Hii imekaaje watu wa mitazamo ya mbali, uwekeze Mil. 330,000,000 upate Mil. 27,500,000 kwa mwaka?

Bnafs naomba kujua umri wako for me kma ww n kijna ni uoga kuwekeza hiyo pesa kwenye real easte maybe ufanye 50/50 aslmia 50 uwekeze kwenye nyumba alafu 50 uwekeze kwenye biashra.
Kama n mzee kuanzia 50's uko sawa wekeza huko 100% biashra n ngumu yec but kma kijana lazima upambne na hizo changamoto zootee Ili uwe na financial stable ya mda mrefu [emoji120].
 
Hata biashara ni lazima upambane zisimane juu ya assets.

Huwezi kuanzisha biashara ya kumbi za starehe, bars, hotel juu ya majengo ya watu halafu ukategemea hiyo biashara itakuwa endelevu. Too risky
 
Gb490:sijajua umewaza nni ktk umri ila umri nikupambana na yanayokutokea.nikijana mpambanaji kwa kifupi.pia nashukuru kwa ushauri wako naufanyia kazi
 

Ushauri mzuri
 
Msininunukuu vibaya, biashara ya nyumba sio biashara kichaa lakini mimi sipendezwi nayo. Kama ulivyosema mtoa mada, unagharamia 30M kujenga nyumba moja ili upate kodi ya 2.5M kwa mwaka.

Na hapo itokee umemaliza tu kujenga akapatikana mteja, inaweza ukamaliza kujenga leo mteja ukapata baada ya miezi mitatu mpaka mwaka. Hilo la kwanza

La pili: ili uendelee kupangisha hiyo nyumba kwa kodi ya 2.5M kama ulivyoanza nayo utalazimika nyumba yako kuifanyia repair, uibadilishe muoneko izidi kuwa ya kisasa. Ukijenga leo 2023 baada ya miaka 10 that means 2033 hiyo nyumba bila repair huwezi pangisha kwa 2.5M itapungua.

La tatu; watu watasema nyumba inapanda thamani, ukweli ni kwamba nyumba haipandi thamani kinachopanda thamani ni kiwanja. Eneo husika nyumba ilipo ndo inapanda thamani ndo maana unaweza kukuta nyumba ya kawaida sana ya kizamani mno inauzwa 500M kariakoo lakini nyumba nyengine kali tu ya kisasa kabisa ikauzwa 200M huko Matipwili. Kwahiyo unapoamua kujenga nyumba ya biashara zingatia sana eneo, eneo zuri litakupa wateja wa kutosha pia itapandisha thamani ya kiwanja chako au ndo tuseme nyumba.

USHAURI WANGU: Kama unayo hiyo 330M, jenga nyumba chache zikizidi sana nyumba nne, pesa inayobaki tafuta uwekezaji mwengine uufanye. Jaribu kutupia jicho pia kwenye hatifungani za serikali. Hatifungani za miaka 25 itakupa return ya zaidi ya 42M kwa mwaka kwa miaka 25 mfululizo kama ukiwekeza 330M

HITIMISHO: Jenga nyumba chache kuwa selective sana kwenye eneo, jenga nyumba ya kibiashara iwe simple lakini itakayomshawishi mteja kutoa 2.5M kwa mwaka. Pesa inayobaki fanya uwekezaji mwengine.

Nyumba nne zitakugharimu 120M (@30M). 150M peleka kwenye hatifungani za serikali, bid ile ya miaka 25. Kiasi kitakachobaki (60M) fanya biashara, au kama hutaki hekaheka za biashara fanya uwekezaji mwengine. Ni vizuri sana kutawanya pesa zako. Usiweke mayai yote katika kapu moja.
 
Habarini wana jf,nimerudi napambana bado.ila nilipitia ushauri wenu nikaamua kufanya ujenzi.na kurudi Mara nyingine kupambana tena.View attachment 2477941
Pongezi sana ndugu kwa uthubutu na maamuzi uliyochukua. Pesa yako iko mahali salama hata kama itachukua muda kurudi.

Hizi biashara nyingine zinachangamoto unaweza kuingia kichwa kichwa ukalamba mchanga ndani ya mwaka mmoja.
 
Nikiweka milioni 3 kwenye hati fungani kwa miaka 19 napata sh ngapi mkuu
 
Ndugu yangu hongera sana kuwa na mawazo ya kesho ya kukutoa.
Mimi mwaka 2022 Nilichojifunza ni "Uchambuzi wa kitakwimu kutabiri yajayo".
Data acquisition is very important for future profit in any investment/business. Jifunze kutumia data kuwekeza pesa yako.
Mfano mwezi wa sita 2022 data zilionesha kuwa kutakuwa na upungufu wa nafaka nchini na nje ya
nchi, hivyo basi
Kwa kutumia data zile wenye macho, akili na mitaji waliwekeza sehemu sahihi kwa muda mfupi wametengeneza shilingi kwa shilingi. Yani wewe ungetengeneza milioni 700+ ugepapa au kufuata ushauri mzuri ungekuwa unaitafuta bilioni moja.
Jibu la utajiri ni DATA sio wazo la uwekezaji.
 
