Hii kauli ya Mo ingekuwa ni kwa wana Yanga asingekaa

Hii kauli ya Mo ingekuwa ni kwa wana Yanga asingekaa

Hii kauli ya kanjibai kwa wanasimba ingekuwa kwa wana yanga kusinekucha kuachia ngazi. Sema wanasimba hawajali sana wapo wapo tu. Ifike wakati wanasimba tuamke bora timu iwe kama PRISON kuliko kusimangwaaaa
Kuna mtu alishawaita nyie ni 'wala mihogo' tu, mlimfanyaje?
 
Klabu ya Simba imetenga bajeti ya zaidi ya Sh 13.7 Bilioni mwaka 2023/2024.
Katika bajeti hiyo, Simba inatarajia kukusanya fedha kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato ikiwamo udhamini.
Akisoma taarifa ya mapato na matumizi, Mkuu wa kitengo cha fedha wa klabu hiyo, Suleiman Kahumbu amesema kwenye udhamini wataingiza zaidi ya Sh 3.9 Bilioni.

"Pia Vunja Bei atatoa Sh 725 Milioni, haki za matangazo Azam Tv Sh 2.5 Bilioni na matangazo ya Ligi Sh
410 Milioni na kwenye vyanzo vinginevyo" anasema
Anasema katika bajeti hiyo,
kuna upungufu wa Bilioni 3.9 ambazo rais wa heshima wa klabu hiyo, Mohammed 'Mo' Dewji ameitoa.
Akitoa mchanganuo wa matumizi ya bajeti hiyo anasema kwenye usajili watatumia zaidi ya Sh 2.4 Bilioni wakati mishahara ya wachezaji na wafanyakazi wengine wa klabu ni zaidi ya Sh 4.8 Bilioni.
"Bonusi kwa wachezaji ni Sh 840 milioni, leseni na vibali kwa wageni na benchi la ufundi ni Sh 189 Milioni," anasema.
Simba pia imetenga Sh 578 Milioni za kodi ya pango, usafiri wa ndani na nje ya nchi Sh 874 milion, posho za wachezaji Sh 102milioni .
Huku ikitenga pia zaidi ya Sh 26 Milioni za matengenezo ya magari yao, Sh 500 milioni za chakula timu zao zikiwa kambini.
Suleiman aligusia bajeti ya msimu uliopita ya Sh 11.9 ambayo ilipitishwa na mkutano mkuu uliopita na kukusanya Sh 12.7 Bilioni huku Mo Dewji akiongeza Sh 2 Bilioni katika bajeti hiyo.
Msimu uliopita, klabu hiyo ilitumia zaidi ya Sh 4.38 bilioni kwenye mishahara, kambi ya wakubwa Sh 2.2 Bilioni, timu ya wanawake Sh 199 milioni.
Masuala ya utendaji zaidi ya Sh 2.6 Bilioni na malipo mengineyo Sh 385 milioni wakati usajili ulitumia Sh 1 Bilioni
 
Mbona hata injinia Hersi alisha kili hilo kuwa Yanga inaendeshwa kwa hasara.

Kiufupi Tukiachana na ujuaji wa kipumbavu kama ilivyo kawaida yetu watz ni kuwa karibia asilimia 97 ya virabu barani Afrika vinajiendesha kwa hasara.

Mtu hajawahi kuendesha hata biashara ya mtaji wa milion 2 lakini amejaa ujuaji kibao na wakijinga.
Sio Africa tu kiujumla biashara ya mpira kwa wawekezaji hata kama ina faida si kama ile waipatayo kwenye biashara zao nyingind, ni mapenz yao ya soka ama lah prestige tu wala sio ishu za faida.

Ndio maana wawekezaji huwa ni matajiri haswa na sio wataftaji
 
Back
Top Bottom