Hii michango inayochangishwa na watu binafsi kwa ajili ya janga la Karikoo ifuatiliwe

Hii michango inayochangishwa na watu binafsi kwa ajili ya janga la Karikoo ifuatiliwe

Kiukweli nimejaribu kutafakari ili kujiridhisha kuhusu michango inayochangishwa na baadhi ya watu maarufu kuhusu janga la Kariakoo ila naona ni kama utapeli. Ikumbukwe kwa ishu ya Kariakoo tayari serikali iko pale na kusimamia kila kitu kwa 100% huku taasisi kubwa nyeti nchini zikiwa kwa karibu sana na serikali.

Na hadi sasa msaada mkubwa unaohitajika ni jinsi tu ya kuwatoa walionasa. Sasa hawa wenzetu wanaochangisha wananchi pesa nini lengo lao?

Pia soma: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Watu 7 wengine waokolewa

Ifike sehemu Watanzania tusiwe kama nyumbu kuchanga pesa hovyo hovyo na kuishia kuwafaidisha wahuni wachache. Pia serikali iwe inatoa kibali maalum cha kuchangisha michango na sio mtu kujiamulia tu kisa ni maarufu.
Walaumiwe wanaotuma na sio wachangishaji
 
Serikali na wenyewe wameweka bakuli. Bora kuchanga kwa mtu baki kuliko serikali.
 
Hata usisumbuke kufuatilia, Tuliwahi kupokea michango ya Tetemeko la Ardhi lililo haribu miundombinu na makazi ya watu huko Kagera, hatakujua ilitumikaje na nini kilitokea.

Balozi zingine zikajitolea kujenga mashule na kurudisha miundombinu, lakini serikali ikasema walifanya wao, kwasababu tu walitoa SUMA JKT kujenga.
Duh! ...usitukumbushe mkuu yale ya Kagera enzi zile maana....
 
Ulichoandika inaonyesha una wivu pia kwa Niffer, nawe unauza nini?

Umejiandika kwa sababu unafikiri kila mtu kama wewe.
Utapeli wabongo tunawajuwa
Hapo angewapelekea biskuti,juice za 500 basi pesa zingine zingewekwa kibindoni


Ova
 
Back
Top Bottom