamo...Hapa Serikali imejichanganya. Maana nchi yetu inatambulika kama ni secular state!! Sasa mambo ya masomo ya dini kwenye mitaala yanafuata nini, tena kwenye hii karne ya 21?
Elimu ya dini haikutakiwa kuingizwa kwenye mitaala. Na badala yake utaratibu ungetumika kama ule wa zamani. Kila mwanafunzi anakuwa huru kushiriki kwenye imani yake.
Hili swali pia nimejiuliza mkuuSomo la dini limewekwa ili liwasaidie nini wanafunzi?
Mtoto anasoma dini ili iweje?
Siyo Upuuzi mkuu.Acha upuuzi wewe na mwenzako Mmoja aliyetoa comment Kama hii hapo juu
Atakuwa aliyeandaa hii ana akili kama za LIKUD ...Yaani wenyewe hawafikiri nje ya box.,Wanajua mtoto kazaliwa kigoma so lazima asome fani ya uvuvi,yaanj hawafikiri kuna maisha nje ya kigoma,kuna maisha nje ya Tanzania,hawaoni maisha ya sasa tunakimbizana na globalisation,Dah Tanzania bado tuna safari sana
Nchi zilizoendelea zina community college hata ambaye ajafaulu anaenda huko kujitoa kwa fani anayoitaka bado mfumo hautoi suluhisho la moja kwa moja kwa watuMABADILIKO MAPYA YA MITAALA YA ELIMU SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO 2025
MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU:
1.Mtihani wa darasa la Saba utafutwa.
2.Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize Kidato cha nne.
3.Kutakuwa Mtihani wa Upimaji wa Kitaifa wa darasa la sita (STANDARD SIX NATIONAL ASSESSMENT).
4.Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza Kidato cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza.
5.Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa kama somo kwa Shule za Kiswahili Medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa Kama somo kwa Shule za English Medium.
6.Elimu ya Msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6 tofauti na ya sasa miaka 7.
8.Elimu ya Awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5.
9.Masomo ya Elimu ya Msingi yatakuwa ni KKK, Jiografia,kiswahili, Sanaa na Michezo, Hisabati,Sayansi, historia ya TANZANIA na Maadili,Dini na kiingereza na Stadi za Kazi itachomekwa.
10.Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza.
11.Shule zenye uwezo zitafundisha angalau somo moja la lugha za kigeni kama Kichina au Kifaransa.
12.Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na Amali (Ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na uwezo,matakwa na malengo yake ya baadaye.
13.Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani zifuatazo:-
Kilimo na Ufugaji.
Umakenika.
Biashara na Ujasiriamali.
Sanaa na Ubunifu.
Elimu ya Michezo.
Ufugaji wa Nyuki.
Uchimbaji wa Madini.
Urembo.
14.Mwanafunzi wa Mkondo wa Amali atatakiwa kuchukua Masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.
15.Masomo ya jumla ya wanafunzi wa Amali ni:-
Hisabati.
Elimu ya Biashara.
Kiingereza.
Historia ya Tanzania na Maadili.
16.Wahitimu wa Amali watapata vyeti viwili yaani:-
Cheti cha ujumla cha Elimu ya Sekondari (NECTA) na Cheti cha Amali ( NACTIVET).
17.Kila shule itakuwa na Wakala wa VETA ili kusimamia masuala ya Ufundi.
18.Kila shule haitakuwa na Mikondo zaidi ya miwili ya Ufundi,hii ni kwa ajili ya Ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.
19.Kutaanzishwa somo jipya la Mawasiliano ya Kitaaluma (ACADEMIC COMMUNICATION) katika A-level na Ualimu.
20.CODING itafundishwa Shule za Msingi.
21.INFORMATION and COMPUTER STUDIES (ICS) itabadilishwa na kuitwa COMPUTER SCIENCE.Somo limesukwa upya.
22.CIVICS itaunganishwa na Historia ya TANZANIA na Maadili kwa O-level.
23.O-level Masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa.
24.Katika O-level Masomo ya Biology na Geography yatakuwa Masomo ya kuchagua pia kwa sababu Maudhui yake yamekuwa kwenye Masomo ya Jiografia na Sayansi ya Shule ya Msingi kwa mfano Afya ya Jamii,Afya ya Uzazi, Magonjwa ambukizi nk.
25.Civics, Maarifa ya Jamii,Uraia na Maadili yamefutwa, Maudhui yake yameingia katika somo la Historia ya TANZANIA na Maadili.
26.General Studies (GS) katika A-level itafutwa na Maudhui yake yatawekwa katika Somo la Historia ya TANZANIA na Maadili na Mawasiliano ya Kitaaluma.
27.Kufuta baadhi ya Masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudiarudia kwa Maudhui.
28.Michepuo katika Elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9).
Michepuo iliyoongezeka ni:-
Sanaa.
Lugha.
Muziki.
Michezo.
Tehama.
29.Masomo ya O-level yatakuwa:-
Biology.
Physics.
Chemistry.
History.
Geography.
Historia ya TANZANIA na Maadili.
Hisabati.
Kiswahili.
English.
Elimu ya Biashara.
Utunzaji wa _Taarifa za Fedha.
Computer Science.
Bible Knowledge.
Elimu ya Dini ya kiislamu etc.
30.Astashahada ya Ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (DIPLOMA) ya Elimu ya Awali, Ualimu wa Msingi na Ualimu wa Elimu Maalumu.
Watakaosoma Stashahada watakuwa waliomaliza Kidato cha Sita na itasomwa kwa miaka miwili.
31.Walimu wa Sekondari wote watakuwa na Shahada (DEGREE). kwa sababu nchi nyingi zinaenda na mwelekeo huu.
32.Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (DIPLOMA) ya Ualimu wa Sekondari vitatumika kutoa continuous Professional Development.
Wala haijulikani si unaona hata hakuna TV ya Kilimo, somo la Kilimo sio ishu, ila masomo ya dini yamepenyaHivi kilimo bado ni UTI WA MGONGO?
Tutapeleka Nairobi watoto wetu,mambo ya kuwang'ang'aniza watoto wetu wasome kilimo cha nyanya kisa wanakaa Ilula hatutaweza,...Unajuaje kama Sio Likud mwenyewe ndio kaandaa hiyo programme?
🤣🤣🤣🤣🤣
Anyways ?
A. Is Likud a prophet or
B. Likud yupo kwenye system anawaambia watu wawatoe watoto Wao shule za EM Kwa sababu anajua what is going on behind the scene?
Only God knows.
But what?
Listen to Likud so that your days shall be many and Merry.
Thanks me later 🙏🙏🙏🙏🙏