Hii imekaaje watu wa mitazamo ya mbali, uwekeze Mil. 330,000,000 upate Mil. 27,500,000 kwa mwaka?

Hii imekaaje watu wa mitazamo ya mbali, uwekeze Mil. 330,000,000 upate Mil. 27,500,000 kwa mwaka?

Habar za mda huu ndg na Jamaa ktk jukwaa hili.

Mimi binafsi akili imegoma Kujenga nyumba 11, kila nyumba iwe na vigezo vifuatavyo.

1.S/room 1
2. Vyumba vya kulala viwili kimoja master
3. Jiko
4. dining
5. choo cha public
6. stoo (nje ya gharama ya viwanja)sasa hii nyumba ikamilike ya kisasa itaghalimu 30m.

Kwa idadi ya nyumba 11 itaghalimu 330M.

kutokana na Mkoa husika kwa thamani ya nyumba hiyo utapangisha kwa gharama ya 2,500,000M, ikitokea bahati ukapangisha kwa 3M.

Sasa twende kwenye point unawekeza 330M unakuja kupata return yake kwa mwaka 27,500,000M.

Huu kitu imenifanya nione utajenga kama sifa ila siyo kuwa utakuwa na hela, maana ili uwanze kupata faida nimiaka 11, 12 toka umeanza kuweka vichwa.

Tusaidiane mawazo ndg ZANGU namna yakutengeneza utajiri wa akili, fikra na mitazamo mipana zaidi, najua wapo walio wekeza sehemu tofauti tofauti ila kwa nyanja Nyingine tofauti na ujenzi na wanapiga hela naomba MAWAZO yenu mitazamo yenu pia.

Hofu yangu unaweza ukawekeza kiasi kidogo lakini return yake kwa mwaka ukaipata ata ndani ya miezi 6, hiki ndo ninacho kihitaji ndg ZANGU.

Pia sina maana mbaya yakuwa watu wasiwekeze ktk nyumba hapana ila kwa Mimi hesabu zangu zinakataa tu, kama kwa kulenga kizazi chako ndo kiwape faida sawa, ila kwa Mimi ambaye nakitazama hicho kinanipa shida Ki-fikra.

Baada ya miaka 10 ukiwekeza hii Pesa ndo ninako jiona ila siyo ktk nyumba,
msaada wenu wadau.

Ahsante.
Fungua kampuni ya ukopeshaji hasa deal na watumishi wa umma kwa maana dhamana ya mkopo atakaochukua ni mshahara wake wa kila mwezi.

pia zingatia riba utakayowachaji ushauri wangu tumia 20% kwa mikopo itakayolipika ndani ya mwenzi na 40% kwa mikopo itakayolipika ndani ya miezi minne...
 
Dongo jeusi:nashukuru kwa ushauri wako...ila kunachangamoto ktk hii biashara ndg.kipindi nafanya kazi kampuni x sijaacha kazi,niliona hiyo hali walitaabika wafanyakaz sna wengine hadi wakawa wana mrahani mtoa mikopo.lakini baadae mkopeshaji sijui alikosea wapi.nilimkuta sehemu mmi ninamkumbuka ila yye hakunikumbuka kazi aliyo kuwa anafanya kipindi cha kukopesha na sasa nikumuachia MUNGU tu.
 
Wewe unatakaje ??
Usaidike
Unique Flower:umeuliza swali zuri sna.mmi nilikuwa nataka ktk hii hela nifanye biashara au uwekezaji wanamna yoyote ile ili kila siku nipate Hela itakayo kuwa inazunguka.ndo nikiwa nawaza nikasema hivi hakuna ata biashara ambazo unaweza mtu ukafanya 10m ikaleta ata kwa siku 100,000.ambazo nikifanya Mara 33,hiyo hela kwa mwaka nitapata kitu kizuri.sitaki kuwekeza kitu ambacho sitashika hela ktk mzunguko kwa siku,kwa wiki au mwezi,nataka nipumzishe Mwili kazi za kutumia nguvu nyingi nimefanya sna sasa mda wakutumia akili nyingi nguvu kidogo ili nione matunda ya nguvu zilizo potea.japo wadau mbali mbali wametoa maoni mbali mbali ninayachukuwa nayachakata nifanye lipi ahsante.
 
