Hii imekaaje kuhusu huu mtaala mpya wadau

Kuhusu namba 5
Hivi kwanini tunang'ang'ania kufundisha watoto elimu ya primary kwa kiswahili.
Wakati kijana akifika sekondari au chuoni au kwenye udahili au ofisini katika kuandaa ripoti lugha inayotumika ni kingereza..!
Hivi hawa wapuuzi hawalioni hili gapu...?
Kwanini tusiweke msingi wa hii lugha kwa watoto toka primary..?

Halafu namba 29
Hiyo Historia na Historia ya Tz na maadili yaani sijaelewa.
 
Wala haijulikani si unaona hata hakuna TV ya Kilimo, somo la Kilimo sio ishu, ila masomo ya dini yamepenya
Noma sana, SUA sijui wanafundisha nini siku hizi?! Kilimo kimekua kama mafanikio, hata ukisoma sio lazima ufanikiwe, kwahiyo hata kilimo ni hivyo hivyo, unaweza usisome kilimo na ukalima na ukafanikiwa. Tunabahatisha bahatisha tu, kama mafanikio ya doto magari
 
No. 30 Kwahiyo Form four leavers hawataweza kusoma Astashahada ya Ualimu means ili mtu apate diploma lazima aende Advance🤔🤔,.
Au mie ndio sijaelewa
Ndio hivyo hakutakuwa na astashahada ya ualimu nk elimu ya sekondari kidato cha nne ni kazma kwa kila mwanafunz ila tu watakao faulu kidato cha 4 kwenda 6 hao ndoo watatupatia professionalisms wakutosha
 
Kwenye lugha hapo, nashauri Kiingereza pekee kitumike kwa shule zote. Kutuwekea Kiswahili kwa shule za Serikali halafu Binafsi waendelee na Kiingereza ni upigaji kwa dunia ya sasa.

Kiswahili kila mtu anazaliwa anafahamu, tupambane na Kiingereza tu.
 
📌 POINT #4 Nimekuwa naipigia chapuo sana bora wameiweka iwe lazima maana sasahivi GRADUATES wengi wamekimbilia kuwa MAWINGA😬😬😬 wakati kuna fursa kibao kwenye UFUNDI!!!

#Vijana nendeni VETA mkasome ufundi huko siku za usoni hakuna ujanjaujanja watu wenye ujuzi ndo watakuwa na hela sana.

KOZI AMBAZO HAZIMTUPI MTU;
1. UFUNDI WA UMEME WA MAGARI
2.UFUNDI UMEME WA MAJUMBANI NA VIWANDANI.
3.UFUNDI UASHI
4.UFUNDI SEREMALA
5.UFUNDI MAKENIKA
5.UFUNDI WA VIFAA VYA UMEME.
6.UFUNDI SIMU,COMPUTER NA VIFAA VYA MAWASILIANO.
7.UFUNDI BOMBA,N.K.

📌BILA KUSAHAU KUJUA KUENDESHA GARI NA KUWA NA LESENI NA PASSPORT💪💪💪SIO MCHONGO UNATOKEA NJE YA NCHI UNAMAVYETI YOTE PLUS UJUZI ILA HUNA PASSPORT HUU NAO NI UJINGA,VIJANA FANYENI MMILIKI PASSPORT,ACHENI KUZUBAAA!!!
 
Waziri wa Elimu ni Prof. Adolf Mkenda ambaye kwa sasa ana miaka takribani 62! Watoto wake hawasomi shule hizi saint kayumba! Na wala hana fikra za kumpeleka mtoto wake au mjukuu wake Muungano Shule ya Msingi au Uhuru Shule ya Msingi.
Miaka mitano mbeleni 2030 wanaifuta haya madudu na kuweka madudu mengi! Watoto wetu wanalishwa ujinga na watu ambao watoto wao hawalishiwi ujinga huu.
 
Seen
 
Mtoto wangu ataenda soma Great Britain.. elimu ya Tanzania kama homa za majira

 
WaTz mmezoa kulalamika tu... Ndiyo maana hamfanikiwi ktk maisha... Jambo hata liwe zuri kiasi gani mmanataka kuleta upinzani hamtaki kujadili mambo ktk upekee wake...
Halafu muwe mnajitahidi kusoma mabadiriko mbalimbali ya kisekta yanapotokea...
HAPANA SIO BURE MI NAHISI TUMEROGWA

Ila mambo ni mengi mno japo hoja zingine za ukosoaji zipo poa sana tu yani ila tuzingatie huu ni mwanzo na Wala si wageni tunajua serikali Huwa inalahumiwa Kwa utekelezaji m'bovu Kwa mipango mbalimbali. Ila hii nchi Kunasehemu tumevrugwa.

Watoto wanamaliza form4 wengine chuo ila hawana hili Wala lile,basi sio mbaya acha tuweka elimu ya ujuzi ngazi ya o level,povu kibao mara watoto wetu watafanywa kuwa saidia fundi tu mara hivi.

Sijui utekelezaji utakuwaje(kimazoe au kiumakini?) na uzuri Raia tushaanza kuonesha wasi wasi juu ya serikali hasa kwenye swala la utekelezaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…