Hii imekaaje watu wa mitazamo ya mbali, uwekeze Mil. 330,000,000 upate Mil. 27,500,000 kwa mwaka?

Hii imekaaje watu wa mitazamo ya mbali, uwekeze Mil. 330,000,000 upate Mil. 27,500,000 kwa mwaka?

mimi nikitaka kuweka hilo wazo basi siaangali short term naangalia na mbali. hata watoto wangu watulie level inayo staili
Wazo lako zuri ila ninachotaka hii iliyopo niizalishe VP?at list ndani ya mda mfupi iongezeke.pia ukifanikiwa kuilinda na kuongezeka kwanini usijenge kwa kizazi chako baadae.ila kilichopo ndo hicho na ukianza ujenzi basi uanze kuishi kwa kitegemea kodi ya nyumba.ndo maana nawaza mbali kidogo je?ata ukifanya 10M kwa siku haiwez kuleta 100k x33x(26 mwezi)x12=?hiki ndo kina niumiza kichwa
 
Ogopa ogopa kwenda INBOX au PM y mtu. Ogopa ogopa mnooo.
Utanishukuru baadae
 
Habari yako.
Hongera Kwa harakati zako zilizokufikisha hapo ulipo na Sasa unategemea kupanuka zaidi kiuchumi.
Fanya hivi (Kwa ushauri wangu)..
1.Jenga nyumba za kupangisha tumia 33% ya mtaji wako,zikiwa tatu au tano sawa,ila usitumie zaidi ya 33% ya mtaji wako kujenga.(ziwe za kuishi au guest house )ni wewe tu
2.Wekeza kwenye biashara ya soko la hisa(stock market).napo tumia 33% tu ya mtaji wako,tafuta mtaalamu wa hii biashara mkae chini,akupe elimu vizuri,ndo biashara ambayo utaweza kupata faida hata mara mbili ya mtaji wako Kwa mwaka kama ukipata mtaalamu mzuri.
Nenda B.O.T au Dar stock exchange(DSE)Kwa ushauri zaidi.au tuwasiliane nitakupa mwongozo Kwa kina na mapana yake.
3. Kiasi kichobaki,itakuwa 34% ya mtaji wako,nayo ingawe mara mbili,Moja ifanye mfuko wa akiba na dharura,Na nyingine ni biashara ya nafaka,uwe na stoo Yako kubwa tu ya nafaka zote za muhimu eneo nzuri ,hapo ndo utakuwa huwazii pesa ndogo ndogo,.utaipata hapo.
4.Stock market inalipa,ingawa ndani na yake Kuna matapeli wengi,inabdii uwe makini,ila watu tunaona wanatajirika Kwa haraka sana kupitia kununua hisa tu za makampuni mbalimbali,Any way,Hilo mimi nakupa ushauri,kama utakuwa tayari,33% ya mtaji wako tukiamua Kwa pamoja kuwekeza huko,maarifa na uzoefu nilioko nao kuhusu stocks market investment,tunaweza kupata return ya karibu mara mbili ya mtaji utakaoweka huko.(mfano umeweka million 100,tukipambana Kwa mwaka mzima unaweza kupata 150MHadi 180M,
Mimi nitakuwa tayari kutoa muda,maarifa na uzoefu wangu,Ili tufanye hiyo biashara
UAMUZI NI WAKO .
Asante sana.
 
Habar za mda huu ndg na Jamaa ktk jukwaa hili.

Mimi binafsi akili imegoma Kujenga nyumba 11, kila nyumba iwe na vigezo vifuatavyo.

1.S/room 1
2. Vyumba vya kulala viwili kimoja master
3. Jiko
4. dining
5. choo cha public
6. stoo (nje ya gharama ya viwanja)sasa hii nyumba ikamilike ya kisasa itaghalimu 30m.

Kwa idadi ya nyumba 11 itaghalimu 330M.

kutokana na Mkoa husika kwa thamani ya nyumba hiyo utapangisha kwa gharama ya 2,500,000M, ikitokea bahati ukapangisha kwa 3M.

Sasa twende kwenye point unawekeza 330M unakuja kupata return yake kwa mwaka 27,500,000M.

Huu kitu imenifanya nione utajenga kama sifa ila siyo kuwa utakuwa na hela, maana ili uwanze kupata faida nimiaka 11, 12 toka umeanza kuweka vichwa.

Tusaidiane mawazo ndg ZANGU namna yakutengeneza utajiri wa akili, fikra na mitazamo mipana zaidi, najua wapo walio wekeza sehemu tofauti tofauti ila kwa nyanja Nyingine tofauti na ujenzi na wanapiga hela naomba MAWAZO yenu mitazamo yenu pia.