Kama ni real estate business.. hiyo return ya kama 8 to 9% kwa mwaka ni sawa kabisa..

Faida yake kubwa utaiona kwenye capital gain endapo value ya hizo nyumba ikipanda thamani..

Na faida nyingine ni kwamba kama una biashara nyingine hizo utazitumia kama collateral ya kupata mkopo.

So unaweza kutumia hiyo 330 million ila ukifanya valuation hapo unaweza kushangaa unapata hata mkopo wa milioni 500 then unai leverage kwenye uwekezaji mngine..

Ndo wealth creation inavofanya kazi hivo..
Hivi mkuu mfano akitumia hizo nyumba za mil 300 akakopa mil 500..halafu iyo hela akajenga tena halafu akaenda tena benki nyingine akakopea hizo nyumba za mil 500 akakopa mil 800...Halafu iyo hela akajenga tena halafu akaenda tena benki nyingine akakopea hizo nyumba za mil 800 akakopa Bil 1....Aluta continua...Inawezekana?
 
Unique Flower:umeuliza swali zuri sna.mmi nilikuwa nataka ktk hii hela nifanye biashara au uwekezaji wanamna yoyote ile ili kila siku nipate Hela itakayo kuwa inazunguka.ndo nikiwa nawaza nikasema hivi hakuna ata biashara ambazo unaweza mtu ukafanya 10m ikaleta ata kwa siku 100,000.ambazo nikifanya Mara 33,hiyo hela kwa mwaka nitapata kitu kizuri.sitaki kuwekeza kitu ambacho sitashika hela ktk mzunguko kwa siku,kwa wiki au mwezi,nataka nipumzishe Mwili kazi za kutumia nguvu nyingi nimefanya sna sasa mda wakutumia akili nyingi nguvu kidogo ili nione matunda ya nguvu zilizo potea.japo wadau mbali mbali wametoa maoni mbali mbali ninayachukuwa nayachakata nifanye lipi ahsante.
Fanya biashara ya mazao unaanza na heka 2 unaangalia inaendaje mf. Maharage na mahindi.
Jingine barber shop na massage palace design kizungu zungu na weka vitu kizungu zungu kwa siku hata laki 250000tsh unapata aisee na ingine biashara ya chakula ni nzuri unaenda shishi food unaangalia wanafanyaje kama mgeni tu nawewe unacopy nakupaste baadhi ya vitu unajua utawezea vizuri good day
Hata nyumba zakupanga ni nzuri sana faida ipo maana kila mwezi hukosi mpangaji anayetakiwa kulipa kodi nayo sio mbaya
 
Ili ujue kujenga ni raha anagalia wazee walijenga mtaa wa congo, kariakoo, magomeni wote hao wakifanya marekebisho kidogo kwenye nyumba kodi inapanda, asikiambie mtu biashara ya nyumba ni nzuri asee
 
Unique Flower:umeuliza swali zuri sna.mmi nilikuwa nataka ktk hii hela nifanye biashara au uwekezaji wanamna yoyote ile ili kila siku nipate Hela itakayo kuwa inazunguka.ndo nikiwa nawaza nikasema hivi hakuna ata biashara ambazo unaweza mtu ukafanya 10m ikaleta ata kwa siku 100,000.ambazo nikifanya Mara 33,hiyo hela kwa mwaka nitapata kitu kizuri.sitaki kuwekeza kitu ambacho sitashika hela ktk mzunguko kwa siku,kwa wiki au mwezi,nataka nipumzishe Mwili kazi za kutumia nguvu nyingi nimefanya sna sasa mda wakutumia akili nyingi nguvu kidogo ili nione matunda ya nguvu zilizo potea.japo wadau mbali mbali wametoa maoni mbali mbali ninayachukuwa nayachakata nifanye lipi ahsante.
Daladala mahesabu kwa siku ni 100k kwa pesa yako unachukua 7. Una laki 7 kwa siku. Ambayo ni milioni 21 kwa mwezi. Ndani ya miaka miwili unarevenue asilimia 165%. Ukiuza zote baada ya miaka miwili hata kwa scrap value.. unauhakika wa 200% revenue... Siyo biashara rahisi.. inahitaji uangalizi na ujanja kudeal na madereva.. mfano: kila siku dereva akija kuamsha gari.. atangulize na mahesabu ya siku.. na kila jioni gari lazima ilale kwako ama kwa mtu wako wa geregi
 
