Hii kasi ya ujenzi wa bararara ya njia nne Mwanza- Usagara ni sawa?

Hii kasi ya ujenzi wa bararara ya njia nne Mwanza- Usagara ni sawa?

johnmashilatu

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2010
Posts
841
Reaction score
909
Wakati bajeti ya mwaka 2024/2025 ikisomwa, ilielezwa ujenzi wa barabara ya njia nne kati ya Mwanza hadi usagara, ungefanyika.

Bajeti mpya ya 2025/2026 itawasilishwa hivi karibuni. Mwezi uliopita waziri mpya wa ujenzi alifanya ziara Mwanza.

Tuliona vifaa vya kutengeneza barabara vikichimba eneo la Mkuyuni. Kisha kimetokea kimya kikuu na hata hivyo vifaa havionekani tena.

Barabara imechimbwa upande mmoja, shughuli nyingi zimeathirika, kisha kimya kikuu kinatokea.

Tunajiuliza kuna nini? Hakuna pesa? Kwanini ilichimbwa wakati wa ziara ya waziri?

Maswali ni mengi pale wanapojenga SGR barabara imefungwa upande wa kutoka mjini, kuanzia Chakechake hadi Mswahili, kufanya matengenezo ya kama mita 500, sasa ni zaidi ya mwezi, hakuna kinachoendelea.

SGR yenyewe imesimama, Mv Mwanza haijulikani, Soko kuu? Daraja la Magufuli? Kuna nini?
 
Huko hakuna tofauti na Mbeya,, Upanuzi wa njia nne katikati ya Jiji Toka mwaka jana mwanzoni mwa mwaka Hadi kufika Leo hii kazi haieleweki. Hawa Kandarasi sijui wanafanyia nn,,
Wanaichelewesha sana Serikali kumaliza miradi waliyojiwekea kwa wakati.
 
Nafikiri wakandarasi tutawaonea, hapa ni yule aliyetoa kazi, ajitokeze atupe majibu.
 
Sio mwanza tu hata kahama hakuna la maana barabara za mitaani zifumuliwa na kuachwa tu bila muendelezo.
Tuliambiwa kuna mabilioni kwa ajili ya matengenezo ya barabara zilizoharibiwa na mvua za mwaka jana, lakini hali ni tofauti.
Hapo Mwanza, barabara nyingi za mitaa ni kama zimepigwa mabomu!
 
Huko hakuna tofauti na Mbeya,, Upanuzi wa njia nne katikati ya Jiji Toka mwaka jana mwanzoni mwa mwaka Hadi kufika Leo hii kazi haieleweki. Hawa Kandarasi sijui wanafanyia nn,,
Wanaichelewesha sana Serikali kumaliza miradi waliyojiwekea kwa wakati.
Hapa tatizo linalojitokeza ni kuanza miradi mipya kabla ya kumaliza Ile ya zamani. Miradi inarundikana hata haijulikani upi ni upi. Mawaziri husika hudaganywa kuwa kazi inaendelea na wafanyapo ziara Wakandarasi huwekwa vifaa vyao kazini ila wakiondika vinarudishwa camp. Kibaya zaidi ni kutoa taarifa za uongo kwamba mradi umefikia asilimia 95 ilhali hata kwa macho hizo 20 hazifiki. Hali hii inatisha na si salama kwa maendeleo ya Taifa.
 
Back
Top Bottom