Hofu yangu unaweza ukawekeza kiasi kidogo lakini return yake kwa mwaka ukaipata ata ndani ya miezi 6, hiki ndo ninacho kihitaji ndg ZANGU.

Pia sina maana mbaya yakuwa watu wasiwekeze ktk nyumba hapana ila kwa Mimi hesabu zangu zinakataa tu, kama kwa kulenga kizazi chako ndo kiwape faida sawa, ila kwa Mimi ambaye nakitazama hicho kinanipa shida Ki-fikra.

Baada ya miaka 10 ukiwekeza hii Pesa ndo ninako jiona ila siyo ktk nyumba,
msaada wenu wadau.

Ahsante.
Mkuu mbona ni sawa tu! miaka 11 ni mbali? tangu Mwinyi awe rais huu ni mwaka wa ngapi? au ulikua bado hujazaliwa!
Je wale wenye mashamba ya miti wanawezaje kuvumilia?
 
Mkuu mie nakushauri usirudi nyuma narudia Tena usirudi nyuma narudia Tena usirudi nyuma kwa sababu zifuatazo:
1-risk Ni ndogo
2- hakuna kushuka thamani ya bidhaa yako i.e Iyo nyumba ukisema uje kuuza after 10yrs utaweza uza like 600M.
3- both mental and financial capital ziko salama mno hakuna usumbufu na watu ama wafanyakazi otherwise like ukinunua coaster ama hiace ama bizness ingine.
4- unaweza ukazichukulia mkopo wa kujenge zingine tano Sasa ukawa na nyumba 15 so zote hizo 15 zikawa zinatumika kulipa mkopo. You've to leverage with others money, time, and all resources ili usonge mbele.
Sasa unazo 15 kwa 3m kwa mwaka unazo 45M Kama umechukua mkopo wa 160M utaulipwa nadhani ndani ya 5yrs umemaliza mkopo wao mkuu.

Baada ya hapo unachukua Tena mkopo wa nyumba 10 ambao Ni 350M unajenga zingine 10 jumla una nyumba 25 so kwa mwaka 75 Ni ndani ya miaka mitano unamaliza mkopo wao, yaani unaendelea ivyo ivyo mkuu kikubwa discipline ndio kila kitu. Fungua akaunti kwa ajili ya huo mradi yaani hela ya Kodi ya nyumba usiishike ikiwekwa huko benki wanachukua Chao ama ufungue loji uweke CCTV kamera uwe unazifuatilia japo zinahitaji close monitoring.

5- hakuna Cha economic crisis i.e inflation kwako ujue.
6- urithi mzuri kwa kizazi chako kwa baadaye na unaweza ukawa na real estate business ya uhakika baadaye ukaifnaya ikawa ama ukaisajili na abnb kwa ajili ya kupata wateja wa nje.


Naomba usirudi nyumba. Wekeza kwa basic needs za binadamu like houses aka shelter ,foods iwe isiwe lazima watu watakula ama watalala hakuna ku spare hizo basics.

Yangu Ni hayo mkuu.

Waza for 30 yrs to come utakuwa mbali mno yaani Ile uko like 60/70s wenzako wanakutamania mno yaani mno.

Yaani utashangaa unakuwa na jina na unapewa uenyekiti ccm mkoa ama wilaya Mara mbunge,kumbuka like attracts likes.
Hapo ndipo utachukua mkopo wa bilioni plus na kushusha vitu vyako kila mji mkubwa hapa tz.

Nakuombea uendelee ivyo ivyo yaani uwe litajiri ili utoe ugali kwa vijana wengi mno mtaani.


Vijana wangekuwa waaaminifu ningekuambia agiza boda zako like 150, halafu wape vijana kila boda now mktaba halafu usiwe na tamaa wewe waambie kuwa unahitaji profit ya laki sita kila boda hizi unaagiza direct from China. So kwa hizo boda zako 150*.6 unazo 90M kwa mwaka ukifanya like 10 yrs you're untouchable sema Sasa sie wazembe tunapenda kula asali pasipo kung'atwa na nyuki ujue.
Ama tunawaza kuiba ,na ndio Mana afrika matajiri Ni wachache ambao sio politicians or sio wezi ama wa magendo
Nipo 20's ila ngoja ni save hii nondo huku nikiendelea kuifuatilia kwa ukaribu kabisa .
 
Biashara ya nyumba ukusaidia usife njaa na kulinda mtaji wako maana kila siku hizo nyumba zitapanda thamani. Zitarudi hio pesa kwa miaka 10 na thamani yake itapanda toka m330 hadi m 500 ukitaka kuziuza.
 
