Kichaka12
JF-Expert Member
- Dec 11, 2018
- 300
- 263
Umeandika vizuri.. Japo naona kile kibiashara cha matikiti kiliingia kwa mbaali.. 😁😁😁.Mkuu mie nakushauri usirudi nyuma narudia Tena usirudi nyuma narudia Tena usirudi nyuma kwa sababu zifuatazo:
1-risk Ni ndogo
2- hakuna kushuka thamani ya bidhaa yako i.e Iyo nyumba ukisema uje kuuza after 10yrs utaweza uza like 600M.
3- both mental and financial capital ziko salama mno hakuna usumbufu na watu ama wafanyakazi otherwise like ukinunua coaster ama hiace ama bizness ingine.
4- unaweza ukazichukulia mkopo wa kujenge zingine tano Sasa ukawa na nyumba 15 so zote hizo 15 zikawa zinatumika kulipa mkopo. You've to leverage with others money, time, and all resources ili usonge mbele.
Sasa unazo 15 kwa 3m kwa mwaka unazo 45M Kama umechukua mkopo wa 160M utaulipwa nadhani ndani ya 5yrs umemaliza mkopo wao mkuu.
Baada ya hapo unachukua Tena mkopo wa nyumba 10 ambao Ni 350M unajenga zingine 10 jumla una nyumba 25 so kwa mwaka 75 Ni ndani ya miaka mitano unamaliza mkopo wao, yaani unaendelea ivyo ivyo mkuu kikubwa discipline ndio kila kitu. Fungua akaunti kwa ajili ya huo mradi yaani hela ya Kodi ya nyumba usiishike ikiwekwa huko benki wanachukua Chao ama ufungue loji uweke CCTV kamera uwe unazifuatilia japo zinahitaji close monitoring.
5- hakuna Cha economic crisis i.e inflation kwako ujue.
6- urithi mzuri kwa kizazi chako kwa baadaye na unaweza ukawa na real estate business ya uhakika baadaye ukaifnaya ikawa ama ukaisajili na abnb kwa ajili ya kupata wateja wa nje.
Naomba usirudi nyumba. Wekeza kwa basic needs za binadamu like houses aka shelter ,foods iwe isiwe lazima watu watakula ama watalala hakuna ku spare hizo basics.
Yangu Ni hayo mkuu.
Waza for 30 yrs to come utakuwa mbali mno yaani Ile uko like 60/70s wenzako wanakutamania mno yaani mno.
Yaani utashangaa unakuwa na jina na unapewa uenyekiti ccm mkoa ama wilaya Mara mbunge,kumbuka like attracts likes.
Hapo ndipo utachukua mkopo wa bilioni plus na kushusha vitu vyako kila mji mkubwa hapa tz.
Nakuombea uendelee ivyo ivyo yaani uwe litajiri ili utoe ugali kwa vijana wengi mno mtaani.
Vijana wangekuwa waaaminifu ningekuambia agiza boda zako like 150, halafu wape vijana kila boda now mktaba halafu usiwe na tamaa wewe waambie kuwa unahitaji profit ya laki sita kila boda hizi unaagiza direct from China. So kwa hizo boda zako 150*.6 unazo 90M kwa mwaka ukifanya like 10 yrs you're untouchable sema Sasa sie wazembe tunapenda kula asali pasipo kung'atwa na nyuki ujue.
Ama tunawaza kuiba ,na ndio Mana afrika matajiri Ni wachache ambao sio politicians or sio wezi ama wa magendo
Ila ni ushauri mzuri.