Hii kasumba ya mtu kutoa comment ili apate reactions nyingi huwa inawafaidisha nini?

Hamna Chocho
Tu Tuishii Tyu MakeMake
 
Eti nini? Unataka tuwe siriazi humu mitandaoni? Aaaa wapi!

Napost cho chote ninachojisikia katika mada yo yote muda wo wote na po pote...na hakuna kitu utanifanya! 😂😂😂

View attachment 3645454
Yeah, hata mimi naandika cho chote,
muda wo wote,
nikitukanwa tusi lo lote,
Mimi hujibu kwa matusi yote,
yaani tutafikisha po pote.

Potelea pote!
 
Mmeshimiwa anataka tuwe wapole,wenye umaridadi na unyoofu kama tunaenda kula kiapo cha utii.
Sio kiviile. Nilivyomwelewa ni kwamba unaweza kukoment lakini kwa mtindo wa kulichangamsha jamvi. e.g. hii comment yako hapo juu umeianza vizuri na ulivyoimalizia "tunaenda kula kiapo cha utii" imewaacha wasomaji wako wakiwa na furaha mithili ya wale wanaokwenda kula kiapo hicho na sio wakiwa wamekereka kama mtu aliyelimwa barua ya onyo kali na boss wake.
 
Ebo!

Gunner unapenda kucontrol dunia, yesu mwenyewe alishindwa…. Mambo mengine let them slide.

Wakati we yanakukasirisha mimi i wonder wanatoa wapi hivi vipicha ili na mi niwe navitumia, hadi kuna siku niliuliza kwenye uzi.

Elewa kitu … tunatofautiana sana, na hiyo ndio raha ya community. Kikawaida binadamu huchoka kutumia akili, na ndio hapo mediocre na matani yanapochukua nafasi.

Ukiweka mada focus na wale wanaoijadili. Zamani kulikuwa na mtu lazima aweke picha, sijui yuko wapi yule jamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…