Kelams Swali zuri,
Kwanza sijajua umri wako lakini mathalani kwa kijana wa makamo (25-35) ni vema kabla hajaingia kwenye swala la ndoa atambue anataka nini kwenye maisha yake (vipaumbele).
Wapo watu ambao familia ni kipaumbele cha kwanza kwenye maisha yao, wapo wengine wanahitaji kutimiza malengo mengine tofauti ya kimaisha kabla ya ndoa, yote kwa yote hakuna umri maalum ulioahinishwa kuoa, cha kuzingatia ni viupaumbele vyako ulivyojiwekea.
Kukujibu swali lako la kuhusu kipato na ni kwa namna gani atagundua kuwa amefikia kiwango kitachomuwezesha kuoa.
Kwanza pesa haijawahi kutosha maishani, mathalani hata matajiri kila siku wanapambana kuongeza vipato vyao, kwahiyo hakuna muda utafika na kusema pesa imetosha kuingia kwenye ndoa ila cha msingi ni pale ambapo utaona unaweza kujikimu wewe na huyo mtarajiwa wako pamoja na familia, hii pia itategemea na mtu utakaetaka kuwa nae na maisha (lifestyle) mnayoishi, kama utataka kuingia kwenye ndoa na "madunga embe" (slay queens) hapo ni lazima ujipange haswaaa, lakini kwa maisha yetu ya kitanzania hakikisha una kuwa na mtu utakae mmudu kwa kipato chako lakini pia jitahidi uongeze vyanzo vyako vya mapato kwasababu unapoingia kwenye ndoa tegemea baada ya muda familia itaongezeka (watoto), watahitaji kula, kuvaa,kusoma n.k.
Kupanga ni kuchagua.