Pongezi sana ndugu kwa uthubutu na maamuzi uliyochukua. Pesa yako iko mahali salama hata kama itachukua muda kurudi.

Hizi biashara nyingine zinachangamoto unaweza kuingia kichwa kichwa ukalamba mchanga ndani ya mwaka mmoja.
Hizo nyumba ni kama zipo njombe au sio.Hongera ila jiandae kwa changamoto za wapangaji.
 
Ingia transport business Nunua Daladala kama za kutosha budgetbya 200m

Una option mbili
1.Nunua kutoka Japan
2.Nujua kwa mtu umtunzaji wa gari nzuri

Hiyo 27m inarudi kabla ya mwaka kwisha kama na wewe utasimamia vzr
 
Asilimia flani ya wanaojenga hivyo ni wanatakatisha fedha au wanafanya kama long term investment.
Unakuta mtu kapiga bilioni kwenye mishe. Sasa ile kuhofia kuziweka bank na kuchota attention anaamua kuisambaza kwenye real estate ila sio kwamba anajenga eti isomeshe watoto january.

So wewe kama unafanya ufanye kwa malengo na uwe na pesa mara mbili ya hiyo ya kukusukuma kwenye mambo mengine ila huko kwenye kodi fanya kama umechimbia
 
Binafsi mm nko km ww. Siamini ktk uwekezaji wa nyumba. Nakumbuka mwaka juzi nilinunua Mpunga gunia 100 kwa gharama ya 5M. Baada ya miezi 6 nikauza nikapata 8M. Faida nilipata 3M. So binafsi siwez kuwekeza kwny nyumba kwa huu utamu nilioupata. Nunua Mpunga hutojuta
 
Hivi nyumba za kupanga na fremu za biashara ni zipi zina lipa haswa ukipata location nzuri
 
Enkulu:habar ndg,unacho kisema hapa uko sawa kabisa.hadi sasa nimefanya ila ktk akili yangu nimesema haipo ktk hesabu zangu ila kwa walio toka ktk kiuno.maana siku moja niliwatoa wakasafishe macho,nikakaa pembeni najifanya nachezea simu nika waangalia madogooo...likaja wazo hivi nikikato moto hawa madogo wamekwisha na wao.ndo nikaona nifanye hivyo ndg.ila nimefanya kwa ajiri ya madogo na sikwa hesabu ninazo waza hadi sasa. Ndo maana nikasema narudi kwenye mapambano tena baada yakumalizia hii inshu.nitabaki na mtaji kidogo nikakaze mgongo tena.
 
Pongezi sana ndugu kwa uthubutu na maamuzi uliyochukua. Pesa yako iko mahali salama hata kama itachukua muda kurudi.

Hizi biashara nyingine zinachangamoto unaweza kuingia kichwa kichwa ukalamba mchanga ndani ya mwaka mmoja.
Jooohs:ahsante sna
 
Tangantika:umenipa hongera ila ktk kipindi cha penati umepaisha na ndo unasema ndg.uzuri umekuja ktk kipindi kizuri pia,unakitu cha utofauti umekuja ninako waza ila nisaidie/tusaidie MADINI uliyo nayo pia ahsante.
 
Ingia transport business Nunua Daladala kama za kutosha budgetbya 200m

Una option mbili
1.Nunua kutoka Japan
2.Nujua kwa mtu umtunzaji wa gari nzuri

Hiyo 27m inarudi kabla ya mwaka kwisha kama na wewe utasimamia vzr
Ngapulila:mmi biashara ya magari hapana,kunawatu wanazijua hizo biashara ila siyo mmi.yupo mmoja aliuza mabasi yake mwanza akaenda mbeya kuwekeza kwenye mpunga.nikafatilia nikasikia Jamaa alisema kisa cha kufa mapema na presha yanni.ndo nasikia anaingiza hela kwa sasa kuliko kwenye magari alipo kuwepo.
 
BT:nimekaa mda nikiwaz cha kufanya ila Madogo ndo walinifikilisha sna,maana kodi yenyewe hadi hela irudi siyo leo.ndo maana siwazi kwahiki nilicho kifanya nimefumba macho kabisa.alafu naenda kukaza mgongo tena hadi 2024 December nitakuwa najua nachezea wapi?nimejipa miaka miwili ya kutesa Mwili tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…