Hivi mkuu mfano akitumia hizo nyumba za mil 300 akakopa mil 500..halafu iyo hela akajenga tena halafu akaenda tena benki nyingine akakopea hizo nyumba za mil 500 akakopa mil 800...Halafu iyo hela akajenga tena halafu akaenda tena benki nyingine akakopea hizo nyumba za mil 800 akakopa Bil 1....Aluta continua...Inawezekana?
Inawezekana kama ana credit score nzuri.. na collateral valuation ikawa kubwa kuzidi loan disbursements alizonazo.. ila hatoweza kupoka zaidi ya mkopo wa awali... siku hizi ukikopa benki moja taarifa zinaenda hata kwa benki nyingine ulizopo kama umeapply mkopo.
 
Sijakuelewa vizuri swali lako la kwanza ila nitakujibu kwa kadri ya nilivyoelewa swali

Swali No 1. Thamani ya Tsh ipo kwenye interest unayolipwa kwa mwaka, mfano mzuri ni benki kuu ilitangaza mfumuko wa bei kwa mwaka huu ni 4.5% na kwasababu riba ya T-Bond ya miaka 25 ni 12.4308% ina maana thamani ya pesa yako itabaki vile vile pia utakuwa umepata faida ya 7.9308% kwa mwaka. Uwekezaji wa 330M italeta kwenye T-Bonds utaleta faida ya faida ya 26,171,640 /= TSH (hapo ukishatoa na ile asimilia ya mfumuko wa bei yaani pesa yako itabaki na thamani ile ile + na hio faida)

Swali No 2. Nchi ikifilisika ina maana itashindwa kulipa madeni yake kwa wakati, lakini madeni yatabaki pale pale si madeni ya ndani tu hata madeni ya nje. Unaponunua T-Bonds maana yake umeikopesha serikali. Nchi kufilisika ndio hatari pekee kwenye huu uwekezaji, sidhani kama kuna biashara au project au uwekezaji wenye 100% profit guaranteed. Uwekezaji ambao hauna hatari hata kidogo sidhani kama upo. Na kama upo basi nigependa sana kuujua.

Swali No 3. Vigezo vya kupanga riba ya mikopo vina tofautiana kwa kila bank. Hivyo basi jibu sahihi zaidi kuhusu hili swali watakupa benki husika unayotaka kukopa. Uzuri Benki zote zilizo chini ya usimamizi wa benki kuu wanakubali kutoa mikopo kwa dhamana ya T-Bonds.

Swali No 4. T-Bonds ya miaka 25 ina riba ya 12.4308% kwa mwaka. Hii riba inalipwa mara mbili ambayo huitwa coupon. Yaani T-Bond moja ina coupon mbili, na kwasababu ni hesabu ya mwaka ina maana kila coupon inalipwa kwa kila baada ya miezi sita. Asilimia 12.4308 ya 330,000,000 ni 41,021,640 (hii utalipwa kwa mwaka mmoja). Hivyo basi utalipwa nusu kwa miezi sita ya kwanza, na nusu ya kwa miezi sita ya mwisho. Hapo ndo tunapata 20,510,820 kwa kila baada ya miezi sita

Nadhani nimejibu maswali yako, kama kuna swali lengine Tafadhali uliza

KARIBU SANA
Samahini mkuu je mtu akiwekeza million 20.atapata gawio kiasi gani?
 
