johnmashilatu
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 841
- 909
Wakati bajeti ya mwaka 2024/2025 ikisomwa, ilielezwa ujenzi wa barabara ya njia nne kati ya Mwanza hadi usagara, ungefanyika.
Bajeti mpya ya 2025/2026 itawasilishwa hivi karibuni. Mwezi uliopita waziri mpya wa ujenzi alifanya ziara Mwanza.
Tuliona vifaa vya kutengeneza barabara vikichimba eneo la Mkuyuni. Kisha kimetokea kimya kikuu na hata hivyo vifaa havionekani tena.
Barabara imechimbwa upande mmoja, shughuli nyingi zimeathirika, kisha kimya kikuu kinatokea.
Tunajiuliza kuna nini? Hakuna pesa? Kwanini ilichimbwa wakati wa ziara ya waziri?
Maswali ni mengi pale wanapojenga SGR barabara imefungwa upande wa kutoka mjini, kuanzia Chakechake hadi Mswahili, kufanya matengenezo ya kama mita 500, sasa ni zaidi ya mwezi, hakuna kinachoendelea.
SGR yenyewe imesimama, Mv Mwanza haijulikani, Soko kuu? Daraja la Magufuli? Kuna nini?