May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Kumekuwa na mijadala iliyoibuka haswa kwa hizi timu zetu kongwe huku kila upande wakijaribu kutumu kuwa Refa alipendelea timu kubwa.
Mbaya zaidi ni pale hata wale wenye nafasi ya kusikilizwa au kuaminiwa kama Makocha, nao wakiingia kwenye mkumbo huo.
Inashangaza na kuhuzunisha kwa Mtu Mzima mwenye akili timamu anapopambana kupinga adhabu kwa tukio ambalo hata angekuwa yeye ndio anachezesha angelazimika kutoa kadi kwani sheria na kanuni inataka hivyo.
Tunawapa presha bure Waamuzi ili hali hakuna tukio mahsusi Mtu analoweza kulisisitizia kuwa Refa kafanya upendeleo wa makusudi...matukio mengine ni hamsini kwa hamsini na kwa uamuzi wowote ambao Refa angefanya basi lazima angelaumiwa na upande mmoja.
Mimi sio Mtaalamu wa soka lakini kwa kuona tu walau naweza kufanya tathmini ya kiwango changu.
Kwa mfano mechi ya juzi ya Simba na Namungo ilitawaliwa sana na uchezaji wa kukamia haswa kwa upande mmoja ambapo Refa alikuwa kwenye mtihani mkubwa wa kukwepa mitego ya udanganyifu iliyokuwa ikifanywa na Wachezaji ili kunufaika kirahisi... haswa wale wa Namungo..kiukweli tunatakiwa kumpongeza Muamuzi maana alikuwa kwenye wakati mgumu.
Mara kadhaa tuliona Wachezaji wakijiangusha na Refa alipowapotezea waliamua kuamka wenyewe na kuendelea na Mchezo.
Tukio kama la Morison, Manula au Boko, huenda wengi tungetamani Refa angetoa adhabu lakini sasa tukumbuke kwa aina ya uchezaji waliokuwa wanaonesha Vijana wale ni ngumu kujua kama kweli ilitumika nguvu kubwa au aliguswa tu na kujitupa chini kwa kishindo ili kumshawishi Mu/Waamuzi?.
Tukumbuke sisi tunaangalia kwa karibu kupitia Runinga ili hali Muamuzi yeye alikuwa anafuatilia kule Mpira ulipo tofauti na camera inayotuonesha sisi Watazamaji...Hivyo Waamuzi wasipokuwa makini wangejikuta wanatoa adhabu kwa faida ya aliyedanganya.
Tukio kama la Inonga kwenye mechi na Coast ambapo ilibidi aadhibiwe kwani kupeleka kichwa chake tu inatosha kuonesha nia ovu hata kama Mchezaji yule hakuguswa...na tusiwe Wanafiki hivi Mtaani kweli Mtu ataangushwa kwa kupigwa kichwa chepesi vile?...lakini kwa kuwa kuna sheria za mpira na kanuni basi ilibidi aadhibiwe na ilikuwa haki.
Kadi nyekundu ya Namungo, Ruvu shooting hivi kweli tunawataka nini Marefa?. Kwa Mechi zote hizi mbili sijaona kukosea kukubwa kwa Marefa mpaka kustahili kushutumiwa kwa nguvu na misuli ya shingo kututoka.