Hii imekaaje kuhusu huu mtaala mpya wadau

Kati ya watu ambao walitani situ moja tuondokane na ile mitaala yenye mafungamano na elimu ya kikoloni (Colonial Education), basi na mimi nimo!
Na kwa hiyo katika hili, kwa kweli naipongeza sana serikali kwa kufanya mabadiliko ya mitaala ya elimu ili iendane na dunia ya sasa, lakini pia mahitaji ya nchi na watu wake.

NB: Sasa hivi mashambulizi yote yataelekezwa kwenye kuyavunja majeshi yetu mawili (Jeshi la polisi na magereza) ili na yenyewe yawe huru na ya kisasa! Kuliko ilivyo sasa ambapo hayana tofauti na majeshi ya Kikoloni tuliyo yasoma kwenye somo la Historia kule sekondari.


Lakini pia kuirejesha ile Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba ili nchi nayo isonge mbele kwenye nyanja za kiuchumi na kisiasa.
 
Hicho ndio kitakachofuata,wanaanza kuwachorea watoto picha za computer ubaoni
 
Somo la dini limewekwa ili liwasaidie nini wanafunzi?

Mtoto anasoma dini ili iweje?
Elimu ya DINI ingetoka kwenye list maana inaongoza kwa kuchezea bongo zetu kwa kuamini vitu vinapatikana kwa sababu ya kumtumaini MUNGU ambae hatuna uhakika nae kama ana huruma na sisi.ASANTE
Hapa Serikali imejichanganya. Maana nchi yetu inatambulika kama ni secular state!! Sasa mambo ya masomo ya dini kwenye mitaala yanafuata nini, tena kwenye hii karne ya 21?

Elimu ya dini haikutakiwa kuingizwa kwenye mitaala. Na badala yake utaratibu ungetumika kama ule wa zamani. Kila mwanafunzi anakuwa huru kushiriki kwenye imani yake.
 
Atakuwa aliyeandaa hii ana akili kama za LIKUD ...Yaani wenyewe hawafikiri nje ya box.,Wanajua mtoto kazaliwa kigoma so lazima asome fani ya uvuvi,yaanj hawafikiri kuna maisha nje ya kigoma,kuna maisha nje ya Tanzania,hawaoni maisha ya sasa tunakimbizana na globalisation,Dah Tanzania bado tuna safari sana
 
Mambo yanaanzaga taratibu kaka,mwishowe utasikia yaliyomo yamo...
 
Elimu ndio imekufa rasmi ,ni mtaala wa hovyo kuwahi kutoka,kwanza hatuwezi kuwa implemented kwa kuwa shule nyingi hazina hyo miundombinu
 

Unajuaje kama Sio Likud mwenyewe ndio kaandaa hiyo programme?

🀣🀣🀣🀣🀣

Anyways ?


A. Is Likud a prophet or

B. Likud yupo kwenye system anawaambia watu wawatoe watoto Wao shule za EM Kwa sababu anajua what is going on behind the scene?


Only God knows.
But what?

Listen to Likud so that your days shall be many and Merry.


Thanks me later πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
 
Nchi zilizoendelea zina community college hata ambaye ajafaulu anaenda huko kujitoa kwa fani anayoitaka bado mfumo hautoi suluhisho la moja kwa moja kwa watu
 
WaTz mmezoa kulalamika tu... Ndiyo maana hamfanikiwi ktk maisha... Jambo hata liwe zuri kiasi gani mmanataka kuleta upinzani hamtaki kujadili mambo ktk upekee wake...
Halafu muwe mnajitahidi kusoma mabadiriko mbalimbali ya kisekta yanapotokea...
 
Tutapeleka Nairobi watoto wetu,mambo ya kuwang'ang'aniza watoto wetu wasome kilimo cha nyanya kisa wanakaa Ilula hatutaweza,...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…