Hii imekaaje kuhusu huu mtaala mpya wadau

Hii imekaaje kuhusu huu mtaala mpya wadau

Hapo kwenye lugha ya kiswahili kutumika sijaelewa naomba kufahamishwa? Ina maana Yale masomo tuliyokuwa tunasoma sekondari Kwa lugha ya kingereza sasa yatafundishwa Kwa kiswahili mpa advance ama?
 
Kuhusu namba 5
Hivi kwanini tunang'ang'ania kufundisha watoto elimu ya primary kwa kiswahili.
Wakati kijana akifika sekondari au chuoni au kwenye udahili au ofisini katika kuandaa ripoti lugha inayotumika ni kingereza..!
Hivi hawa wapuuzi hawalioni hili gapu...?
Kwanini tusiweke msingi wa hii lugha kwa watoto toka primary..?
Wanataka watoto wa maskini wabakie kuwa makuli,vibarua na watoto wao ndio wa hold nafasi kubwa serikalini.
 
Mtoto anaenda kusomea course ya mtume mwamposa.. hayo mengine pambaneni nayo tu
Course yenye uhakika wa Mabunda hio hapo nakuunga mkono🤣,,,nimepita kijiweni sijakusoma kabisa. Nicheki kwa line kuna jambo tubonge.
 
Dini iondolewe maana inachangia kutuongozea mazombie ya imani na target ya elimu tupate vichwa vitenda kazi
 
Number 9. Dini wangeitoa kwenye mitaala ya elimu za shule, likabaki swala la wazazi na maamuzi yao kwa mtoto wao.

Dini itatuvuruga sana mashuleni.
 
CCM wajinga sana, wanavuruga Elimu Kila kukicha.

Basi hapo wanajipiga vifuani,, ati wamefikiria sana kuhusu Elimu Yetu.
 
Hapo kwenye lugha ya kiswahili kutumika sijaelewa naomba kufahamishwa? Ina maana Yale masomo tuliyokuwa tunasoma sekondari Kwa lugha ya kingereza sasa yatafundishwa Kwa kiswahili mpa advance ama?
Sasa hivi tu Wakenya na WaUganda kimataifa wanatupiga bao kwasababu ya lugha ya Kiingereza na bado tumeondoa kabisa kama lugha yakufundishia kwa uchache wa vocabulary words za lugha ya kiswahili masomo kama biology, chemistry etc kufundisha kwa lugha ya kiswahili ndio wataongeza ugumu zaidi unless maneno yasibadilike japo nayo ni mtihani bado!

Kiswahili tunachotumia mtaani kinatosha kabisa, angalao wangetumia Kiingereza kama lugha ya kufundishia kuanzia huku chini, wenzetu wanaotumia lugha za kigeni kimataifa wanashine, tusijifananishe na miinchi kama China huku ambao wao walianza kitambo na walikuwa na misingi dhabiti ya kupeleka wanafunzi Marekani na ulaya wakaiba technology na kuleta kwao!
 
Upuuzi gani ? Unamfundisha mtu masomo ya dini ili iweje ? Kwani makanisa na misikiti wameshindwa kutoa hizo Elimu ?
Hatukuzi taifa la wapagani litakalokuwa limejaa maatheists uchwara, watoto ni lazima wafundishwe kuhusu dini maana kila mwenye akili timamu anajua umuhimu WA dini kwenye jamii yetu, Kwa hiyo Kwa vile Kuna miskiti na makanisa basi somo la dini halitakiwi kuwa na nafasi kwenye mitahala ya elimu? Akili zenu Huwa ni ndogo sana japo mnajionaga ni binadamu wenye akili
 
Siyo Upuuzi mkuu.
Sehemu za kujifunza mambo ya Imani/Dini inajulikana ni makanisani na misikitini.
Hiyo tu ilitosha na siyo kuyapeleka shuleni.
Hauko sahihi hata kidogo...!!

Kwa somo/kipindi Cha dini kinachukua muda Gani? Kikifundishwa mara Moja Kwa wiki Kuna shida?

Au labda uniambie Kuna madhara Gani na somo la dini likiwepo kwenye mtahala?
 
Sasa hivi tu Wakenya na WaUganda kimataifa wanatupiga bao kwasababu ya lugha ya Kiingereza na bado tumeondoa kabisa kama lugha yakufundishia kwa uchache wa vocabulary words za lugha ya kiswahili masomo kama biology, chemistry etc kufundisha kwa lugha ya kiswahili ndio wataongeza ugumu zaidi unless maneno yasibadilike japo nayo ni mtihani bado!
Na hii imefanywa kwenye shule za walala hoi siyo shule wanazosoma watoto wao
 
Ukisoma comments za WaTz humu ndiyo utaelewa ni rahisi sana kuwatawala WaTz, ni rahisi sana wazungu kurudi na kuitawala tena Tz...
Sijui WaTz mlimkosea nini Mungu, mbona mambo mengine ni rahisi kuyaelewa na yapo ndani ya uwezo wenu lakini hamtaki kutumia akili..?
Hamtaki kusoma... Hamtaki kufanya kazi... Hamtaki kujifunza mabadiriko mbalimbali ya kijamii sayansi na uchumi... Hamtaki kubadirika... Hamtaki kukua na hamtaki kuzeeka...
Taifa lina watu duni

Nimesahau nilikuwa nataka niseme nini mtanikumbusha baadae ngoja nilale mie nitalijenga taifa kitandan kwenye nyumba ya urithi...
 
Nilimsikia Afisa mmoja wa watengeneza mitaala akisema masomo ya dini yamewekwa ili yawasaidie kujiajili kama alivyo Gwajima, Mwamposa, Kakobe na wengine wanaofanana na hao
Hapo sawa. Kwa hapo nimeelewa.
 
Back
Top Bottom