Jenga hizo nyumba then zipangishe pia zitumie kuombea mkopo kisha fanyia biashara ya kuuza viwanja. Unanunua mashamba unayaongeza thamani kwa kuweka miundo mbinu then unauza so hela ya mkopo itarudi , plus faida juu
 
Nenda mtwara nunua shamba ekari 150 lima kwa kutumia mtaalamu wa kuajir ashaur kuanzia uchaguzi shamba usiwe bahili miaka 3.5 utaanza vuna mwaka wa 5 utakuwa unapata mil 300 naaa kila mwaka kwa miaka 15 mfululizo
 
Usipopata wewe watapata watoto wako au wajukuu zako, jenga nyumba.
 
Mkuu mbona ni sawa tu! miaka 11 ni mbali? tangu Mwinyi awe rais huu ni mwaka wa ngapi? au ulikua bado hujazaliwa!
Je wale wenye mashamba ya miti wanawezaje kuvumilia?
Ahsante kwa ushauri wako,ila sitaki kurudia nilicho kifanya kwani nimeteseka kipindi cha nyuma niliwekeza Miti ya mbao tushamba twangu bado sijavuna ila nilitaabika sna ata bank walikataa kunipa mkopo kisa wakinga wengi walienda miaka ya nyuma wakachukuwa mikopo kupitia miti,sasa mkinga kumbe ndo kauza hivyo hakuna la marejesho kinacho tokea bank inataifisha Miti ukika kuangalia Miti imebakia labda miaka 5/6 ivunwe sasa bank inakosa mzunguko hadi ikomae Miti inakuwa mtihani kwa bank.hapo mwenyeji kaenda kununua ghorofa dar kibiashara zaidi.ndo bank inataka hati ya nyumba na rekodi za biashara unayo fanya ili ikupe mkopo na elimu wanakupa ya mkopo,sasa mmi ninakajishamba kangu alafu sina biashara yoyote pia ndo nilitegemea hiyo miti kwahiyo ndg niliteseka sna,ndo kuja hapa nikitaka RAMANI ya kunipeleka Mbele na kuiona hela ikiongezeka,siyo nisubilie tena baada ya kuwekeza.
 
Jenga hizo nyumba then zipangishe pia zitumie kuombea mkopo kisha fanyia biashara ya kuuza viwanja. Unanunua mashamba unayaongeza thamani kwa kuweka miundo mbinu then unauza so hela ya mkopo itarudi , plus faida juu
Ahsante ndg kwa ushauri wako, kuna MTU niliwahi kumuona miaka ya nyuma alinunua shamba kama heka 6 kisha akazikata viwanja na barabara akaweka nguzo na Umeme na maji akawa anauza 6m- 8m umenikumbusha mbali sna zaidi ya miaka 15 niliona ahsante sna ndg
 
Usipopata wewe watapata watoto wako au wajukuu zako, jenga nyumba.
Ahsante ndg kwa ushauri wako,kujenga nitajenga ila kwa faida mfano ninao umiza kichwa hapa ni je?10m (kwa siku laki inawezekana?) Kwa biashara zipi?Mara 33 alafu Mara mwaka nitakuwa nimepata hela ata yakujenga Mara mbili ya Pesa hii.faida mwaka mmoja siyo tena miaka 11 ya kusubilia faida nahisi umeelewa hesabu ninazo waza mkuu
 
Biashara ya nyumba ukusaidia usife njaa na kulinda mtaji wako maana kila siku hizo nyumba zitapanda thamani. Zitarudi hio pesa kwa miaka 10 na thamani yake itapanda toka m330 hadi m 500 ukitaka kuziuza.
Nimekuelewa ndg,sijakataa kujenga ila natazama je?hii hela niwekeze kwenye nini ndani ya mwaka nipate faida na hela irudi ata kujenga unajenga bila shida.kuliko nisubilie miaka 10-11 na ndo niaze kuona matunda,labda umepata PICHA kidogo
 
Nimekuelewa ndg,sijakataa kujenga ila natazama je?hii hela niwekeze kwenye nini ndani ya mwaka nipate faida na hela irudi ata kujenga unajenga bila shida.kuliko nisubilie miaka 10-11 na ndo niaze kuona matunda,labda umepata PICHA kidogo
Jenga ndani ya miezi 3 upangishe kisha chukulia mkopo ufanye biashara ya kuuza viwanja au kama hobbies ipo nunua plant ya kusaga kokoto KILA siku watu wanajenga haina hasara hii wala stress.
Au nunua hisa au bond kwenye makampuni makubwa nje ya nchi kila baada ya mwezi unakula gawio
 
Back
Top Bottom