Samahini mkuu je mtu akiwekeza million 20.atapata gawio kiasi gani?
Kiwango cha gawio katika huu uwekezaji T-Bonds una tofautiana kulingana na kipindi (idadi ya miaka uliyoamua kuikopesha serikali).

Vipindi ya uwekezaji vipo saba (07) kuna miaka miwili, miaka mitano, saba, kumi, kumi na tano, ishirini na miaka ishirini na tano

Kwa mfano ukiwekeza 20M kwa
Miaka 2 gawio ni 1,586,240
Miaka 5 gawio ni 1,815,500
Miaka 7 gawio ni 1,892,660
Miaka 10 gawio ni 2,249,120
Miaka 15 gawio ni 2,281,200
Miaka 20 gawio ni 2,406,140
Miaka 25 gawio ni 2,486,160

Gawio utalipwa mara mbili kwa mwaka, nusu ndani ya miezi sita ya kwanza na nusu nyengine baada ya miezi sita ya pili. Na utalipwa hela hiyo kwa muda wote ulioamua kuwekeza. kama ni utawekeza 20M kwa miaka miwili utalipwa gawio la Tsh 1,586,240 kwa mwaka wa kwanza na hiyo hiyo pesa kwa mwaka wa pili pia. Baada ya hapo utapewa 20M yako uliowakopesha.

Utaratibu ni huo huo kama ukiwekeza kwa miaka mingine pia.
 
Asante sana kwa muongozo wako. Na nimekupata vzr..
JE kuna hii nyingine unauelewa nayo kama ndio naomba msaada wako kwa uwekezaji wa 20 million kwa mwaka mmoja kwenye LIQUID FUND. Nitapata kiasi gani cha gawio
 
Liquid fund mfuko huu unatoa gawio kwa mwaka ni 12% kwa mfn 20,000,000×12%÷100=2,000,000 ndo gawio lako kwa mwaka.
 
A
Daladala mahesabu kwa siku ni 100k kwa pesa yako unachukua 7. Una laki 7 kwa siku. Ambayo ni milioni 21 kwa mwezi. Ndani ya miaka miwili unarevenue asilimia 165%. Ukiuza zote baada ya miaka miwili hata kwa scrap value.. unauhakika wa 200% revenue... Siyo biashara rahisi.. inahitaji uangalizi na ujanja kudeal na madereva.. mfano: kila siku dereva akija kuamsha gari.. atangulize na mahesabu ya siku.. na kila jioni gari lazima ilale kwako ama kwa mtu wako wa geregi
Ayo magari hayaharibiki? Mbona hujatoa matumizi kuhusu service za kila wik mbili kumwaga Oil kubadili vipuri matairi, mbona hujalipa Bima Ratla Mapato posho za madereva emergence ndogo ndogo ajali za barabaran kukwanguliwa break down
 
Nenda njombe mkuu, kwa hiyo hela kilimo cha parachichi, unaweza nunua kijiji kizima.
Kilimo kama kubet tu,risk ya ukame,mvua chache,shamba kuungua,...ni kubwa mno kuliko risk ya kujenga nyumba na kisha zikaja kuvunjwa na tetemeko
 
hii kazi ninayo fanya unatumia msuli sna na pia mda uliotumika ni wa jasho na damu.kwa sasa mataka nipumzike ktk style ya utaftaj nibadili.ndo maana yakurudi hapa chanzo cha madini mengi.kuna watu watanielewa kazi za uchimbaj ni ngumu sna na kilicho nifanya nibadili aina ya kazi nikuona wengi wanapata 800m,500m,150m sasa baada ya muda unakuta hawapo tena ktk ramani.inabaki historia tu sasa niliona nahitaj badiliko.
Kwa nini usiwekeze kwenye government bonds
 
Back
Top Bottom