Kwa kua umenijaza kichwa ngoja nishushe madini kamili kwa mtoa swali Hahaha iko hivi lengo mama la protocol (Itifaki) ni kuhakikisha ukamilifu wa hafla husika(hafla iende kama ilivyopangwa kuanzia mda, dhima, ukaaji, uondokaji, chakula nk) , kustarehe kwa wahusika wakati wa hafla bila bugudha na karaha(being comfortable+ not being embarrassed)....Kwa kuzingatia hilo afisa itifaki aliyekomaa ni lazima awe shapu kwenye kujiongeza hiyo inahusisha vitu kama kuwa uelewa juu ya tamaduni za kwao na mgeni zikoje(mf Utamaduni wa barabados mwanamke anakaa kushoto wewe kama afisa itifaki kwenye hafla mgeni wa Barbados ambaye ni mwanamke imeonekana atakaa kulia moja moja hawezi kuwa comfortable hivyo afisa anajiongeza anammegua kiana) , wanaokutana mahusiano yao binafsi yakoje mf enzi za jakaya usingeweza kumpanga pemben ya kagame hata kama seniority/precedence ya ukaaji ilitaka hivyo(walikua hawaivi hivyo wasingekua comfortable)....kwa kusema hayo sasa turudi kwenye swali la msingi la Bwana
MUTUYAMUNGU kumbuka nchi ya Misri ni dola ya kiarabu na Rais wake ni Muislamu safi unajua kwenye taratibu za Kiislamu na kiarabu mwanamke hawezi kuongoza dola, Huenda ilibabisha Rais wa Misri kuwa uncomfortable na kumhost Rais wa kike ila kwa maslahi ya nchi akawa hana jinsi kuipa nguvu hoja hii kiitifaki aliyetakiwa kumsinidkiza Rais Samia kama Rais wa Misri alikua na Udhuru usiokwepeka basi ni waziri wa mambo ya nje ila bahati mbaya naye ni mwanaume na muislamu swafi...Chief of Protocol wa misri kwa utashi akaamua kumpa mwanamke ambaye kwanza atakua na comfortable kuwa na mwanamke mwenzie ambaye ni kongozi mwenza.
2.Sababu ya pili ni ushawishi lengo la mahusiano ni kufikia interest za nchi husika inawezekana janja ya Egypt kumtumia mwanamke mwenza ili kumlainisha zaidi katika kupersue interest za dola ya Misri, si unajua mambo ya wadada tena (Kama upo makini utagundua sababu hii inarejea comfortable and not being embarrassed...
3.Sababu ya tatu imetajwa kama Udhuru wa Rais wa Misri kwenye kikao
Kwa Mantiki hayo ITIFAKI ITAKUA IMEZINGATIWA BILA KUJALI NANI KAMUAGA IKIWA TU ZIARA ILIENDA KAMA ILIVYOPANGWA NA RAIS SAMIA PLUS WENYEJI WAKE WALIKU COMFORTABLE NA HAKUKARAHISHWA