PreGE2025 Hii kauli "Kama washaharibu nchini kwao wasije nchini kwetu kutuharibia pia" Rais Samia alikosea sana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Libya ilidondoshwa na mtu mmoja kwa speech ya dk kadhaa akiwa nchi nyingine. Ije kuwa watu watano waliobeba ajenda za taifa/mataifa

Msichukulie mambo poa mkuu
 
Na wewe unataka 🍰 keki....

Je ingekuwa wewe ndio rais ungeacha tu upumbavuu unaotaka kukuengua kirahisi


Pakichafuka
Kwani wanachodai ni cha uongo? Wangekuwa wanasema uongo wala mimi nisingewasuport ila ni vya kweli mtupu!
 
Andishi zuri lakini kuna careless au deliberate mistakes nyingi. Edit
 
Hajui diplomasia
 
Bors ungeficha Ujinga wako.
Ila basi!
 
Machafuko gani? Mbona Uganda wamepolekelewa vizuri tu umeona kuna vurugu au machafuko?
 
Hana habari , maana mwendo wa kikasuku
 
Tanzania sio shamba la bibi, tunayo mengi sana ya kufanyia kazi ili uchumi wetu upae. Sio jukwaa la kisiasa.

Tupunguze kujiona wanyonge kwenye hizi siasa za kikanda.
 
Kama nchi tume tumechafukaaa sana
Wamechafuka hao kina Karua na marafiki zao wa huko Ulaya wanaowatuma kufanya upuuzi huku afrika.

Mudavadi kuwakosoa wanaharakati wa Kenya akiwa ni mwanasiasa mwandamizi ni ushahidi tosha hao wanaharakati wamechamka vibaya.
 
Libya ilidondoshwa na mtu mmoja kwa speech ya dk kadhaa akiwa nchi nyingine. Ije kuwa watu watano waliobeba ajenda za taifa/mataifa

Msichukulie mambo poa mkuu


Nyie ndio mnamfanya Rais apoteze uelekeo na aataanguka vibaya .Ni bora mngemshauri vizuri . Libya hakuanhushwa kwa kura bali kwa nchi kuvamiwa.

Samia anaogopa kushindwa kwenye sanduku la kura sasa anataka kupeleka nchi kwenye vita na majirani .

Hivi uliwahi kuona wapi mapinduzi yanayofanywa na Vyama vya upinzani kama sio ulimbukeni na ujinga wa kisiasa.
Yana kwa akili za kijinga kabisa mtu anasema eti Tundu Lisu anataka kupindua nchi . Huo ujinga wanaambiwa wapumbavu na watu walioishia kwenye elimu ya madarasa na kufundishwa ugaidi tu sio siasa .

Hakuna Chama kinachoweza kuingia madarakani kwa mapinduzi ?
Mapinduzi yanafanywa na Jeshi na sio wanasiasa .

Wanasiasa wanafanya siasa na harakati za kupata kura kupitia uchaguzi tu. Hakuna mwanasiasa mjinga anayeweza kujaribu kupindua serikali maana hataweza kutawala .
Ataipundua serikali halafu atakaaje madarakani wakati yeye ni raia. Ataapishwa na nani ili awe amiri jeshi mkuu . Atafanyaje kazi wakati chama alichokipindua kina watu wengi na wenye nguvu za kisiasa ,kiuchumi na hata kuishawishi . Hivi unafikiri CCM ni chama kidogo cha kuipindua kirahisi tu halafu ukalie kiti ikulu ?
Ni mitizamo ya kishetani tu inayotumika kuua na kuumiza watu lakini wenye akili wanakataa huo ujinga ndio maana maaskofu wenye akili kubwa kabisa wanakataa hizo propaganda maana wanaelewa na wamesoma na kuzijua siasa za dunia na Roma ndio waasisi wa siasa ,utawala ,mifumo ya kijeshi na protocol zake na sheria zote za kiutawala duniani nzima .

Lisu na wanaharakati duniani kote wanataka kuona uchaguzi ukifanyika kwa haki .Ili watu wachague . Tunaona hata ndani ya Chadema uchaguzi ulifanyika kwa wazi lakini hakuna vurugu kwa sababu hapakuwa na kificho . Lisu alitumia nguvu ya ushawishi na propaganda za kisiasa akamshunda mshindani wake na kuingia madarakani .
Hizo ni mbinu za kisiasa na sio uhaini .

Mara ooh Libya sijui wanajuta kumuua Gadaffi sijui upuuzi gani ?
Hata waliomuua Jiwe wanajuta maana kiti hakikaliki .

Gadafi alikosea mwenyewe kuua watu wake . Yaani alianza kuwaona waandamanaji kama panya na akaapa kuwamaliza wote kwa risasi.
Kwa upumbavu wake kufikiri kwamba kuwa Rais ni kumiliki mpaka roho za binadam kama mnavyomdangaya Rais Samia .

