Ndugu
Nyamesocho unahoja kubwa sana japo watu watachelewa kukuelewa na nadhani kwa sababu zifuatazo:-
1. ATHARI YA KUONA WANAWAKE WAKITEMBEA NUSU UCHI
Watu wengi wanashindwa kuona uzito wa hoja yako kwakuwa wameathirika na mwenendo wa wanawake wengi wa sasa juu ya mavazi yao. Wengi katika wachangiaji wanaishia kulinganisha hali halisi ya wanawake kwenye mavazi na hiyo midoli na hivyo kuifanya hiyo midoli kuweka bila stara kwamba sio kitu. Kwa kifupi tu,kama kuona LIVE kupo na kushazoeleka sasa RECORDED inakusumbua vipi?
2. KIASHIRIA CHA NAMNA GANI MAADILI YETU YAMEMOMONYOKA.
Hoja namba moja inaenda sambamba na hii,tofauti ni kwamba hii ni hitimisho lake. Waingereza wanasema "Two wrongs dont make it right", na ndicho kinachotokea hapo. Watu kuchukulia kawaida tena hadi kuleta mzaha ni kipimo tosha cha kiasi gani maadili yetu hayapo sawa kwa kiwango kikubwa kama tulivyozoea kusikia kwa mababu zetu. Japo hata wao ndipo athari zilipoanzia ila hakukuwa na mitandao kuchagiza hayo masuala.
Hivyo ni kweli kabisa hiyo midoli inaathari,watu wapende kukiri ama wasipende na wadhihaki kwamba unateseka kwa kuona midoli. Na kuthibitisha hilo hata wanayoyatumia kama display ya products zao wanaelewa target yao ni hiyo kushawishi watu. Na vina uhusiano kati ya sanamu za ulaya na magharibi zinazoonyesha maumbile na hii midoli ya kwetu sema watu ni wavivu kufatilia malalamiko ya watu wa ulaya juu ya masanamu hayo na pengine hufikia hatua hata kujaribu kuyaharibu kwa kuyavunja. Ni sisi tu ndo hupenda kupiga nayo picha ili kuonyeshea watu kama kielelezo cha kufika ulaya!
Wizara na Mama Gwajima kama inahusika na hili,nalo ilitizame kwa namna ya kipekee. Sio njia pekee ya kufanya bishara.