Mlitegemea Dunia ikae kimya Gadafi aue wale wote waliokua wanaandamana kumpinga .
Mbona Tunisia, Morocco na Misri kuko shwari baada ya maandamano ya kuwapinga viongozi wao . Watu ni muhimu kuwasikiliza na sio kuwaua eti ndio unatafuta amani ? Katika mifumo ya kidemokrasia duniani kote watu wanaheshimiwa sana .Vingenevyo basi CCM waachie nchi jeshi litawale kuliko wanajifanya kuwa kuna demokrasia huku wakiwa wanatumia jeshi kutawala kwa manufaa yao .

Na kumlinganisha na Gadafi ni utovu wa nidhamu maana Gadaf aliingia kwa mapinduzi kuitawala Libya wakati Tanzania Rais anapatikana kwa kura . Hata hivyo, Gadafi angekaa chini na wapinzani wake angepata hasara gani kama sio Tamaa ya madaraka kama aliyonayo Samia ?
Asili ilivyo yeyote anayetaka kwa mapinduzi naye atatolewa kwa mapinduzi . Hata Zanzibar kama sio Tanganyika kuwabeba wangekuwa wanapinduana kila siku maana wameingia kwa mapinduzi .
Lini Watanganyika waliwahi kutafuta silaha za kuuana kwa sababu ya siasa .? Jibu ni hakuna. Rais Samia ameonyesha wazi kuwa ndiye aliyekua anamshauri vibaya Magufuli kisiasa maana amebaki peke yake lakini amekua mbaya zaidi na Muoga huku akishindwa kulinda rasilimali za nchi jambo ambalo ndilo limalonyemelewa na Mabeberu .

Kama Samia angekuwa mzalendo wa kulinda mali za umma kwa nguvu zote hata mimi ningeamini kuwa huenda kuna chokochoko za kutaka kumpindua lakini yeye ni kibaraka wa kuuza rasilimali zote za nchi kwa Wazungu na washirika wake wa Falme za Kiarabu halafu eti wazungu wanataka kumpindua, ni mwenda wazimu pekee atakubali hizo propaganda za wezi .
Ni Kibaraka gani anayemtaka Lisu Gwiji la Sheria za kimataifa na mikataba yake .
Mwizi anatabia ya kugeuza kibao anapoona watu wanamkimbiza kistaarabu .

Mara sijui ushoga sijui wanatumiwa na wazungu ,ujinga mtupu . Wakati Samia alifadhiliwa na wazungu kuwa kama Mvumbuzi na mchora tamani wa ukoloni mambo leo kupitia Filamu ya Royal Tours. Wazungu na waarabu wakauona utajiri wa Tanganyika wote na jinsi ambavyo watu wake ni wapole na wasio na uwezo wa kutumia rasilimali zao wenyewe matokeo ya udalali wa royal tours ni nchi kuvamiwa na matajiri wa kiarabu na kizungu kugawana ardhi na misitu na kila kitu kwa kutumia rushwa kubwa kila mahali na ndio wanaotumia nguvu kubwa na kumpa mabomu ya kuwaua wapinzani na Maaskofu na kuumaliza ukristo Tanganyika iwe kama Zanzibar .

Kama Samia anakubalika basi aweke Tume huru na aache kutumia vyombo vya dola kuua na kutesa watu kisha uchaguzi ufanyike kwa haki tuone kama atashinda kwa kwa zaidi ya 53 % kama sio kushindwa kabisa.

wazungu miaka yote walipinga ujeniz w mahoteli y kitaalii kwenye mbuga za awn'ewnyama lakini kwenye utawala wa Samia wazungu na waarabu wanashindana kujenga mahoteli kwenye mbuga za wanyam
 
Bora uchaguzi ufike na upite salama, tuendelee na maisha mengne. Maana inataka kuwa kama...
 
Mali ndio zinatakiwa zilindwe kwa hali na mali
Watu wanaiba matrillion kwenye ripoti ya CAG wametajwa ila hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua wapo mtaani wanadunda na wanatukana na kukejeli raia.
 
I will say it again, Samia is incompetent, kea, maneno ya, Profesa,mmoja wa, Kenya, "she was, promoted to incompetence" Samia(AKA, idi amini mama"amepewa, kazi, asiyoijua, hakustahili hata kua mkuu wa, wilaya, Leo ndio yupo ikulu, ni, mwendo wa, kuiba, tu, kwa, sababu wasaidizi wake, ambao na wao ni wezi wanajua boss wao ni kila za, so watamsaidia kubaki ikulu, Ila na yeye asiwaingilie kwenye deals zao, za kupiga deals haramu za kuikamua nchi! Kila, MTU aide, alimbikize kwa uwezo wake,
 
Sio kila wakati au kila jambo hujibiwa kwa kuwa humble inatakiwa uonyeshe ukali ili wale wanaotamani kukuchezea wapate hofu...hii inaitwa situational style of leadership
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…